Thursday, March 31, 2011

Harusi ya Moshi Mbully na mkewe Mwashada


Februari 11, 2011 itabaki siku maalumu na kumbukumbu ya milele kwa Bw. Moshi Mbully wa Kinondoni Dar es Salaam na mkewe Bi. Mwashada wa Kigogo Mbuyuni Dar es salaam, kwani ndiyo siku waliounganishwa rasmi kama mke na mume.


Mwashada akimuongoza mumewe kwenda kuwaaga wazazi wake kabla ya kuondoka na mumewe baada ya ndoa yao.


Wageni waalikwa wakitoa mkono wa kwaheri kwa maharusi kabla ya kuondoka ukumbini.


Mama wa Bi. Harusi, Mrs Ewald Mushi akiwa katika pozi siku ya harusi ya mwanae.



Shangazi wa bibi harusi, Mrs G. Ishengoma (katikati) akiwa pamoja na wageni waalikwa


Shughuli mbalimbali zikiendelea ukumbini



Mambo ya maakuli ilikuwa ni uwezo wako tu


DJ wa harusi hiyo Frank Bush (kulia) akiwa na Mrs Herry aka Mama Rose ambaye ni mdogo wa Bi. harusi wakiwa kwenye mapoz ya picha. Picha zote na Mdau Mkuu wa HM.

Tuesday, March 29, 2011

Obama aeleza sababu za kumpiga Gadhafi


Rais wa Marekani, Barrack Obama

RAIS Barrack Obama wa Marekani, ameeleza sababu za kuingilia mgogoro uliokuwa ukiendelea nchini Libya, kati ya Rais wa nchi hiyo, Moammar Gadhafi na waasi waliokuwa wakimpinga na maandamano yaliokuwa yakifanywa na makundi ya wananchi nchini humo.

Miongoni mwa sababu ya msingi ambazo Obama amewaeleza waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, ni kwamba waliamua kufanya hivyo ili kunusuru maisha ya wana-Libya waliokuwa wakiuawa na majeshi ya Serikali yaliokuwa yakiwazuia waandamanaji waliokuwa wakimpinga Gadhafi.

Obama alisema nchi yake isingelipenda kuona wananchi wakiuawa na kunyanyasika ilhali hawana hatia na ndio maana yeye (USA) na washirika wake walifanya uamuzi wa kuivamia Libya kwa lengo la kumuondoa Gadhafi madarakani.

"Tunamalizia kufanya mashambulizi ya mwisho kwenye mji ambao ulikuwa makazi na ngome ya Gadhafi lakini baada ya hapo tutakabidhi madaraka ya kuiongoza nchi ya Libya kwa Jeshi la NATO, ili waweke utaratibu wa nchi kurudi wakati wake," alisema Obama akionekana kujiamini.

Monday, March 28, 2011

Ujumbe maalumu wa Rais Omar el Bashir kwa JK


Rais Jakaya Kikwete akipokea ujumbe maalumu wa Rais Omar El Bashir wa Sudan kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan,  Ali Ahmed Karti aliouwasilisha Ikulu Dar es Salaam. (PICHA NA MDAU FREDDY MARO)

Saturday, March 26, 2011

BREAKING NEWZZZ; Roho za Watanzania zaendelea kuteketea

*Ajali mbaya yaua tena 9, yajeruhi wengine

IKIWA ni siku chache tangu ajali ya wasanii wa kundi la five star kutokea Mkoa wa Morogoro na kuua wasanii 13 wa kundi hilo na nyingine kutokea tena eneo jirani na lile na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa, imetokea nyingine mbaya na kuua watu tisa.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata muda huu kutoka kwa shuhuda ambaye yupo safarini eneo hilo, gari aina ya coaster namba T 566 AZP lililokuwa likitoka Chalinze kwenda Dar es Salaam limegongana na lori namba T 535 AAG; na imedaiwa watu tisa wamekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na shuhuda huyo amesema coaster ililikuta lori limesimama njiani na likitaka kulipita lilitokea lori lingine mbele ndipo dereva alipoamua kulivamia lori lililosimama akijaribu kukwepa kugongana uso kwa uso na lori la mbele yake.

Shuhuda huyo amesema kuwa waliokufa wote wametoka kwenye coaster na maiti zinaondolewa na inadaiwa zinapelekwa hospitali ya Tumbi, Kibaha.

“Ajali hii imehusisha gari aina ya coaster ambalo lilikuwa likitokea Chalinze kwenda Dar es Salaam, limegongana na lori lenye tela dereva wa coaster inaonekana kavunjika miguu yote…na gari imebondeka vibaya mbele…,” anasema na kuendelea.

“Hapa kwa sasa magari hayatembei maana ajali imeziba barabara foleni ni ndefu kuanzia maeneo ya Daraja la Ruvu hadi eneo la ajali,” alisema shuhuda huyo liyejitaja kwa jina moja la Ally akizungumza kwa njia ya simu Harusi na Matukio (HM).

Aidha alisema eneo ilipotokea ajali ni kilomita chache kabla ya kufika Kiluvya ukitokea Chalinze majira ya saa tano na tayari askari wa usalama barabarani wamefika kutoa msaada kwa wahusika, huku wakijitahidi kuongoza magari kwani barabara ilifungwa na ajali hiyo.

Tunaendelea kukusanya taarifa na tutawaleteeni kadri zinavyotufikia kutoka kwa vyanzo vya HM.

Tuesday, March 22, 2011

Jambo Leo wawafanya vibaya TBC1 kombe la NSSF



Baadhi ya wachezaji wa Jambo Leo katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao na TBC1.


TIMU ya Soka ya Gazeti la Jambo Leo, linalomilikiwa na kampuni ya Jambo Concepts Ltd, imeshindilia timu ya Soka ya Shirika la Habari Tanzania (TBC 1) mabao 3 kwa moja.

Wakicheza mpira ulioonekana wa hali ya juu kiasi cha kuwapa tabu muda wote, TBC1 Jambo Leo ndio walioanza kuanza kufungua mvua ya magoli baada ya muda mfupi tangu kuanza kwa pambano hilo.

Goli la kwanza la Jambo Leo, liliwachanganya zaidi washambuliaji wa TBC1 na kujitahidi kusawazisha muda mfupi baadaye kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa kwa wachezaji wa Jambo Leo ambao walionekana kuwaelemea zaidi TBC1 na kuandika mabao mawili mengine ya harakaharaka.

Hadi mwisho wa mchezo huo Jambo Leo 3 na TBC1 waliambulia goli moja.


Benchi la ufundi la Jambo Leo pamoja na wachezaji wa akiba. Watatu kulia waliokaa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Jambo Concepts Ltd, Benny Kissaka akifuatilia vijana wake.




Kikosi kizima cha timu ya Jambo Leo kikiwa na kocha wake (wa kwanza kushoto waliosimama) na kiongozi wa benchi la ufundi (wa pili waliosimama) kabla ya kuanza kwa pambano kati ya TBC1 na timu hiyo.

Waamuzi wa mchezo huo wakiwa katika picha ya pamoja, kabla ya kuanza kwa pambano.




Kikosi cha TBC1 kilichoshindiliwa 3-1 katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Picha na Mdau Mkuu wa Harusi na Matukio.

BREAKING NEWS: Issa Kijoti wa 5 Star, wenzake wa 5 wafariki kwenye ajali Morogoro, walikuwa safarini kurudi Dar


Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani.


Na Mwandishi Wetu

TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa, wanamuziki wa kundi la 5 star wamepata ajali mbaya eneo la Mikumi Morogoro na watu watano akiwemo muimbaji maarufu wa kundi hilo Issa Kijoti wamefariki dunia.

Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarabu la 5 Star, kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati wakitokea mikoani kuja Dar es Salaam.

Inasemekana waliotambuliwa kufariki dunia mpaka sasa ni pamoja na Issa Kijoti, Hamisa Omary, Husna Mapande, omary Hashim, Nasor na Shaby Juma. Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinasema tayari miili ya marehemu hao imeondolewa eneo la ajali na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro.

Mdau mmoja wa masuala ya muziki amethibitisha kupatwa na ajali kwa wanamuziki hao, kwani amedai simu zao zinapigwa na kuita bila majibu kati ya kundi lililokuwa likisafiri katika gari hilo.

Inadaiwa jumla ya watu sita (6) wamefariki dunia katika ajali hiyo. Taarifa zaidi zitatolewa na HM kadri zitakavyotufikia, endelea kufuatilia.




Thursday, March 17, 2011

Picha mbalimbali za ziara ya NSSF Bukoba na Mwanza kukagua miradi yao



Meneja wa Kiwanda cha Sukari Kagera, Nestory Ruchungura (wa kwanza kulia aliye nyoosha mkono mbele) akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea kiwanda hicho juzi mjini Kagera. 


Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana akitoa maelezo mafupi ya kiwanda hicho kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF walipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.








Meneja wa Kiwanda cha Sukari Kagera, Nestory Ruchungura (wa kwanza kulia aliye nyoosha mkono mbele) akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea kiwanda hicho juzi mjini Kagera. 


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF (waliosimama msitari wa mbele) wakipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa juu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera (waliosimama nyuma). Wapili kushoto mbele ni Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda, Buddana Rau. Nyuma ni moja ya matrekta ya kisasa yalionunuliwa na kiwanda hicho baada ya mkopo wa NSSF kwa kiwanda hicho, matrekta hayo yanauwezo wa kufanya kazi yenyewe kwa msaada mdogo wa dereva.


Miongoni mwa matrekta ya kisasa yaliyonunuliwa na kiwanda hicho baada ya kupata ufadhili wa mkopo wa takriban bilioni 12 kutoka NSSF



Kutoka kushoto ni Mwenekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajab (mwenye koti), Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Mudhihir Mudhihir wakiwaongoza wajumbe wengine wa NSSF kutembelea kiwanda hicho. NSSF imetoa ufadhili wa mkopo wa sh. bilioni 12 kwa kiwanda hicho.








SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...