Thursday, March 17, 2016

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

01
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
1
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni na mbunge wa Kigoma mjini  Zitto Kabwe wakati wajumbe wa kamati hiyo walipowasili katika ofisi za mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
2
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
3
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.

6
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akizungumza katika mkutano huo huku Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo, kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Mbunge wa Kigamboni Mh. Dk. Faustine Ndungulile.

8
Baadhi ya wakurugenzi wa vitengo NHIF wakifuatilia mambo kadhaa wakati wa uwasilishaji wa ripoti hiyo mbele ya Makamti ya Bunge Maendeleo ya Jamii, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Rehani Athumani na Ali Othman Mkurugenzi wa TEHAMA NHIF.

11
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo wakati wa mkutano huo kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando na katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati na Mbunge wa jimbo la Buseka Dk. Raphael Chegeni.
12
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo mbele ya kamati hiyo huku wabunge wakifuatilia.
13
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Mhando akitoa ufafanuzi wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa na kamati hiyo pamoja na uongozi wa NHIF.
15
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kilichoanzishwa kwa ajili ya kuwafanya wateja kupata taarifa mbalimbali kuhusu mfuko huo bila kulazimika kufika ofisini.
16
Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya akiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Michael Muhando wakati akielekea kukagua eneo linaohifadhi kumbukumbu za mfuko huo.

DK. MPOKI AZINDUA MPANGO KAZI WA TAIFA WA DAWA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi mkutano wa  Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2015) leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Henry Irundo na kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Muhamad Kambi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati) akionyesha taarifa ya  Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2015) baada ya uzinduzi   leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Henry Irundo na kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Muhamad Kambi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza  wakati wa uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2015) leo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa taarifa ya  Mpango kazi wa Taifa wa Dawa vifaa Tiba na vitendanishi kwa miaka mitano (2015-2015) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Lorietha Laurence-

ACCESS BANK WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM MTAMBANI

Meneja Masoko wa AccessBank Mr.Muganyizi Jonas Bisheko Akikabidhi Vifaa Mbalimbali kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum wanaosoma  shule ya Msingi Mtambani Iliyopo Boko Manispaa ya Kinondoni.

Benki ya Access Bank imetoa Msaada wa Wanafunzi Wenye Mahitaji maalumu wanaosoma Shule ya Msingi Mtambani Manispaa ya Kinondoni.Meneja Masoko kutoka Access Bank alisema Msaada huo ni sehemu ya faida ya Benki hiyo Ambayo Wnarudisha kwa Jamii ya Watanzania hivyo waliguswa na Changamoto Kubwa Zinazowakabili Wanafunzi hao ikiwwemo Ukosefu wa Miundo mbinu Rafiki kwajili ya Wanafunzi hao kama Madarasa vyoo na Vitendea kazi vingine.Akieleza zaidi Bw Muganyizi Jonas Bisheko Ameomba Makampuni Mbalimbali Kujitokeza Kuwasidia wanafunzi wao wenye mahitaji Maalum kwa lengo la kuwezesha kupata elimu Bora kawa Wanafunzi wengine.Benki hiyo imetoa Vifaa mbalimbali vya kujifunzia pamoja na Michezo kwajili ya kusaidia kutatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao
Msaada huo unajumuisha vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya kujifunzia pamoja na Michezo,akieleza zaidi Meneja Masoko wa Benki hiyo amesema Accessbenk imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii ya watanzania hasa kupitia sekta ya elimu kwa kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo kama vile ukosefu wa vifaa na mazingira rafiki ya kuwezesha kutoa elimu bora
Mwalimu wa shule ya Msingi mtambani anayehusika na Kitengo cha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum akitoa neno la shukrani Mara baada ya Kupokea Msaada huo.Ameishukuru sana Accessbenki kwa msaada wao amesema kwa kiasi utatua Changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Wanafunzi Wenye mahitaji Maalum kutoka Shule ya msingi mtambani walionufaika na msaada huo kutoka accessbenki.

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA BANDARI DAR ES SALAAM


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akitoa ufafanuzi wa gati zilizo katika bandari hiyo  kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlakaya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akitoa ufafanuzi kuhusu namna Kamera zinazoendelea kufungwa katika Bandari hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, waliotembelea Mamlaka hiyo .


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Aloyce Matei, akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu eneo itakapo jengwa gati ya 13 na 14.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Bandarini (TICTS), Paul Wallace akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu namna kampuni hiyo inavyohudumia makontena katika bandari ya Dar es Salaam.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sehemu ya Uchukuzi, Dk. Leornard Chamuriho akitoa taarifa ya namna Wizara inavyosimamia Mamlaka zilizo chini yake, wakati Kamati ya Bunge ya MIundombinu, ilipo tembelea Mamlaka ya Bandari (TPA).

Saturday, March 12, 2016

TAWLA YAENDESHA SEMINA KWA WANAHABARI JUU YA AFYA YA UZAZI NA CHANGAMOTO ZAKE

Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga akifungua mafunzo kwa wanahabari hawapo pichani yanayolenga kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya haki ya afya ya uzazi Changamoto wanazokutana nazo na namna ambavyo matumizi ya sheria za kimataifa kama Maputo Protocal yataweza kupunguza Chanagamoto hizo, Semina hiyo ya siku mbili ilikuwa ikifanyika Luther House Azania Front jijini Dar es salaam na imemalizika leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga akifungua mafunzo kwa wanahabari hawapo pichani yanayolenga kujenga uelewa kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuala ya haki ya afya ya uzazi Changamoto wanazokutana nazo na namna ambavyo matumizi ya sheria za kimataifa kama Maputo Protocal yataweza kupunguza Chanagamoto hizo, Semina hiyo ya siku mbili ilikuwa ikifanyika Luther House Azania Front jijini Dar es salaam na imemalizika leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU
2
Wanahabari wakimsikiliza Afisa Uchechemuzi wa Shirika la Wanasheria wanawake la TAWLA Bi. Sime Bateyunga wakati akifungua semina hiyo jana.
3
6
Afisa Mipango wa TAWLA Bi. Sara Kinyaga kulia akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuendesha mafunzo hayo kwa waandishi wa habari leo.
7
Maofisa wa TAWLA pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja nmara baada ya kumalizika kwa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.

Friday, March 11, 2016

DK. POSSI AZINDUA KITABU CHA JINSI YA KUONDOKANA NA UMASIKINI

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi ( wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho nkwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii(UDSM) Prof Godius Kahyarara. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi ( wa pili kulia) akionesha kitabu pamoja na Mhariri Mkuu wa kitabu hicho nkwa washiriki na waandishi wa habari Prof Lician Msambichaka katika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli na kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sayansi na Jamii(UDSM) Prof Godius Kahyarara.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi (wa pili Kushoto) akionesha kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi katika uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dare s Salaam Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli wa pili kulia ni Prof Lician Msambichaka Mhariri Mkuu wa kitabu hicho na kulia ni Prof Delphin Rwegasira kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[/caption] Na Raymond Mushumbusi ,MAELEZO Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Dkt Abdallah Possi amezindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dkt Abdallah Possi amesema amefurahishwa sana kuona wasomi wa Tanzania wakijitolea muda wao na nguvu zao kushirikiana na Serikali katika kuondokana na umasikini ili tuelekee katika ustawi wa taifa. “ Kitabu hiki kimekuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya tano imejikita katika mapinduzi na maendeleo katika sekta ya viwanda ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi nyingi duniani kwa sasa, hivyo tunaahidi kushirikiana na watafiti mbalimbali katika kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazotukabili katika kuondokana na umasikini,”Alisema Dkt. Possi. “ Nimekisoma hiki kitabu kwa ufupi na kuona ni jinsi gani kitaweza kutusaidia katika mapambano dhidi ya umasikini lakini napenda kuwapa changamoto kuwa kazi hii ya kupambana na umasikini isiwe katika vitabu tu na sera bali iwe katika utekelezaji” Aliongeza Dkt Possi. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akielezea jambo kwa washiriki na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mara baada ya kuzindua kitabu  kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akielezea jambo kwa washiriki na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt Jehovanes Aikaeli.[/caption] Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa watafiti wa mambo ya uchumi wanatakiwa kuwashirikisha pia watu wenye ulemavu katika harakati za kuondokana na umasikini kwa kuwashirikisha katika uundwaji wa sera na utekelezaji wake katika kuleta maendeleo ya taifa. Aidha Mhariri mkuu wa kitabu hicho, Prof Lucian Msambichaka amesema dhima kubwa ya kitabu hicho ni utekelzaji wa Sera,Mipango, Sheria na majukumu mbalimbali yahusuyo maendeleo kwa taifa na kuongeza kuwa kitabu hicho pia kimetoa njia bora na muafaka wa kukuza sekta ya viwanda, kuboresha huduma za jamii, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na jinsi gani Tanzania inavyoweza kunufaika na maliasilia zake katika kujileta maendeleo. Kitabu hiki kimeandaliwa na Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kudhaminiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kimeshirikisha waandishi zaidi ya 20 na kina kurasa zaidi ya 400 ambazo zimeelezea kwa kina namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kuondokana na umasikini na kuelekea katika ustawi.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu  kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uchumi kutoka Idara ya Uchumi Chuo Kikuu cha Dar es salaam mara baada ya kuzindua kitabu kinachoelezea namna ya Tanzania inavyoweza kujiondoa katika umasikini na kuelekea kwenye ustawi uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO[/caption]

WATOTO CHINI YA MIAKA 5 KUNUFAIKA NA UPIMAJI WA AFYA BURE KUTOKA BANGO SANGHO

Bango Sangho
Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.
Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13 katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumzia huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa maendeleo ya taifa.
Alisema kupitia huduma hiyo madaktari watawapima watoto walio na umri chini ya miaka mitano afya ya kinywa, uzito, ukaguzi na ushauri wa lishe hivyo kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata huduma bure.
Ali Mzige
Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na waandishi wa habari.
“Tunataka kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.
Nae Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki Al Hilal alisema Bango Sangho kimekuwa chama ambacho kikisaidia jamii ya Tanzania katika sekta ya afya na wamekuwa wakitoa huduma ya kupima watoto bure walio na umri chini ya miaka mitano kwa mwaka wa tatu mfululizo.
Alisema ripoti ya afya Tanzania inaonyesha kuwa kuna watoto 81 wamekuwa wakipoteza maisha kati ya watoto 1,000 walio na umri chini ya miaka mitano kutokana na sababu mbalimbali ambapo wamekuwa hawapati huduma na kupitia huduma hiyo ya kuwapima bure watoto walio na magonjwa wataweza kutambulika.
“Tutafanya huduma ya kupima bure watoto walio chini ya miaka mitano na tutakaobaini wanamatatizo maalum ya kiafya tutawapa rufaa ili wakapate huduma ya matibabu,” alisema Dkt. Mzige.
Huduma hiyo ya kupima watoto walio na umri chini ya miaka mitano ilifanyika pia mwaka jana na watoto 289 walipimwa afya zao huku baadhi walikutwa na matatizo ikiwemo maambukizi ya mfumo wa njia ya mkojo UTI, Utapiamlo, kukatwa vimeo na wengine wakionekana kuwa na afya duni.
Husna Abdallah
Mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Zawadi Chogongwe
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Zawadi Chogongwe (kulia) akiuliza swali kwa wataalamu wa afya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...