Saturday, May 19, 2018

HALI YA UPATIKANAJI WA DAWA MKOANI MBEYA NI ASILIMIA 91.5


 Ofisa Mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mbeya, Rhoda Joseph (kushoto) na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilembo, Dk. Bwire Biseko (kulia), wakihesabu dawa wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kituo hapa jana wilaya ya Mbeya Vijijini. Katikati ni mwanakamati ya Afya wa Kijiji cha Ilembo.
 Ofisa Mauzo wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Mbeya, Rhoda Joseph, akimkabidhi dawa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kijiji cha Ilembo wakati wa zoezi la kukabidhiwa dawa hizo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilembo, Sk.Bwire Biseko.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ilembo, Sk.Bwire Biseko akiangalia dawa hizo baada ya kukabidhiwa.
 Baadhi ya wafanyakazi wa MSD Kanda ya Mbeya wakionesha ishara ya mshikamano baada ya kuandaa mzigo wa dawa kwa ajili ya kwenda kuzisambaza kwenye vituo vya afya mkoani Mbeya.
 Baadhi ya wafanyakazi wa MSD Kanda ya Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuandaa mzigo wa dawa kwa ajili ya kwenda kuzisambaza kwenye vituo vya afya mkoani humo.


Na Dotto Mwaibale, Mbeya

UPATIKANAJI wa dawa na vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani Mbeya umefikia asilimia 91.5 kwa mwezi huu wa Mei, kutokana na ongezeko la bajeti ya dawa kwa mwaka fedha 2017/2018.

Imeelezwa katika mwaka huo wa fedha bajeti imeongezeka kwa asilimia 20.6  kwa hospitali za wilaya na asilimia 51 kwa zahanati na vituo vya afya.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt.Yahya Msuya ameeleza hayo wakati maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) walipotembelea wateja wa vituo vya Afya vitatu, vya Wilaya ya Mbeya vijijini wakati wa kusambaza dawa za mgawo wa mwisho wa mwaka wa fedha wa 2017/2018. 

Dkt. Msuya alisema ongezeko la asilimia 91.5 la upatikanaji wa dawa umeimarisha huduma za afya na na kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu kukosekana kwa dawa.

"Hospitali ya Rufaa ya Mbeya inahudumia wagonjwa wapatao 400 kwa siku; upatikaji wa dawa kwa sasa ni wa uhakika na uwepo wa maduka ya MSD  ni chachu ya kuimarika kwa huduma," alisema.

Alisisitiza kuwa utekelezaji wa agizo la serikali, la kutoa dawa za malaria bure kwa wananchi pamoja na dawa za msaada katika vituo vya afya na hospitaliti linafanyika.

Mfamasia wa Wilaya ya Mbeya, Apolinary Mwakabana alisema  pamoja na upatikanaji wa dawa kuridhisha kwa asilimia 91.5, jitihada zinahitaji ili kuwa na dawa zote, kwani  asilimia 9 ya dawa zinazokosekana hulazimika kuzitafuta nje ya bohari.

Alisifu ushirikiano wa kikanda uliopo kati ya halmashauri na MSD katika huduma hususani  kukiwa na mahitaji ya dharula.

Naye Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Ilembo kilichopo Mbeya vijijini Sk.Bwire Biseko, alisema kwa siku kituo hicho kinahudumia wagonjwa 107 kutoka vijiji 10, vyenye wakazi zaidi ya wakazi 17,000.

Alisema uboreshaji wa huduma za afya katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarisha uchumi na huduma za afya kwa kuwa watu wengi hawamudu gharama za matibabu kutoka nje ya hospitali.

Ubia Enock ni kati ya wakazi ambao walijitokeza katika kamati ya afya ya Kijiji cha Ilembo kushuhudia makabidhiano ya dawa hizo ambapo alisisitiza haja ya serikali kuboresha huduma kwa watu wanaotumia bima za afya.

Wednesday, May 9, 2018

WAKULIMA NJOMBE WAFURAHIA MBEGU BORA YA MUHOGO WAWASHUKURU WATAFITI SERIKALI

 Na Calvin Edward Gwabara, Njombe

WAKULIMA Mkoani Njombe wamewashukuru watafiti na Serikali kwa kuwezesha kupatikana kwa mbegu bora za muhogo ambazo zinauwezo wa kustawi kwenye maeneo ya baridi hasa nyanda za juu kusini baada ya utafiti  wa mwaka mmoja ulifanywa na watafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo cha Mikocheni MARI na chuo kikuu cha Dar es salaam.

Wakulima na wakazi wa kata ya Lupembe Mkoani Njombe wakifurahia mavuno makubwa ya mbegu za Muhogo zinazostawi kwenye maeneo ya baridi kali.

Wakiongea kwa furaha wakati wa zoezi la kuvuna mihogo hiyo ambayo ilipandwa mwaka mmoja uliopita wakulima hao wamesema sasa wamepata zao la biashara la uhakika baada ya zao la la chai kusumbua biashara yake .

Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake bwana Mapambano Luhongori Mkazi wa kijiji cha Lupembe wilaya ya njombe mkoani humo amesema kuwa Zao la Muhogo sasa litakuwa mkombozi kwa wakulima wengi ambao wamekuwa na shauku ya kulima zao hilo ili kuweza kunufaika na fursa kubwa ambazo wanazipata wakulima wa mikoa mingine kama vile Mara, Geita na Pwani.

‘’ Kutokana na uhitaji na soko kubwa la muhogo mkoani njombe nimejaribu mara kadhaa kulima zao la muhogo bila mafanikio lakini siamini macho yangu leo kuona katika eneo hilihili ambalo tulipanda mbegu hizi bora za watafiti kwenye shamba darasa imetoka mihogo mingi na mizuri kiasi hiki, ila nimegundua kuwa mbegu tulizokuwa tunatumia za kienyeji hazifai ukanda wetu’’ Alisema Luhongoli mkulima kutoka mkoa huo.

Mtafiti kiongozi wa Utafiti huo Dkt. Joseph Ndunguru akifafanua jambo kwa wakulima mara baada ya kuvuna baadhi ya mashina hayo kwenye kila aina 75 walizopanda eneo hilo.
Kwa upande wake Bi Rehema Malekela ambaye pia alishiriki kuanzia mwazo wa utafiti mpaka wakati huu wa kuvuna amesema kilimo cha zao hilo kilikuwa kidogo sana ambapo familia zimekuwa zikilima mashina machache kuzunguka nyumba kwaajili ya vitafunywa vya chai tu baada ya kuona zao hilo haliwezi kuwapatia tija kama wakulima wa maene mengine nchini.

Bi Malekela ameongeza kuwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani waislamu hupata shida sana kupata muhogo na hivyo kuwalazimu baadahi ya wafanyabiashara wengi kwenda kufuata mihogo kwenye mikoa mingine inayozalisha zao hilo kwa wingi na kuja kuiuza mkoani humo kwa bei kubwa.

“ Kwakweli ukifunua moyo wangu na moyo wa kila mtu unayemuona hapa aliyekuja kushiriki zoezi hili utaona furaha isiyo na kifani ndio maana unaona tumejitokeza kwa wingi watu kutoka Tarafa nzima kuja kushuhudia kupatikana kwa zao linguine la biashara kwenye eneo letu” Alisema Bi. Malekela kwa niaba ya wakina mama wengine.


Mamia ya wakulima na wakazi wa Kata ya Lupembe na maeneo mengine waliojitokeza kuangalia matokeo hayo ya utafiti kuona kama wanaweza kulima Muhogo kwenye ukanda huo wa baridi kali.

Aliongeza kuwa kingine kikubwa wanachowashukuru watafiti hao ni kuwaahidi kuwapelekea mbegu hizo kila mkulima kupitia vikundi vyao na kuwafundisha namna ya kuchakata muhogo na kupata bidhaa mbalimbali kama vile clips,Biskuti,Maandazi na aina zingine za vyakula ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Kwa upande wake mtafiti kiongozi wa utafiti huo kutoka Kituo cha utafiti wa Kilimo Mikocheni MARI Dkt. Joseph Ndunguru amesema kuwa kwa muda mrefu wakulima kwenye maeneo ya baridi wamekuwa hawalimi zao hili hali ambayo imekuwa ikiwakosesha fursa mbalimbali zitokanazo na zao hilo ambazo wakulima wa maeneo yenye joto wanazipata kwa kuzalisha muhogo.

Amesema katika utafiti huo wamepeleka mbegu aina 75 za muhigo katika maeneo matatu ya utafiti huo ambayo ni Mkoa wa  Njombe ambapo wanaangalia aina za muhogo kati ya hizo ambazo zitastawi na kuvumilia baridi hadi la nyuzijoto 16 -22C na eneo linguine ni mkoa wa Dodoma kuangalia aina ya mihogo itakayoweza kuvumilia ukame na Mkoa wa Pwani katika eneo la Chambezi ambapo wanaangalia changamoto ya joto na magonjwa.


Dkt. Joseph Ndunguru na Dkt. Gladness Temu wakiwa wamebeba moja ya mashina ya mbegu hizo yaliyovunnwa hivi karibuni katika eneo la Chambezi ambalo walikuwa wakiangalia mbegu zinazostawi kwenye eneo la Joto na magonjwa.

‘’ Kwakweli tumepata mafanikio makubwa sana kwa mfano kwa Mkoa wa Njombe kwenye baridi ,aina 47 kati ya aina 75 tulizopanda kwenye shamba hili kwenye eneo lenye bardi zaidi tum  eona zimefanya vizuri sana nah ii ni kutuonyesha kuwa sasa wakulima wa eneo hilo wanaweza kunufaika na kilimo hiki’’ Alisema Dkt. Ndunguru.

Mtafiti huyo ameongeza kuwa pamoja na kufanya vizuri kwa aina hizo 47 lakini wamegundua kuwa katika eneo hilo shina linatoa mihogo mingi sana lakini haiwezi kukomaa kwa muda wa mwaka mmoja kama ilivyo kwenye maeneo yenye joto na hivyo kuhitaji muda zaidi ya mwaka mmoja ili inenepe na kukomaa vizuri.

Kwa upande wake mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt. Gladness Temu ambaye ni mtafiti katika mradi huu amesema kuwa katika kipindi chote cha utafiti huo wamekuwa wakitembelea shamba hilo na kuchukua takwimu mbalimbali muhimu ambazo zitakuja mwishoni kusaidia katika hitimisho na mapendekezo kwa wakulima.

Dkt. Gladness Temu akiinua shina la Muhogo walilovuna huko Chambezi hivi karibuni.

Amesema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na kuangalia kama mbegu hizo zinashambuliwa na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia magonjwa mabayo ni hataro sana kwa mihogo kwa sasa lakini hayakujitokeza kabisa kwenye shamba hilo hali ambayo inawafanya kuamini uzalishaji utakuwa mkubwa sana katika eneo hilo.

‘’ Katika kuhakikisha magonjwa hayo hayatokei kabisa tutawaletea mbegu bora na safi ili waanze kilimo hicho bila magonjwa nah ii itawasaidia sana sasa kuwa wazalishaji wa mbegu za muhogo wazuri maana eneo lao halina magonjwa hayo kwa sasa’’ Alisistizia  Dkt. Gladness.

Mradi huu wa utafiti unafanywa kwa kushirkiana na nchi Tatu za Tanzania,Kenya na Hispania kwa ufadhili wa shirikala la maenedeleo la umoja wa Ulaya kupitia kwa shirikala la chakula na kilimo duniani  FAO.

Baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha utafiti wa Kilimo Mikocheni cha jijini Dar es salaam MARI wakifurahi wakati waliposhirikiana kuinua shina moja la Muhogo huko Chambezi Bagamoyo.


Wednesday, May 2, 2018

GGM na TACAIDS kuzinduwa Kilimanjaro Challenge 2018



















Na Mwandishi Wetu

MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018), litakalo kwenda sambamba na kuendesha harambee kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Akizungumzia tukio hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko alisema shughuli hiyo itafanyika Mei 4, 2018 katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam. Dk. Maboko alisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka 2017 baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro. Aidha aliishukuru na kuipongeza kampuni ya GGM kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa kuchangisha fedha kupitia Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS, fedha ambazo alisisitiza zimekuwa na mchango mkubwa katika mapambano kudhibiti ugonjwa huo maeneo mbalimbali. Akifafanua zaidi, Dk. Maboko alisema Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS, ni mfuko unachangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU). Aliongeza kuwa, Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo. Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro. Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17. “Mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii. Lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu. Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI." " TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu. Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko. Naye Makamu wa Rais miradi endelevu wa Kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo akizungumza alisema, watoto watakaoshiriki katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana na tatizo la VVU/ UKIMWI wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma Orphanage Center kilichopo Geita. Bw. Shayo alibainisha kuwa, changamoto kubwa inayotokana na janga la UKIMWI ni pamoja na maelfu ya watoto yatima wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo. “Aidha, pia kuna tatizo linaloikabili jamii sasa ambapo baadhi yao wanawatenga na kukataa kuishi na watu wenye maambukizi ya VVU/ UKIMWI, kutokana na tatizo hilo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, umeamua kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM,” alisema Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo. “Huu ni mwaka wa 17 sasa tangu Kili Challenge ianze. Pia zaidi ya watu 750 kutoka pande mbalimbali za dunia wameshiriki. Taasisi zaidi ya 40 zimefaidika kutokana na utunishaji wa mfuko huu kwa sababu taasisi ambazo hazina fedha za kuendesha kampeni na shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI zimekuwa zikifaidika na mfuko huu. Pamoja na mambo mengine, watoto waliopoteza wazazi wao sasa wanaweza kutabasamu tena kutokana na uangalizi pamoja na upendo wanaoupata kutokana na mfuko huu. “Tunapenda pia kutambua ushirikiano wa kampuni na taasisi mbalimbali kama vile ACACIA, AKO, Mantrac, NSSF, PUMA, TOYOTA, Prime Fuels, Coastal Aviation, Airtel, Capital Drilling, PPF, Serena Hotel, Geita Power Limited, SGS na wadau wengine tunaoshirikiana nao. Tunawashuruku kutokana na ushirikiano wenu katika mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI hivyo, tunaweza kufurahia mafanikio haya kwa kuwa na mradi endelevu,” aliongeza Simon Shayo. Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Bw. Mrisho Mpoto ameileleza jamii ya Tanzania kuacha kuwa tegemezi kwa sababu ina uwezo wa kujisimamia kwa kutumia vyombo vya habari, na watu wenye ushawishi mkubwa na kwa pamoja UKIMWI unaepukiki. Tanzania inaweza kufikia malengo ya kuwa huru dhidi ya maambukizi ya UKIMWI kufikia mwaka 2030 kama tukishirikiana kwa pamoja katika vita hii. Aliongeza kuwa, ili kushiriki Kili Challenge, muhusika anaweza kuchangia mfuko huu kwa kujifadhili au kumfadhili mwingine kupanda au kuendesha baskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro. Kuwa sehemu ya mafanikio. Kwa mawasiliano zaidi au kutoa mchango wasiliana nasi kupitia email: GGMkilichallenge@anglogoldashant.com, au tovuti www.geitakilichallenge.com. Geita Gold Mine na TACAIDS tunatumia mwamvuli huu wa Kilimanjaro Challenge katika kuelimisha jamii kuhusu janga hili la VVU/Ukimwi na tunatarajia siku moja Tanzania itatangaza kuisha kwa maambukizi ya VVU/ UKIMWI. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.geitakilichallenge.com Mwisho.

Thursday, April 26, 2018

KONCEPT Yawajengea uwezo wanafunzi kidato cha sita 'Kibiti Boys'

Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys. Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla. Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys. Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla. Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Wanafunzi wa kidato cha sita wapatao 451 wa  shule ya wavulana Kibiti Boys  iliyopo wilaya  ya kibiti  Mkoani  wakisikiliza kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele alipotembelea shule hii mapema wiki katika kuwajengea uwezo katika maandalizi yao ya mitihani ya mwisho na pia kuwapa dondoo za mafanikio katika maisha kwa ujumla.

Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa Mkurungezi wa KONCEPT  Krantz  Mwantepele  Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti wakionesha kuwa wamehamasika na nasaha zilizotolewa na Mkurungezi mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.
Mkuu wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys, Dismas Njawa akifafanua jambo kabla ya kufunga kongamano hilo lililoendeshwa na Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele. Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla. Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT akifurahi jambo na Mkuu wa shule ya wavulana Kibiti Boys  Dismas Njawa mara baada ya kumaliza kongamano. Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.




Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiwa katikaa picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys mara baada ya Kongamano.Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa  shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.



Wednesday, April 25, 2018

PUMA YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI



 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbande, Dar es Salaam, Nasri Mustafa akumuonesha Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia) picha aliyoichora na kushinda tuzo  ya usalama barabarani 2017, wakati wa uzinduzi wa mpango wa Puma wa  mafunzo ya ya usalama barabarani kwa wanafunzi, jana katika Makao Makuu ya Puma, Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania.Wa pili kushoto ni SajentiHussein Ramadhan Mwalimu wa Trafiki Makao Makao Makuu ya Usalama Barabarani.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini. 

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.

AKizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu,  alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.

Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria,  bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.

"Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;

"Hivyo kwa kuwafundisha usalama barabarani tunawapa ufahamu wa kuwajenga katika matumizi salama ya barabara...hiki ndicho kipaumbele chetu."

Alifafanua kwamba baada ya mafunzo  wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchora michoro ya usalama barabarani na mshindi pamoja na shule anayotoka wanazawadiwa.

Corsaletti alisema kampuni hiyo ilianzisha mafunzo hayo mwaka 2013 na imeendelea kufanya hivyo hadi sasa kwa kufikia shule 47 na kuwafundisha wanafunzi 60,000 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Geita.

Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa kiwango cha ajali katika shule zilizopatiwa mafunzo kimepungua.


Corsaletti, alisema kampuni hiyo itaendelea na kampeni ya usalama barabarani na kuahidi kufanyakazi pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani, maofisa kutoka manispaa au wilaya zinakotoka shule  zilizochaguliwa ili kuhakikisha lengo linatimia.



 Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kulia), akimshukuru Mbunja kwa kuzindua mpango huo.
 Matibu Mbunja aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Poilisi cha  Usalama Barabarani Tanzania, akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango huo.



Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange  akiiweka sawa picha iliyochorwa na Mwanafunzi Nasri Mustafa na kushinda tuzo ya Usalama barabarani 2027
 Shemu ya wadau wa usalama barabarani
 Baadhi ya walimu na wanafunzi waliohudhuria uzinduzi huo
 Wanahabari wakiwa kazini
 Sehemu ya wadau wa usalama barabarani
 Mwanafunzi Nasri Mustafa akionesha picha aliyoichora ya usalama barabarani. Picha hiyo ilishinda tuzo ya kwanza 2017

 Wadau wa usalama barabrani wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi a mpango huo
 Mgeni rasmi, Mbunja na Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti wakiwa na furaha
  Meneja Mkuu wa Puma,Corsaletti, Akisalimiana na wadau baada ya uzinduzi
 Wakiwa katika picha ya pamoja


Friday, April 13, 2018

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA





Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuhusu mikakati wa bandari hiyo kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike.



Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike.




PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huo.


Mwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huo.


Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga

MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa yaliyofanyika.

Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji .

Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo kusafirisha bidhaa zao.

“Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama.

Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika.

“Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia shehena inayowasili “Alisema.

Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika kufanya kazi hizo kwa wakati (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Wednesday, April 11, 2018

Tigo yawazawadia washindi zaidi wa Nyaka Nyaka Bonus


Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Yusra Ali Ramadhani (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 83 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. 



Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Hamisi Mohammed Yusuph (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00#  tangu kuanza kwa promosheni hiyo. 




Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael  (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo. 




Baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus wakitazama simu zao aina ya Tecno R6 walizoshinda baada ya kukabidhiwa zawadi hizo jana katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo.  
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakabidhi washindi 84 wa wikii hii katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus  iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam.


  • Zaidi ya simu 300 na bonasi za intaneti bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Aprili 10, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imewazawadia wateja wake 84 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
‘Katika promosheni hii murwa, Tigo inatoa bure jumla ya simu janja 12 kila siku.  Pamoja na haya, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter,’

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo, ambapo kufikia sasa tumewazawadia wateja 756 simu hizi janja zenye uwezo wa 4G’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.


Kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.


Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...