Saturday, December 16, 2017

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI MPYA YA KAMPUNI YA MBOLEA YA TAIFA, AIONYA...!

 Waziri wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa katika hafla ya uzinduzi.
 Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa, Egid Mbofu, akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Meneja Mkuu wa TFC, Salum Mkumba.
 Wajumbe wa bodi hiyo wakiwa bize kuchukua maagizo ya Waziri Mwijage.
 Waziri Mwijage akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC), (hawapo pichani), wakati akiizindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam jana.



 Hapa ni kalamu zikizungumza katika uzinduzi huo wakati Waziri Mwijage alipokuwa akiipa majukumu bodi hiyo mpya ya TFC.
 Uzinduzi ukiendelea.
Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, ameitaka Kampuni ya Mbolea ya Taifa (TFC) kubadilisha mfumo wa utendaji ikiwa ni pamoja na kutoingia mikataba inayoweza kuisababishia serikali hasara, badala yake kuangalia wabia wanaoweza kuisaidia kujipanua na kupata faida kubwa zaidi.

Waziri Mwijage, aliyasema hayo juzi wakati akiizindua bodi mpya ya Wakurugenzi ya TFC, na kuongeza kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, haiko tayari kuona taasisi zake za umma zikiingizwa katika mikataba mibovu na isiyokuwa na tija.

Pia aliagiza kwamba, baada ya kuizindua bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo,  Profesa Egid Mbofu na wajumbe wake, waanze kazi mara moja na moja ya majukumu yao ya awali ni kuangalia ama kuipitia upya miokataba ambayo awalo iliingiwa na TFC.

Alisema TFC ikifanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kujielekeza kwenye kazi zenye faida kubwa, itaweza kusaidia kasi ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini, na kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Taifa la uchumi wa kati na wa Viwanda.

"Tunatambua sekta ya kilimo ni nguzo muhimu kwa ajili ya uchumi wa TANZANIA, lakini haiwezi kuleta mafanikio makubwa kwa jamii, ikiwa TFC haitaweza kupewa uwezo na kuwafikia wakulima wengi zaidi", alisema Waziri Mwijage.

Aliongeza kusema kwamba, mazingira ya sasa ya kilimo kwa Tanzania, yanahitaji umakini katika uagizaji wa mbolea zinazotumiwa na wakulima wengi ambao malengo yao ni kupata faida, lakini wamekuwa wakiangushwa na baadhi ya wafanyaviashara wanaoagiza mbolea feki.

TFC ni mtoto wa serikal, hivyo nimeagizwa na mheshimiwa Rais, kuwaonoa hofu na kwamba tunahitaji kuiongezea uwezo ili Taifa liweze kufikia malengo ya uzalishaji mkubwa wa chakula pamoja na mazao mengine yanayohitajika kama malghafi katika viwanda.

Kwa upande wake Profesa Mbofu, alimshukuru Waziri Mwijage na kumuahidi kwamba, wako tayari kwa kazi hiyo lakini pia akasema wamfikishie Rais shukrani zao kwa uaminifu wake kwao.

"Ninaomba kwa niaba ya wajumbe wa bodi hii, menejimenti ya TFC kukushukuru kwa kazi hii nzuri na maagizo yako yote kwetu, tunakuahidi kuifanya kazi hii kwa uaminifu na uadilofu mkubwa na tutaendelea kuomba ushauri wako kila tunapohitaji kufanya hivyo kama njia ya kupata miongozo zaidi," alisema Profesa Mbofu.

Meneja Mkuu (GM),  Salum Mkumba, alimhakikishia Waziri Mwijage, kwamba TFC iko tayari kwa mabadiliko ya aina yeyote na wafanyakazi wako tayari kwa kusimamia maagizo kwa ajili ya kuendana na Tanzania ya Viwanda kulingana na sera na miongozo ya serikali ya awamu ya tano.


Pia GM Mkumba, alisema TFC ni miongoni mwa taasisi za umma zilizo chini ya wizara ya Viwabda na Uwekezaji, ambazo tayari zilianzisha mabaraza ya wafanyakazi kwa ajili ya kuwashirikisha wafanyakazi na kuwajengea uwezo wa kushauri kasi ya maendeleo kwenye kampuni hiyo ya umma.

Thursday, December 14, 2017

RDF WASHEREKEA MWAKA MMOJA TANGU KUANZISHWA...!

 Mkurugenzi Mtendaji wa Reaching Out Destinies Foundation(RDF) Bi. Jane David akifungua rasmi  kwa maombi sherehe za kuwashukuru wadau wao kwa kuwa nao kwa muda wa mwaka mzima, na baadae kutoa shukurani zake za dhati kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote cha mwaka mzima.


Wednesday, December 13, 2017

Mohammed Enterprises yashinda tuzo nne za ATE 2017

Mohammed Enterprises yashinda tuzo nne za ATE 2017

Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Royal Soap, Jackline Mbaga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Star Oil Tanzania Limited , Ester Dotto, Meneja Mkuu wa Mo Assurance Limited, Kura Bonniface, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji, Meneja Mauzo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Holding Limited, David Mziray, Ofisa wa kitengo cha Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Jessica Julius, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Textiles, Godfrey Ndimbo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Food and Packaging, Anna Zongo wakiwa na tuzo nne ambazo wameshinda kwenye tuzo za ATE 2017.

KAMPUNI ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) imeshinda tuzo nne za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 (EYA) zinazotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla ya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. MeTL imeshinda tuzo hizo kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Mo Assurance Limited iliyoshinda kipengele cha Tuzo ya Kampuni Ndogo, 21st Century Holding Limited imeshinda nafasi ya pili ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani na Star Oil Tanzania Limited imeshinda tuzo mbili, Tuzo ya Kampuni ya Kati na nafasi ya tatu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani. Ushindi huo wa tuzo nne, umeiwezesha MeTL Group kuwa moja ya kampuni nne ambazo zimeshinda tuzo nyingi za ATE 2017, na kuwa kampuni ya kizalendo ambayo imeshinda tuzo nyingi kuliko kampuni zingine ambazo zimeshiriki katika tuzo hizo.

Akizungumza kuhusu ushindi huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MeTL Group, Hassan Dewji, alisema wamefurahishwa na ushindi huo, lakini pia unaonyesha jinsi gani kampuni inafanya vizuri katika soko la hapa nchini. "Tuna furaha kushiriki kwenye tuzo za ATE 2017 na tuna furaha kushinda tuzo nne, naamini tumekuwa moja ya kampuni tano ambazo zimeshinda tuzo nyingi. Nafikiri sisi ni moja ya kampuni kubwa nchini na tunaendelea kukua na kugusa maisha ya watu wengi kila siku, ushindi kama huu utuwezesha kuongeza juhudi zaidi," alisema Dewji.

Monday, December 11, 2017

Wadau wa Maliasili na Utalii wampongeza Dk. Kigwangalla



Na Hamza Temba, Arusha



Wadau wa Utalii Jijini Arusha wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kwa kukubali kuyafanyia kazi mapendekezo yao ya kuwaingiza wajasiriamali wadogo katika utoaji wa huduma za kusafirisha watalii nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo wakati akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini humo.

Chambulo alisema kwa muda mrefu sasa kanuni zinazotumika zinamtaka mfanyabiashara ya usafirishaji watalii awe na magari matatu kwa kiwango cha chini ikiwa ni pamoja na kulipia ada ya leseni ya Dola za Kimarekani 2,000 sawa na wafanyabiashara wengine matajiri jambo ambalo limekuwa likiwabagua wafanyabiashara wadogo.

“Tunakupongeza sana Mhe. Waziri kwa kutupa angalao hilo moja, tuliomba mwenye kagari kamoja nae aruhusiwe na apewe leseni walau ya dola 200 ili afanye biashara kidogo kidogo mwishowe atanunua gari tano na kuendelea, tunataka sisi Watanzania wote tufaidike na rasilimali zetu,” alisema Chambulo.

Awali akiwasilisha mapendekezo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu alisema kwa upande wa watanzania ambao ni wajasiriamali wadogo wenye gari moja hadi magari matatu watatakiwa kulipa ada ya leseni ya dola za Kimarekani 200.

Kwa upande wa wafanyabiashara wenye magari kuanzia manne hadi kumi alisema imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 2,000, wenye magari 11 hadi 50 Dola za Kimarekani 3,000, magari 51 hadi 100 Dola za Kimarekani 10,000 na magari 100 na kuendelea Dola za Kimarekani 15,000.

Kwa upande wa wafanyabiashara ambao sio Watanzania wenye magari 10 hadi 30 imependekezwa walipe Dola za Kimarekani 10,000, magari 31 hadi 100 Dola za Kimarekani 15,000 na magari 101 na kuendelea Dola za Kimarekani 20,000.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo ya viwango hivyo vipya vya leseni ya biashara ya utalii kwa wadau ni kuweka ushirikishwaji na makubaliano ya pamoja ya kutekeleza kanuni hizo.

Alisema sehemu kubwa ya mapendekezo hayo imezingatia maombi na maoni ya wadau hao ambayo yaliwasilishwa kwake awali. “Kilio chenu nimekisikia mimi mwenye mamlaka ya kufanya mabadiliko, lengo kubwa la mapendekezo haya ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo wenye gari moja waweze kuingia kwenye biashara hii ya utalii pamoja na kuongeza mapato ya Serikali na jamii kwa ujumla,” alisema Dk. Kigwangalla.

Katika hatua nyingine amewaagiza watalaamu ndani ya Wizara yake kuhakikisha wanakamilisha kanuni hizo mpya ndani ya mwa mwaka huu ili utekelezaji wake uanze mapema mwakani, 2018.

Akizungumzia wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuwasafirisha watalii nyuma ya pazia bila kulipia leseni, alisema Wizara yake inaandaa mfumo maalumu wa kielektroniki utakaowezesha ukaguzi wa magari kwenye mageti ya kuingilia hifadhini ili kudhibiti vitendo hivyo.


Aidha, ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara hao na kuwataka kufanya biashara hiyo kwa weledi na kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kulipa ada ya leseni husika kwa mujibu wa sheria. 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki. 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deogratias Mdamu (kushoto).


Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.


 Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.


 Baadhi ya wadau wa Utalii walioshiriki mkutano huo.


Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Wilbard Chambulo akichangia mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii zilizowasilishwa kwao na Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mkutano huo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitambulishwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) kwa Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO), Merywn Nunes muda mfupi baada ya kikao na wadau wa utalii Jijini Arusha jana ambapo Wizara yake iliwasilisha mapendekezo ya viwango vipya vya leseni za biashara ya utalii na tozo ya ada za malazi katika viwango vya ubora wa nyota. 

Wanahabari wamlilia marehemu Joyce Mmasi

 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.

 Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.

 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.

 Mchungaji Kulwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.

 Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.

 Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.

 Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.


Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.


 Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.

 Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.

 Mtoto mkubwa wa marehemu,  Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.

 Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.

 Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.

Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho.

Na Dotto Mwaibale

VILIO Majonzi na simanzi vilitawala   wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.

Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.

"Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.

Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.

Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.

Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.

Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.

Vijana Zanzibar na Tanzania waangalia fursa zilizopo

 Vijana kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya kulitetea taifa maendeleo. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark jijini Dar es Salaam.

 Majadiliano yakiendelea.


 Msisitizo katika majadiliano hayo.


 Fursa mbalimbali zikiandikwa katika makundi.


Na Dotto Mwaibale

VIJANA wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuliletea taifa maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark vijana hao wapatao 14 kwa niaba ya wenzao walijadiliana mambo mbalimbali na kuangalia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

Kwa ujumla fursa zilizokuwa zimeangaliwa katika maeneo mbalimbali na wazo hilo limekuja baada ya baadhi yao kutembea nchi nzima Tanzania Visiwani na Tanzania Bara na kuziona hivyo wakaona ni vema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwashirikisha wenzao na kuona waanzie wapi.

"Tumetembea nchi nzima na kuona fursa mbalimbali tukaona ni vizuri vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara tukutane tujadiliane na tuone ni fursa zipi tuzifanyie kazi kwa manufaa yetu kama vijana na taifa kwa ujumla" alisema mmoja wa vijana hao ambaye hakupenda kuingia kiundani zaidi kwa kuwa mchakato wa jambo hilo ndio kwanza upo jikoni.

Alisema hivi sasa vijana wasitegemee kuajiriwa badala yake waziangalie fursa zilizopo nchini na hizo ndizo zitakazo waondoa katika mawazo ya kutegemea kuajiriwa.

Alisema kuna fursa za kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ufugaji, ufundi mbalimbali, kilimo na mambo mengine hivyo ni vema vijana wakaangalia huko zaidi.

Alisema wamekutana katika mkutano huo kuangalia fursa hizo na wapi pa kuanzia na mchakato huo ukikamilika wataweka mambo hadharani na kukamilisha mambo yote lengo likiwa ni kuwaunganisha vijana wa nchi nzima.

Tuesday, December 5, 2017

MSD yapongezwa kushinda tenda ya SADC

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI) katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja katika ziara iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI), Respicious Lwezimula (kulia), akizungumza katika kikao hicho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa tatu kushoto), akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika ziara hiyo.

Kikao kikiendelea.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa nne kulia), akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI)
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima, akizungumza na viongozi kutoka MSD. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine Haule. 
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke baada ya kufanya nao mazungumzo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD), imepongezwa kwa kushinda tenda ya kununua dawa Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Pongezi hizo zimetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Lawrence Mseru wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na timu yake wakati wakiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.

"Kwanza tunawapongezeni MSD kwa kufikia hatua ya kununua dawa katika Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) hii ni hatua ya kujivunia kama nchi" alisema Profesa Mseru.

Mseru aliongeza kuwa licha ya kuwepo changamoto ndogo ndogo MSD imejitahidi katika huduma ya usambazaji wa dawa hapa nchini hivyo akaomba ushirikiano baina yao uendelee kudumishwa ili kutoa huduma nzuri zaidi ya kuwahudumia wananchi ukizingatia kuwa taasisi hizo zote zinafanya kazi ya Serikali.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI),Respicious Lwezimula alisema kazi kubwa inayofanywa na MSD inapaswa kuungwa mkono kwa kununua dawa na vifaa tiba.

"Tuna kila sababu ya kuwaunga mkono hawa wenzetu kwa kununua vifaa tiba na dawa kutoka kwao badala ya kununua kwenye maduka ya watu binafsi kikubwa tunawaomba bei yao iwe tofauti kidogo" alisema Lwezimula.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima alisema suala la manunuzi ya dawa na vifaa tiba linachangamoto kubwa lakini MSD wamesaidia sana kuzipunguza kutokana na ushirikiano wanaofanya baina yao na wateja wao hawana budi kupongezwa.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amewaomba wateja wao hao kufanya Maoteo ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha MSD kwa wakati kwa mujibu wa sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba vinavyonunuliwa kwa manunuzi maalumu.

Bwanakunu alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.

Akizungumza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Temeke na Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI), Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na vifaa tiba na kuwa MSD katika kukabiliana na changamoto hizo imepata msaada wa magari 220 kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.

Kuhusu vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila hospitali kuleta kwa wakati wake.

"Vifaa hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu hivyo tukipata oda mapema itatusaidia kupunguza changamoto hiyo " alisema Bwanakunu.




SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...