Thursday, November 5, 2015

Dk. Magufuli, Mama Samia Wala Kiapo cha Urais Tanzania

Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akionesha mkuki na ngao kama ishara ya mamlaka mara baada ya kula kiapo leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Jopo la majaji wa Tanzania wakiongozwa na Jaji Mkuu, Othman Chande (hayupo pichani) wakielekea jukwaa la kiapo, ambapo Jaji Mkuu alimuapisha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Baadhi ya maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama na wageni waalikwa wakiwa katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Wageni mbalimbali walioshiriki sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Wananchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Wananchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Rais mteule Dk. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kula kiapo kuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.
Rais mstaafu wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (kushoto) na Makamu wake, Dk. Gharib Bilal (kulia) wakiaga wananchi mara baada ya kumaliza awamu yao.
Bendera ya Rais wa Tanzania ikipandishwa ikiashiria kuanza kwa utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Dk. Magufuli.
Baadhi ya marais wa nchi mbalimbali na viongozi wakuu wa nchi wakiwa katika sherehe za kiapo cha Rais Dk. John Magufuli.
Baadhi ya maofisa wa majeshi ya ulinzi na usalama wakitoa saluti kwa wimbo wa taifa leo...
Uwanjani sherehe za kiapo cha rais na makamu wake.
Gwaride...Kikosi cha bendera kikitoa heshima kwa rais kwenye sherehe za kiapo cha Rais na Makamu wake.
Wageni waalikwa kwenye sherehe za kiapo cha Rais wa Tanzania na Makamu wake.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo ameapishwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015. Dk. Magufuli amekula kiapo hicho leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru pamoja na Makamu wake wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiahidi kulitumikia taifa kwa uaminifu, unyenyekevu bila ubaguzi wowote.

Sherehe za kuapishwa kwa Rais Dk. Magufuli na Makamu Rais wake, Mama Suluhu Hassan zimehudhuriwa na marais wa nchi mbalimbali, viongozi wawakilishi kutoka mataifa anuai, mabalozi, viongozi wastaafu wa Serikali ya Tanzania, maofisa wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, wabunge wateule na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Miongoni mwa marais walioshiriki katika sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Congo (DRC), Joseph Kabila, Rais wa Zimbabwe, Robart Mugabe, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na viongozi wengine wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Aidha, Dk. Magufuli amekabidhiwa kijiti na Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ambaye anakwenda kupumzika baada ya kulitumikia taifa kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano alivyochaguliwa kuliendesha taifa la Tanzania. Licha ya uwepo wa mvua jijini Dar es Salaam tangu alfajiri ya leo sherehe za kiapo cha Dk. Magufuli zimehudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi walioanza kuingia uwanjani tangu saa kumi na moja ya asubuhi. Uwanja wa Uhuru ulifurika hivyo kuamriwa wananchi kuanza kuingia katika Uwanja wa Taifa ambao ulikuwa ukionesha matukio ya kiapo kupitia runinga kubwa zilizofungwa katika uwanja huo ambao nao ulifurika.

Watanzania wanamatumaini makubwa na Rais Dk. Magufuli kutokana na historia ya utendaji katika baadhi ya nafasi za uwaziri alioshika hapo nyuma, ambapo amekuwa akifanya vizuri kiutendaji kiasi cha kumpa jina la utani la 'Tingatinga' jina lililoendelea kuvuma hadi sasa. Tanzania inaingia katika historia ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwa ni nafasi ya juu ya uongozi wa nchi kushikwa na mwanamama tangu nchi ipate uhuru wake.

Monday, November 2, 2015

Mtoto Careen Modest Anahitaji Msaada Wako...!


Mtoto Careen Modest Kassuw pichani, ana umri wa mwaka mmoja, amezaliwa ana tatizo la Moyo ukiwa na matundu mawili na valvu zake nyembamba  zimebana kiasi  hivyo analazimika kusafirishwa kwenda India kwa matibabu.

Wazazi wa mtoto huyo wanaomba msaada wako wewe Mtanzania kwa atakayeguswa ili wafanikishe gharama za matibabu ya mtoto Careen ambayo ni Shilingi Milioni 30 zinahitajika ili kuokoa maisha yake.
Ewe Mtanzania, ewe mzazi tunaomba mchango wako wa hali na mali, kwa atakayeguswa tunaomba utume mchango wako kwa mama mzazi wa mtoto huyo Eunice kwa namba0713 034866 au kwa namba 0715 083055

Mungu awabariki wote mtakaochangia kwa njia moja au nyingine.

Saturday, October 31, 2015

Harusi ya Bwana Said na Mkewe Salma Ilivyofana Jijini Dar es Salaam...!

 Bwana Harusi Said akimnywesha Shampeni mkewe Salma wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Best Choice uliopo Tabata jijini Dar es Salaam, jana usiku ambapo wanandoa hao walijiwekea historia ya ndoa yao kwa kusherehekea siku maalum ya utambulisho wa Rais mpya wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli aliyekabidhiwa hati ya utambulisho wa ama cheti cha ushindi kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliomalizika wiki iliyopita.

Aidha wanandoa hao walifunga Ndoa Okt 27 huko Karatu mkoani Arusha.
 Bi Harusi Salma akimlisha Keki mumewe Said ikiwa ni ishara ya upendo.
 Bwana harusi na Bi Harusi,wakimkabidhi keki Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe yao, George John, ikiwa ni sehemu ya kumshukuru kwa kusheresha na kufanikisha sherehe hiyo.
 Mdogo wa Bi harusi akifanya yake ukumbini hapo...
 Bw na Bi Harusi wakiwa katika pozi.... 

Friday, October 30, 2015

Rais Mteule Dk Magufuli na Makamu Wake Wakabidhiwa Hati ya Uteuzi Dar

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wengine walioshiriki hafla ya kukabidhiwa hati za uteuzi kwa Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan leo  jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali waandamizi wa taifa wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hati za uteuzi kwa Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan leo  jijini Dar es Salaam.
Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan (nyuma yake) leo  jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa hati.
Meza kuu katika hafla hiyo Diamond Jubilee Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwakilisha mataifa yao, mabalozi na waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wakiwa katika hafla hiyo.
Jaji mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi hati ya uteuzi Rais wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) kwenye hafla maalum iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubelee Dar es Salaam leo.
Kushoto ni makamu wa Rais anayesubiri kuapishwa, Mama Samia Suluhu Hassan akionesha hati ya uteuzi wa nafasi hiyo mara baada ya kukabidhiwa na Jaji Damian Lubuva leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Magufuli akimuonesha hati ya uteuzi Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, wa kwanza kulia ni Makamu wake Mama Suluhu.
Viongozi mbalimbali wakiwakilisha mataifa yao, mabalozi na waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wakiwa katika hafla hiyo.
Wananchi na wanaCCM wakishangilia jambo katika hafla hiyo.
Dk. Magufuli akipunga mkono juu ya gari akitokea Ukumbi wa Diamond Jubilee kupokea kiapo cha uteuzi.
Dk Jakaya Kikwete akizungumza katika hafla hiyo.
Dk. Magufuli akizungumza ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokewa.
Dk. Magufuli akizungumza ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokewa.
Rais mteule wa Tanzania, Dk. John Magufuli akionesha hati ya uteuzi walizokabidhiwa na Tumea ya Taifa ya Uchaguzi kwa wanaCCM na wananchi waliofika kumlaki katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es Salaam leo

Dk John Pombe Magufuli Atangazwa Kushinda Urais Tanzania, JK Ampongeza Ikulu...!

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (kushoto) akimpa mkono wa pongezi Dk. John Magufuli baada ya kutangazwa kushinda urais Tanzania. 
Rais Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi Dk. John Magufuli baada ya kutangazwa kushinda urais Tanzania ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimpa mkono wa pongezi Dk. John Magufuli baada ya kutangazwa kushinda urais Tanzania ikulu Dar es Salaam. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Dk Magufuli akipokea pongezi mbalimbali kwa njia ya simu muda mfupi baada ya kutangazwa alipokuwa Ikulu kupongezwa na Rais Kikwete.
Dk. Magufuli na Rais Kikwete katika mazungumzo ya pongezi Ikulu jijini Dar es Salaam.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...