[caption id="attachment_71549" align="alignnone" width="640"]
Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Tuesday, May 10, 2016
Tozo Daraja la Nyerere Kuanza Rasmi Jumamosi
[caption id="attachment_71549" align="alignnone" width="640"]
Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira, Atembelea Kambi Tiba ya GSM Dodoma
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI, ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.
Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza, ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi kila mwaka.
"Nimeshtushwa na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo, hongereni sana", alisema Mavunde.
Mavunde amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja tu kubwa na ya msingi ya utanzania.
PICHANI JUU: Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI Shannon Kiwamba(kushoto)
Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini
Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
Mavunde akibadilishana mawazo na mratibu wa kambi tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma, wanaosikiliza ni Kibwana Matukio kutoka GSM, na Mganga mkuu wa mkoa Bw Jordan Rugimana
Mgodi wa Bulhanhlu Waingia Makubaliano na Taasisi ya Benjamini Mkapa Kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto Shinyanga
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika wilayani Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa (nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.
Na Dixon Busagaga
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko
wilayani Kahama umetiliana saini hatii ya makubaliano ya Dola 200,000 sawa na shilingi
Milioni 440 za Tanzania na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) kwa ajili ya
mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto katika wilaya ya
Msalala mkoani Shinyanga
Mgodi
Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia na Taasisi ya Benjamin
W. Mkapa (BMF) wamesaini hati ya makubaliano ili kushirikiana katika kutekeleza
mradi wa miaka miwili unaolenga kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto
katika jamii .
Mgodi wa Bulyanhulu kupitia Mfuko wa
Maendeleo wa Acacia utatoa kiasi cha dola za Kimarekani 200,000 kusaidia awamu
ya pili ya mradi wa BMF utakaosaidia kuboresha huduma ya vituo viwili vya afya
wilayani humo, Kituo cha Afya cha Bugarama na Zahanati ya Kakola kupitia mradi
huo.
Mradi huo katika vituo tajwa
unatarajiwa kunufaisha wananchi 321,852 katika Halmashauri ya Msalala ambapo makubaliano
hayo ya miaka miwili yanaanzia, 01 April 2016 hadi 30 Machi 2018.
“Mgodi wetu unaendesha shughuli zake
katika halmashauri ya Msalala hapa mkoani Shinyanga na sehemu ya uwajibikaji
wetu kwenye jamii, kupitia mkakati wa mipango endelevu kwenye jamii na kusaidia
mikakati ya uboreshaji wa sekta ya afya kwa ajili ya jamii inayozunguka mgodi.”alisema
Graham Crew.
“Ushirikiano huu na Taasisi ya BMF
umekuja wakati muafaka ambapo BGML imewekeza katika miundombinu ya kuipandisha
hadhi zahanati ya Bugarama kuwa kituo cha afya na pia kumalizia ujenzi wa
Zahanati ya Kakola.” Aliongeza meneja huyo mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew.
Awamu ya pili ya Mradi wa BMF
inalenga kutekeleza mradi utakaoboresha huduma za HIV/AIDS, huduma za mama na
mtoto kwa kuongeza upatikanaji wa wataalamu wa afya na kuboresha miundombinu ya
kutolea huduma za afya.
Afisa Mtendaji Mkuu wa BMF Dk Ellen
Mkondya Senkoro amesema; “Takwimu zinaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga una
maambukizi kwa asilimia 7.4% ambapo kiwango kikubwa kipo katika halmashauri ya
Msalala kutokana na shughuli za uchimbaji madini hasa uchimbaji mdogo mdogo.”
“Kiwango hiki kimeendelea kuwa hivyo
tangu mwaka 2007/2008 hadi 2011/2012 ingawa kiwango cha maambukizi nchini
kimepungua kutoka asilimia 5.7% hadi 5.1% hivyo sehemu hii inahitaji hatua
maalumu. “alisema Dkt Mkondya.
Alishukuru Kampuni ya ACACIA kwa msaada huo na kwamba utasaidia kwenye
utekelezaji wa uboreshaji wa mifumo ya kukabiliana na tatizo la Virusi vya
Ukimwi, huduma za uzazi na watoto kwa kuongeza rasilimali watu ya watalaamu wa
afya, uendelezaji wa miundombinu na kujengea uwezo maeneo yanayohitaji ufanisi
zaidi.
Tangu mwaka 2013 Taasisi ya
Benjamin William Mkapa (BMF) imekuwa ikishirikiana na Acacia kupitia Mfuko wake
wa Acacia Maendeleo Fund katika kutekeleza sehemu ya miradi ya awamu ya pili ya
mfuko wa taasisi ya BMF katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na Halmashauri
iliyokuwa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa Acacia:
Mfuko wa Maendeleo wa Acacia maarufu
kama Acacia Maendeleo Fund ulianzishwa mwaka 2011 kama sehemu ya dhamira katika
kuboresha maendeleo endelevu katika jamii kwenye maeneo tunayofanya kazi. Hadi
sasa tumefanikiwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 35.0 katika miradi 150
kwenye maeneo mbalimbali.
Misaada kutoka kwenye mfuko huu hutoa
kipaumbele kwa vitega uchumi vinavyosaidia maendeleo ya jamii, ujengaji wa
uwezo, sekta ya afya, elimu, maji, mazingira katika maeneo tunakoendesha
shughuli zetu.
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ilianzishwa April 2006
na Rais Mtaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin W.
Mkapa, taasisi hii isiyo ya kiserikali ina dhamira ya kuboresha afya na hali za
watanzania hasa katika maeneo yaliyoko vijijini kwa kutekeleza miradi yenye
kutoa matokeo.
Kilimo Hifadhi cha Nyanya katikati ya Dar es salaam
Dk. Sophia Mlote, mkazi wa Kinyerezi Zimbili jijini
Dar es Salaam akiweka sawa vifaa mbalimbali kwenye banda lake la kilimo ambamo
amepanda nyanya. Dk. Mlote anatekeleza kilimo hai kupitia mradi wa Green Voices
unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa ambayo inaongozwa na
Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María
Teresa Fernández de la Vega. (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com).
PSPF Yatoa Msaada Vifaa vya Shule kwa Wanafunzi Waishio Mazingira Magumu
Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta
Mnyamani akiwaelimisha wanafunzi wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyoko mkoani
Geita kuhusiana na Mfuko wa Penseheni wa PSPF na lengo la kusaidia jamii katika
hususan katika masuala ya elimu. Mabegi yenye vifaa vya kusomea
yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio
kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Wanafunzi
wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia
msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni
hapo.
Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta
Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani)
pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia
jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.
Wanafunzi waishio katika mazingira
magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa
mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Wanafunzi waishio katika mazingira
magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa
mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Uendashaji wa PSPF Mkoa wa Geita, Bw. Noel
Tuga, akiwapa maelezo wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya
msingi Nyansalwa namna ya kutumia vifaa vilivyopo kwenye mabegi PSPF iliyotoa
msaada. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF
kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi
Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka,
Bw. Jumanne Masumbuko, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake
kwa masaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni
wa PSPF.
Monday, May 2, 2016
NSSF YADHAMINI SIKU YA MADANSA DUNIANI
Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara
ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim
Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya
siku ya madansa duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es
Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisa Mwandamizi Masoko
na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto) akimkabidhi fulana, Jumanne Mnola alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa
duniani iliyofanyika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto), akimkabidhi fulana mmoja wa wateja wao, Said Ally, alipotembelea
banda lao wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika kwenye
viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko
na Uhusiano (Nssf), Amina Mbaga akigawa vipeperushi kwa baadhi ya
wananchi waliotembelea banda lao.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Faides Mdee, akigawa vipeperushi
kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika uzinduzi wa siku ya
madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dares Salaam, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na NSSF.
Wafanyakazi wa NSSF
wakimkabidhi fulana mteja wao, Antela Salumu (katikati).
Ofisa wa
NSSF, Innocent Shao, (kulia) akiwaandikisha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF walipotembelea banda la NSSF katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyoadhimishwa kwenye
viwanja vya TCC Club Chang’ombe na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa
uandikishaji NSSF, Amina Kisawaga (kulia) akitoa maelezo kwa mteja alietembelea
banda lao Fumbwe Juma, katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Picha ya pamoja.
MBUNGE WA VUNJO ATEMBELEA BARABARA YA KILEMA NA KUJIONEA UHARIBIFU WA MVUA
Na Dixon Busagaga
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea Hospitali ya wilaya ,Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule iliyo jirani na barabara hiyo wakitizama sehemu ya korongo lililopo katika barabara hiyo ambayo ni tegemeo kwa Chuo cha Ualimu Mandaka,Seminari ya Mtakatifu James ,shle za sekondari pamoja na msingi.
Baaadhi ya madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakipita katika barabara hiyo ambapo kwa
sasa nauli ya kupandisha abiria kwenda Hospitali ya wilaya ya Moshi,Kilima imepanda kutoka kiasi cha sh 3000 hadi 6000 .
Moja ya Magari yanayotumia barabara hiyo likijaribu kupita katika barabar hiyo ambayo imeharibika vibaya kutokana na maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya barabara hiyo likionekana korongo ambalo limeanza kumegwa na maji na kuhatarisha kukatika kwa mawasiliano katika baina ya vijiji 12 ambavyo wakazi wake wanatumia barabara hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akishirikiana na wakulima wa Kijiji cha Itinje Wilaya y...


















