Tuesday, December 5, 2017

Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina yakutana na Balozi Maiga




Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina alipokutana nayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour.
Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (wa kwanza kushoto) kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (katikati) akisaini kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli kabla ya kumkabidhi Balozi Augustino Maiga. 

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akipitia kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea mara baada ya kukabidhiwa.Kutoka kushoto ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck.

Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ikiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga.

Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo (kushoto) akitoa utaratibu wa mazungumzo katika mkutano huo na wanahabari. 
 






Monday, December 4, 2017

Mbunge wa Segerea, Bonnah ashiriki bonanza la michezo

Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa amejumuika na wakazi wa jimbo lake katika  bonanza lilijomuisha michezo mbalimbali. Bonanza hilo lililofanyika katika uwanja wa Sigara uliopo Tabata lilikuwa ni hitimisho la mashindano ya Bonnah Cup 2017 ambapo fainali ilikuwa ni kati ya Kimanga Bodaboda na Sigara FC huku timu ya Bodaboda ikiibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4.

Mshindi wa fainali alijishindia shilingi milioni moja taslimu pamoja na pikipiki wakati mshindi wa pili akipata shilingi laki tano na mshindi wa tatu akiondoka na  shilingi laki tatu.

Akizungumza baada ya fainali Mheshimiwa Bonnah Kaluwa amesema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwisho wa mwaka ili kuinua michezo jimboni hapo na kusema mshindi wa mwaka huu atapata nafasi ya kwenda Dodoma kushindana na timu ya wabunge.
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda Kimanga kabla ya mchezo wa fainali
Mbunge wa Segerea Mh. Bonnah Kaluwa katika picha ya pamoja na EFM jogging club
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akionyesha umahiri wa kupiga danadana akitazamwa na wachezaji wa zamani wa Taifa Stars
Mshambuliaji wa timu ya Sigara FC akijaribu kuwatoka mabeki wa Bodaboda
Mamia ya mashabiki wakifuatilia mchezo


Wachezaji wa Bodaboda Kimanga wakifurahia kombe lao
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akiungana na mashabiki kucheza singeli
Mkali wa muziki wa Singeli Msaga Sumu akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi

Simba SC kuanza kuzalisha nafasi za ajira

MWEKEZAJI mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO amesema amejipanga kushirikiana na wanahisa wenzake wa klabu hiyo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia kampuni ya Simba Sports Club Limited. Dewji aliyasema hayo wakati akitoa salamu kwa wanachama na mashabiki wa Simba kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo, baada ya kutangazwa na kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba, kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo. Alisema klabu ya Simba inampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuongoza serikali ya awamu ya tano, na wao wamedhamiria kuhakikisha wanakwenda sambamba na kasi yake kupitia mchezo wa mpira kwa kutoa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mpya itakayosimamia timu hiyo katika mfumo wa hisa. Mwekezaji mpya katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji MO akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere. "Tamati yangu nielekeze kwa sisi sote kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayofanya ya kuongoza taifa hili. Wote tumtakie kila la kheri, baraka na fanaka tele katika utumishi wake uliotukuka, "Pamoja na kupongeza sera yake ya ujenzi wa viwanda nchini, ambapo sisi kwa upande wetu, klabu ya Simba inamuunga mkono kwa ujenzi wa kiwanda kikubwa kabisa cha soka yaani Simba Sports Club Limited, ambacho licha ya kuongeza ajira lakini pia tutaendelea kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi," alisema Dewji. Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed Entreprises, alitumia mkutano huo kuelezea mipango ambayo wameipanga ili kuiwezesha Simba kuwa klabu kubwa zaidi barani Afrika kuliko ilivyo sasa, huku malengo ikiwa ni kuwania mataji makubwa barani Afrika.
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah akimkabidhi cheti cha ushindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu ya Simba mfanyabiashara na mwanachama wa muda mrefu wa klabu hiyo, Mohammed Dewji MO kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.
"Katika mwaka wa kwanza, nawaahidi kwa kushirikiana na ninyi tutakuwa na kiwanja cha nyasi asilia, na kiwanja cha nyasi za bandia ambapo viwanja hivi tutavitumia kwa mazoezi kwa kadri ya mahitaji ya mechi tunayokwenda kucheza, "Pia tutajenga hosteli ambayo itakuwa na vyumba 35 ambavyo wataishi wachezaji 30 na support staff, kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 35 square- meter... ili kufanya eneo hilo kuwa bora kwa wachezaji wetu," alisema Dewji na kuongeza. "Wote tunaopenda mpira, tunajua kama ukitaka kuwa na wachezaji bora lazima utumie pesa. Nia yetu kwa mwaka wa kwanza, tunatarajia kiwango cha chini cha pesa ya usajili iwe bilioni moja. Pia tumetenga milioni 500 kuboresha benchi la ufundi, kwa kushirikiana na benchi liliopo sasa." Hata hivyo Dewji, alisema klabu ya Simba itajenga kituo cha kukuzia vipaji ambacho kitakuwa na wachezaji vijana. Jambo ambalo litaisaidia Simba kuwa na wachezaji bora vijana ambao wamefundishwa kucheza soka katika kituo cha timu hiyo. "Ili kuwa na wachezaji bora kwa miaka ijayo tunahitaji kuwa na kituo cha kukuzia vipaji kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 14, 16, 18. Na mipango yetu ya baadae ni kushirikiana na timu kubwa za ulaya kutuongoza na kutuelemsha jinsi gani ya kujenga kituo chenye hadhi ya kimataifa na mungu akipenda tutakuwa na kituo bora barani Afrika." alisema Dewji.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba wakishangilia baada ya kamati maalum ya kusimamia mchakato wa kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba kumtangaza Mohammed Dewji MO kuwa mshindi wa tenda ya kuwekeza katika klabu hiyo.

Saturday, December 2, 2017

SBL yazinduwa kampeni ya unywaji pombe kistaarbu

Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhimiza unywaji kistaarabu katika msimu huu wa sikukuu pembeni yake kutoka kulia ni Meneja Masoko wa SBL, Anitha Rwehumbiza na kushoto kwake ni Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Meneja Masoko wa SBL Anitha Rwehumbiza akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu ambayo imeshirikisha timu ya Taifa mapema jana katika hoteli ya hyatt Regency jijni Dar es salaam.


Ofisa  Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha unywaji kistaarabu uliofanyika mapema jana katika Hotel ya Hyatt Regency na mwishoni ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau .



Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau akiongea na waandishi wa habari namna ambayo Timu ya stars ilivyoshiriki kampeni hiyo na pia akishukuru  udhamini wa SBL kwa timu hiyo ,Katikati ni Ofisa  Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya na mwishoni ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie ,mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.


Waandishi wa habari wakichukua matukio 




Moja ya Matangazo ambayo yatakuwa yakihamasisha unywaji wa kistaarabu 

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni ya miezi miwili kuhamasisha wanywaji juu ya unywaji pombe wa kistaarbu kama jitihada za kampuni katika kupunguza changamoto za ajali nyingi barabarani hasa katika msimu huu wa sikukuu.
Katika kampeni hii, bia ya Serengeti Premium Lager imeungana na Timu ya Taifa, Taufa Stars kuhimiza umuhimu wa unywaji kistaarbu.
Kampeni hiyo iliyopewa jina la “Mastaa wa kweli hunywa kistaarabu” Bia ya Serengeti imejikita kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto, abiria, waenda kwa miguu na jamii yote kwa ujumla juu ya umuhimu wa usalama barabarani msimu huu wa sikukuu. Kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi miwili.
Kampeni hii ya kitaifa inayohusisha wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars itaonekana katika baa na vilabu mbalimbali na pia kwenye matangazo ya nje, runinga, redioni na mitandao mbalimbali ya kijamii. Bia ya Serengeti Premium ndiyo mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.
“SBL imejikita sio tu katika usalama wa wafanyakazi wetu na mali zetu pia katika jamii kubwa ya Watanzania kwa ujumla ambapo biashara yetu ni kati ya sehemu hiyo. Ni kwa misingi hiyo basi kampeni hii ya “Mastaa wa kweli hunywa kistaarabu” inalenga kutoa elimu kwa vijana, waendesha magari na bodaboda, waenda kwa miguu na jamii nzima kwa ujumla juu ya unywaji kistaarabu katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa sikukuu na kuonya matumizi ya uendeshaji chombo cha moto ukiwa katika hali ya ulevi” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SBL Bi Helene Weesie wakati wa sherehe za uzinduzi.
Mkurugenzi huyo wa SBL amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikiendesha kampeni ya Unywaji wa Kistaarbu kwa takribani miaka mitano sasa kwa ushirikiano kutoka kwa Jeshi la Polisi nchini na wadau mbalimbali waliojitolea katika kuhakikisha usalama barabarani. Uelimishaji wa unywaji pombe kistaarabu unafanywa kwenye vyuo, sehemu za kazi na kwenye baa ambapo wahusika huelimishwa ni kwa kiasi gani kinywaji akipendacho kina kilevi ndani yake.
“Katika kuwatakia Watanzania msimu wa fanaka na Baraka za sikukuu, tuna jukumu la kuwakumbusha kuendelea kufurahia bidhaa za SBL kistaarabu na kubaki salama wakati wakisherehekea na marafiki na familia” aliongezea.
Akihudhuria hafla hiyo, Ofisa  Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya  aliwashukuru SBL kwa mpango wao akisema kuwa ni mchango chanya katika kukuza usalama wa barabarani katika msimu huu wa sikukuu.
Malya alilaumu juu ya uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na ajali akisisitiza kuwa ajali za barabarani pia zinawapa mzigo mkubwa sana sekta ya afya nchini katika kuwahudumia manusura wa ajali.

EfG wazinduwa siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia

 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika Dar es Salaam jana Soko la Tabata Muslim.
 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita akimpatia fulana Mwakilishi wa Mbunge wa Segerea, Bonah Kaluwa aliyefika kwaniaba yake kama mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed wakati wa uzinduzi huo.


  Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi.

 Mwenyekiti wa Soko la Tabata Muslim, Haji Mohamed akihutubia.

 Mratibu wa Mradi wa Mpe Riziki Si Matusi, Susan Sita, akihutubia.

 Wawezeshaji wa kisheria wa EfG wakiwa na furaha katika uzinduzi huo.

 Burudani ikitolewa.

 Burudani ikiendelea.


 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akihutubia.

 mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed, akihutubia wakati wa uzinduzi huo.

 uzinduzi ukiendelea.

 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Mkurugenzi wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akiteta jambo na mgeni rasmi.

Mgeni rasmi akijumuika na wadau mbalimbali na wawezeshaji sheria wa shirika hilo.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Equality for Growth (EfG) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, jana limezindua siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Soko la Tabata Muslim Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa shirika hilo, Jane Magigita amesema kwa sasa EfG inaendesha mradi unaoitwa "MPE RIZIKI SI MATUSI" ambao umeongeza wigo wa mapambano ya ukatili wa kijinsia  katika Wilaya ya Ilala na Temeke katika masoko sita.

Ameyataja masoko hayo kuwa ni Mchikichini, Kisutu,Tabata Muslim, Feri, Gezaulole na Temeke Stereo.

Magigita aliongeza kuwa, lengo la mradi huo ni kuona wanawake wafanyabiashara wa Manispaa ya Ilala na Temeke wanafanyabiashara katika mazingira huru dhidi ya ukatili wa kingono, kimwili, matusi na kisiasa, vilevile kuona wanawake wakipewa heshima kama binadamu wengine ili waweze kujipatia kipato chao bila vikwazo.

"Mbali na kuwepo mashirika mbalimbali yanayojihusisha na masuala ya ukatili wa kijinsia, EfG pekee ndiyo ambayo inajihusisha na kuwasaidia wafanyabiashara katika masoko na kuwapa elimu ya haki za binadamu, sheria na ukatili wa kijinsia," alisema mkurugenzi huyo na kuongeza;

"Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tulivyoweza kutambua kuwa sekta isiyo rasmi inasahaulika ukilinganisha na sekta zingine."

Aidha, Magigita alitumia fursa hiyo kulishukuru Shirika la UN Trust Fund kwa kuwawezesha ili kufikia azma mahususi.

Mkurugenzi huyo wa EfG amesema madhumuni ya kuwepo kwetu hapa leo ni kutokana na azma yetu sote kama taifa na kuungana na mataifa mengine duniani katika kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na pia kuweka msisitizo kwenye utawala wa sheria na upatikanaji wa haki.

"Kama wote tunavyofahamu, chanzo cha maadhimisho haya ni mauaji ya kikatili ya wasichana wa Mirabelle huko nchini Dominika yaliyofanyika mnamo miaka  ya 1960. 
Kutokana na hali hiyo, mwaka 1991, Umoja wa Mataifa ulitenga siku 16 kuanzia Novemba 25 kila mwaka kama siku ya kimataifa ya kuopinga unyanyasaji dhidi ya wanawake. Vilevile, siku ya kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambayo ni Desemba 10," alisema.

Ameongeza kuwa, utafiti unaonyesha wanawake wa Dar es Salaam walio katika sekta isiyo rasmi ndiyo kundi ambalo linakumbwa kwa kiasi kikubwa na ukatili wa kijinsia wawapo nyumbani hata wanapokuwa maeneo yao ya kazi.

Pia utafiti unaonyesha wanawake hao, wanakosa ulinzi toka kwa serikali na mamlaka husika.

"Wanawake wafanyabiashara sokoni ni kundi mojawapo la wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi walioamua kukataa umaskini na kuingia katika harakati za kuinua uchumi wao na familia zao. 

Utafiti uliofanywa na shirika letu la EfG mwaka 2015 ulionyesha kuwa wanawake katika masoko yetu wanafanyakazi kwenye mazingira magumu na wengi wao wakiendesha biashara duni na zenye ufanisi mdogo.

Akisoma risala hiyo kwa mgeni rasmi, Shanisudin Ahmed ambaye ni Katibu wa Ofisi ya Mbunge wa Segerea aliyemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mheshimiwa Bona Kilua ambaye hakufika kutokana na tatizo la kiafya, Magigita alisema;

" Katika masoko kumi yaliyotembelewa  wakati wa utafiti huu uliofanywa kwenye Manispaa ya Ilala na Temeke ulionyesha kuwa asilimia 95.97% ya wanawake wanapitia ukatili wa kijinsia wanapokuwa mahala pa kazi yaani sokoni, wanawake hawa hukosa mitaji ya kutosha wakati wa kuanzisha baishara, wengi hawana elimu ya usimamizi wa biashara na wala hawashiriki katika kufanya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi katika masoko pia ilionekana kwamba hawana dhamana kwa ajili ya kuchukua mikopo, hivyo kubaki na zana na vitendea kazi duni vya kuendesha biashara zao," alisema na kuongeza;

"Ukatili ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara katika masoko ni pamoja na kushikwa maongo ya mwili, lugha chafu na matusi, vitisho, jaribio la kubakwa na kejeli, rushwa ya ngono. Pia utafiti ulionyesha madhara wanayoyapata wanawake hawa katika masoko ambayo ni kushindwa kuzalisha ipasavyo, kuharibika kisaikolojia, kutojiamini, kuwa na hofu, uwoga, kutoheshimika pia kudhalilika," alisema.

Magigita alisema kuwa kupitia mradi wa "MPE RIZIKI SI MATUSI" unaofadhiliwa na Un Trust Fund, shirika limefanikisha kuwafikia wafanyabiashara wapatao 10,250 kwa kuwapa elimu ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia wapatao 1800 ambao mashauri yao yametatuliwa, kutoa rufaa zipatazo 75, masoko 10 yameridhia kuanza kutumia mwongozo wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko, kugawa machapisho yapatayo 5,500 kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali katika kuongeza uelewa wao.

Ameongeza kuwa, wafanyabiashara wameweza kujitambua na wanajua wapi waende kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili, pia kumekuwepo na ongezeko la utoaji wa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa viongozi wa masoko na polisi, maofisa 120 wa vyombo vya ulinzi na usalama wameongeza uelewa juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia, sheria na haki za wanawake jambo lililofanya ukatili masokoni kupungua kwa asilimia 81 kwa mujibu wa utafiti wa Machi 2017 hasa lugha ya matusi na bughudha kwa wanawake.

Mkurugenzi huyo amesema, kupitia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema; "FUNGUKA! UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO HAUMUACHI MTU SALAMA. CHUKUA HATUA" tunakusudia kutoa elimu kwa wafanyabiashara katika masoko yote ili wasikae kimya wanapofanyiwa ukatili wa kijinsia kwani madhara yake ni makubwa sana na yanarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu.

"Ombi letu kwa Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya zinazohusika katika kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ni kuwepo mikakati ya wazi kuhakikisha wanawake katika sekta hii wanapewa kipaumbele ili kuwaweka huru na bughudha zote za ukatili dhidi yao. 

Pia ni muhimu kwa vyombo vya utoaji haki vihakikishe kuwa wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wanapata haki na wale wanaohusika katika kutenda vitendo hivyo wanakumbana na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

"Kwa hili tunaomba jeshi la polisi lishirikiane kwa ukaribu na watoa huduma wetu ambao hutoa huduma ya rufaa kwa wahanga na wapate fursa za kuongeza kipato na kunia uchumi wa taifa," alisema Magigita.

Naye Ahmed aliyemwakilisha Mbunge wa Segerea akizungumza baada ya kusikia risala hiyo alisema amefarijika sana kuona kuwa ili kuinua uchumi na kutokomeza ukatili wa kijinsia si tu kwa wananchi bali kila mtaalam anachukua nafasi yake ili kutoa mchango wake.

"Hili limenipa faraja kubwa mimi binafsi na serikali kwa ujumla hasa hasa katika kuimalishaaa sekta binafsi, mmeweza kuonyesha kwamba kila Mtanzania anafanya bidii kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu katika ukuaji wa sekta isiyo rasmi Tanzania ambayo ipo katika sekta binafsi. Nawashukuru sana EfG kwa kuwa mfano mzuri kwa hili," alisema Ahmed.


Katibu huyo wa Mbunge wa Segerea aliongeza kuwa, Dira ya Taifa inaeleza kuwa Tanzania itakuwa na jamii yenye usawa wa kijinsia ifikapo mwaka 2020. Hatuwezi kufikia dira hiyo tutaruhusu aina ya ukatili wa kijinsia kujitokeza tena au aina mpya kabisa kujitokeza na kukua miongoni mwetu. Tunahitaji kuwa na jamii yenye usawa kijinsia nyakati zote.

"Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati kwa hatua hiyo kubwa ya kupeleka huduma hizo kwa wafanyabiashara kwani mara nyingi baadhi ya wafanyabiashara hawafikiwi katika maeneo yao ya biashara na hivyo kukosa fursa ya kukosa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia," alisema Ahmed.

Friday, December 1, 2017

Mwili wa mwanafunzi uliozikwa, kuzikwa tena...!


Na Dixon Busagaga


MWILI uliofukuliwa hivi karibuni kwa kibali cha mahakama kuondoa utata wa taarifa za kupotea kwa Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica, Humphrey Makundi (16) utazikwa kwa mara ya pili Jumamosi. 



Hatua ya kuzikwa kwa mwili huo uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa zaidi ya siku 14 sasa inatokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Makundi.



Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu Humphrey, Bw. Jackson Makundi alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Mamba kwa Makundi, Marangu wilaya ya Moshi baada ya kupata kibali cha mahakama cha kuruhusu kuzikwa kwa mwili huo.



Makundi alisema shughuli za mazishi ya mwanae yataoongozwa na maaskofu wasaidizi kutoka Dayosisi ya Dodoma akiwemo mchungaji Samwel Mshana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) wakisaidiana na Askofu Msaidizi wa (KKKT) dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Elingaya Saria.





Novemba 6, mwaka huu taarifa za kutoweka kwa mwanafunzi 
huyo katika shule aliyokuwa akisoma ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii na baadae Novemba 7 mwaka huu mwili ulikutwa ukiwa umetelekezwa mto Ghona unaokadiliwa kuwa mita 300 kutoka katika shule hiyo.



Mwili huo ambao awali ulifikishwa katika Hosptali ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi ulipokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na baadae kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga  kama mwili usiokuwa na ndugu.



Hata hivyo, baada ya kuwepo kwa taarifa ya kuzikwa kwa mwili huo, familia ya Makundi iliomba kibali cha mahakama kuruhusu  kufukuliwa mwili huo kwa lengo la kujiridhisha, mtu aliyezikwa kama kweli ni mzee kama taarifa za awali zilivyotolewa au ni ndugu yao. 



Tayari watuhumiwa watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi huyo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Moshi na kusomewa shtaka la mauaji.


Waliofikishwa mahakamani ni pamoja na anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Scolastica, Edward Shayo, aliyekuwa mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha na Labani Nabiswa raia wa Kenya anayetajwa kuwa Mwalimu katika shule hiyo.


Mbele ya mahakama ya Hakimu mkazi, Moshi, upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi, Julieti Mawore uliwakilishwa na Mwanasheria wa serikali Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea, Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anayemtetea Mshatakiwa wa pili katika shtaka hilo Edward Shayo.


Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka mbele ya mahakama hiyo, Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza, Hamis Chacha (28), wa pili Edward Shayo (63)  na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.


Kutokana na maelezo hayo Hakimu, Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.


Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.


Hakimu Mkazi, Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu  na  kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana.


UBA Group Emerges African Bank of the Year

Former British Broadcasting Corporation(BBC) correspondent, Mr. Michael Buerk; Chief Executive, UBA Capital(Europe) Limited, representing UBA Group, Mr. Andrew Martin; and  Editor,  Middle East and Africa, The Banker. Mr. James King, during  The Banker Awards 2017, organised by The Banker Magazine, a publication of Financial Times(FT), where UBA Group coveted five awards, including the prestigious ‘African Bank of the Year 2017’, at a ceremony in London on Wednesday.
                                                                                                                   
PAN-African financial institution, United Bank for Africa (UBA) Plc has once again proven its leadership on the continent, as the Banker Magazine crowned UBA the “African Bank of the Year 2017”. This Banker Award is premier for Nigeria, as it marks the first time a Nigerian-headquartered bank will be wining the prestigious and highly coveted regional award.
To further demonstrate the group’s strength and dominance in the financial sector on the continent, four of UBA Group’s operations in Africa also led contenders in their respective countries to emerge the Best Bank of the Year 2017 in their respective markets. UBA Congo, UBA Tchad, UBA Gabon and UBA Senegal emerged the Best Bank of the Year in Congo, Tchad, Gabon and Senegal, reinforcing the strong franchise of the Group across its chosen markets in Africa. Notably, UBA Gabon and UBA Senegal won the same awards in 2016, as both subsidiaries of UBA Group remain the Banks to beat in Gabon and Senegal.   
A publication of the Financial Times Newspaper, The Banker Magazine is a global financial intelligence magazine that provides global bank ratings/analysis and it is the definitive reference in international banking for high level decision makers globally. According to the magazine, the aim of the award “is to highlight industry wide excellence within the global banking community. The winner is selected from participating banks in each of the 120 countries from which entries are received for the competition.”
Explaining the rationale behind UBA carting multiple categories in its December issue, the Banker’s Magazine noted that Africa’s economic landscape has been unpredictable in recent times which resulted in recession in some of Africa’s best performing economies, while the region as a whole only expanded by about 1.3% in 2016. “In these conditions only the most diversified and innovative of regional banks can prosper. And this is precisely why the United Bank for Africa (UBA) has scooped the 2017 regional winner award. For one, the lender registered impressive top- and bottom-line growth over the review period,” it noted.
The magazine went further to enumerate the various achievements recorded by UBA group during the period, noting that earnings for the year reached N384bn ($1.07bn) signalling 22% growth from its 2015 performance while profit before tax also grew, by 32%, to reach N91bn. According to the organisers, “Equally impressive is UBA’s capital adequacy ratio which, at the end of 2016, stood at 20%, while its nonperforming loan ratio was a healthy 3.9%. Operating across 19 markets in Africa, the bank serves more than 14 million customers.”
It added that the Pan-African bank’s foray into various ventures in Africa also helped to clinch its activities in the year under consideration, stating, “Beyond the numbers, the bank has won and acted on a number of headline deals. These include the financing a new stadium in Douala, Cameroon, for the 2019 Africa Cup of Nations for $285m. In Senegal, more than $250m of trade finance was provided to the state oil company, while the lender acted as arranger and bank agent in the raising of $160m to finance road infrastructure. The bank’s digital tax collection solutions are also helping regional governments in Senegal and Burkina Faso.”
The organisers noted that UBA is making impressive strides in the digital space, adding that in terms of internet banking, the organisation processed 7 million transactions valued at more than N600bn in 2016. Mobile banking processed transactions valued at N70bn over the same period. UBA has also launched eMailMoni, a service that lets customers transfer funds via e-mail, while Chat Banking allows clients to perform basic transactions through social media platforms. “For these reasons, and others, UBA is the winner of our 2017 African Bank of the Year award,” the Magazine stated.
The Group Managing Director/Chief Executive Officer, UBA Plc, Mr. Kennedy Uzoka, who was delighted by the recognition from The Bankers said; “These awards mark another milestone for UBA Group and is a testament of the diligent execution of the bank’s strategic initiatives on customer service. Being recognized as Africa’s best bank complements positive feedback from customers and is a recognition of our improving efficiencies, service quality and innovation. I therefore dedicate it to our growing loyal corporate and retail customers, who are our essence. Given our heritage commitment to Africa’s development, we continue to impact lives through our service as well as funding to individuals, businesses and government.”
Uzoka added; “The bank remains focused on its goal of democratizing banking in Africa, leveraging on new technologies and our rich pool of talent. It is satisfying that our efforts towards leadership are yielding great results. We continue to gain market share across our chosen markets, as we deepen financial inclusion, meeting basic and complex financial service needs of the growing African population. We are Africans and determined to change the narrative of financial services in Africa and this is just the beginning,” he noted.
On his part, Mr. Emeke Iweriebor, Regional CEO, UBA Francophone Africa, described the awards as exciting, stating that the bank’s great work in Africa is increasingly being recognized.
Iweriebor who dedicated the awards to the bank’s esteemed customers, said “Our pioneering innovations in the African banking sector are undoubtedly critical to the growth and development of the continent. Africa’s banking sector has come a long way but we still have a lot to do. We at UBA Group are dedicated to being a critical part of this transformation.”
He added that the bank will continue to leverage its local knowledge, global exposure as well as presence to drive positive change in Africa, working actively with the government, local businesses, regulators and other stakeholders in deepening financial services.
The Banker award’s “Bank of the Year Awards” are widely regarded as the Oscars of the Banking Industry.  For 90 years, The Banker has been the world’s leading monthly journal of record for the banking industry.  The organisers note that the aim of the awards programme is to highlight industry wide excellence within the global banking community.
The Banker selects one winning bank for each of the 120 countries that are covered. Over 1,000 applications are entered and judges select winning banks based on the ones that have made most progress over the past 12 months.
UBA was incorporated in Nigeria as a limited liability company after taking over the assets of the British and French Bank Limited who had been operating in Nigeria since 1949. The United Bank for Africa (UBA) Plc merged with Standard Trust Bank in 2005 and from a single country operation founded in 1949 in Nigeria - Africa's largest economy - UBA has become one of the leading providers of banking and other financial services on the African continent. The Bank provides services to over 14 million customers globally, through one of the most diverse service channels in sub-Saharan Africa, with over 1,000 branches and customer touch points and robust online and mobile banking platforms.
UBA was the first Nigerian bank to make an Initial Public Offering, following its listing on the NSE in1970. It was also the first Nigerian bank to issue Global Depository Receipts. The shares of UBA are publicly traded on the Nigerian Stock Exchange and the Bank has a well-diversified shareholder base, which includes foreign and local institutional investors, as well as individual shareholders.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...