Wednesday, September 14, 2011

Harusi ya Ibra Kaude na mkewe Rahma Mohammed


"Mwenzagu Pokea pete hii iwe ishara ya upendo wangu kwako na uaminifu wangu kwao" Ndivyo inavyoonekana Rahma akisema wakati alipokuwa akimvisha pete ya ndoa mme wake, Ibra Kaude wakati wa Swala ya ndoa yao iliyofanyika Kigurunyembe mkoani Morogoro.


Ibra Kaude na mkewake Rahma Othumani Mohammed wakiingia ukumbini kwa madaha wakati  wakishiriki kwenye sherehe yao ya kuwapongeza iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, maharusi hao walifunga ndoa yao siku ya Septemba 9, 2011 katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-hud uliopo Kigurunyembe mkoani Morogoro.


Bwana Harusi Ibra Kaude na Rahma Othumani Mohammed, wakiwa katika pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao Septemba 9, 2011 mwaka huu katika Msikiti wa Al-Masjid Daarul-Hud uliopo Kigurunyembe mkoani Morogoro. Sherehe ya kuwapongeza ilifanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2011. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi  Vodacom Tanzania. (Picha zote na Mdau Albert Jackson)


Monday, September 5, 2011

Harusi ya Alex Gordian na mkewe Herieth Clavery


Bibi Harusi Herieth Clavery akila kiapo huku akimvisha pete mumewe, Alex Gordian katika ndoa yao iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki la St. Joseph Septemba 3, 2011 jijini Dar es Salaam.


Bwana Harusi, Alex Gordian akiapa mbele ya padre kumpokea mkewe Herieth Clavery na kuishi naye kama mke na mume milele kanisani. 


Maarusi Alex Gordian na mkewe Herieth Clavery (katikati) wakiwa na wasimamizi wao kanisani wakati wa ibada ya ndoa yao. Je, wataka kuingia picha zaidi wasiliana na mdau wa Blog kwa namba hapo juu (Picha zote na mpigapicha wetu)

Harusi ya Rogathe Kiwia na mkewe Patricia Saayo


Rogathe Kiwia (katikati) akiapa mbele ya mkewe Patricia Saayo kuwatayari kuingia katika maisha ya ndoa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 3, 2011.

Bi. Patricia Saayo (katikati) akiongozwa na msimamizi wake kula kiapo cha kuingia katika maisha ya ndoa na mumewe katika ibada ya ndoa yao hiyo. 


Rogathe Kiwia na mkewe Patricia Saayo (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wao kanisani. Waweza kutuma picha zaidi za hafla hii! Wasiliana na mdau wa Blog kwa namba za simu hapo juu (Picha zote na mpiga picha wetu)

Saturday, September 3, 2011

Harusi ya Evarist Lebba na Edna Shao

                                     
Bwana harusi Evarist Lebba (kushoto) akimvisha pete mkewe Edna Shao ikiwa ni ishara ya kuungana katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam Septemba 3, 2011.
   
            

Bwana Harusi Evarist na mkewe Edna (katikati) wakiwa na wasimamizi wao (upande wa kulia na kushoto kwao), wakiongozwa na mmoja wa mapadre waliofungisha ndoa yao kanisani hapo.

 
             

Bwana harusi na bibi harusi wakiwa na wasimamizi wao kanisani wakati ibada ya misa yao ikiendelea. (Picha zote na mpiga picha wetu)

Monday, August 29, 2011

Sherehe ya 'send off' ya Lilian Mbaga


Bi. Lilian Mbaga akiwa na mpambe wake Marry Ezekiel wakiwa katika maandalizi ya mwisho (send off) kabla ya kwenda kufunga ndoa na mme wake Glovann Nguva katika Kanisa la Kristu Mfalme la Tabata jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya FullShangwe)

Harusi ya Mtabi na mkewe Marrygoreth


Mtabi na mke wake Marrygoreth wakiwa katika pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la Mtakatifu Mwenye Heri, Anwarite la Makuburi na kufuatiwa na tafrija kubwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Landmark Hoteli jijini Dar es Salaam. (Picha kwa hisani ya FullShangwe Blog)

Monday, August 22, 2011

Harusi ya Inno Mac na mkewe Macrina Caesar

Maharusi Inno Mac na mkewe Macrina Caesar wakiwa katika mapozi siku ya harusi yao.

 Kutoka kulia ni Inno Mac na mkewe Macrina Caesar mbele yake wakiwa na wapambe wao (kulia) siku ya harusi yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam (Picha kwa hisani ya familia ya Mzee Mac)







SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...