Wednesday, September 27, 2017

Harusi ya Lusajo Mwangambaku na mkewe Neema Stanley

 Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofanyika Ukumbi wa Mirando Sinza jijini Dar es Salaam juzi. Bwana harusi anatoka Tukuyu mkoani Mbeya na Bibi Harusi anatoka Mkoa wa Morogoro.


Wapambe wa maharusi hao wakiwa kwenye pozi. Kulia ni Bwana Yohana na mkewe Bi. Jenifa Yohana.

Maharusi  wakiwa na wapambe wao.

 Mama wa bwana harusi akichukua msosi.

 Msanii wa kujitegemea akitoa burudani.

 Maharusi wakiserebuka kwa raha zao na wafanyakazi wenzao 
wa Serena Hoteli.

 Mziki ukiendelea.

 Mserebuko ukiendelea.

 Bwana harusi akiwa amepozi na mama yake,  Hilda Mulinde. Da kumbe harusi ni tamu.




 Sherehe ikiendelea.

 Wacheza shoo wakionesha umahiri wa kucheza kabla ya maharusi kuingia ukumbini.

 Maharusi wakiwa na Kulwa na Dotto Mwaibale katika 
sherehe hiyo.

 Maharusi wakiingia ukumbini.

 Shoo ikifanyika.

 Kamati ikienda kujitambulisha.

 Mwenyekiti wa Kamati ya harusi hiyo, Desdery Dotto akizungumza.

 Mama wa bwana harusi akisalimia wageni waalikwa.

 Maharusi wakikata keki.

 Mke akimlisha  keki na mmewe.

 Mme akimlisha keki mkewe

 Mama na mkwewe wakikumbatiana kwa furaha.

 Shampeni zikifunguliwa.

 Mume na mke wakinyweshana mvinyo.

 Wageni waalikwa wakiwapongeza maharusi.

 Dereva wa maharusi hao,  Mariam Mkumbukwa kutoka Europcar akiwa na furaha katika hafla hiyo.

 Picha ya pamoja hiyo.

Wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakiwa katika picha ya pamoja na maharusi hao.

Monday, September 25, 2017

Wananchi Kata ya Kibwegere walia na vitendo vya Kijambazi

IGP Simon Sirro.


Na Dotto Mwaibale









WANANCHI wa Kata ya Kibwegere, Kibamba wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam wameiomba Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kuwasaidia kupunguza vitendo vya wizi vinavyofanywa na baadhi ya makundi ya vijana katika eneo hilo na kuhatarisha maisha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na kuomba majina yao kutoandikwa kwa usalama, wananchi hao walisema hali siyo shwari katika eneo hilo kufuatia vijana hao kualika wenzao kutoka maeneo mengine na kwenda kufanya vitendo vya ujambazi.

"Tunaiomba kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itusaidie kukabiliana na vitendo hivi vya wizi vinavyofanywa na hawa vijana kwa kushirikiana na wenzao kutoka maeneo mengine," alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Mkazi huyo alisema katika vipindi tofauti vijana hao walifanya tukio la ujambazi kwa kuvamia nyumba tatu katika eneo hilo na kusabisha vifo vya watu wawili ambao waliwataja kuwa ni Mwalimu wa shule moja ya awali iliyopo eneo hilo na mzee Kaberege ambao waliuawa katika matukio yaliyofanyika mwaka jana huku wengine wakijeruhiwa.

"Matukio haya yote ya wizi wa kuvunja fremu za biashara, wizi wa mifugo kama nguruwe na ng'ombe yamekuwa yanafanyika lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na polisi hali inayotukatisha tamaa wananchi," alisema mzee wa eneo hilo.

Mzee huyo aliongeza kuwa vijana hao wamekwisha fanya matukio mengi ya uhalifu bila kuogopa polisi kwa kuingia kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo zaidi ya mara moja  lakini polisi hawajachukua hatua yoyote hadi mpaka wananchi wanapoteza imani na jeshi hilo hasa kituo cha Mbezi Mwisho kwa kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo.

Aliongeza kuwa viongozi wa eneo hilo wameshindwa kushughulikia suala hilo kwa kuwa baadhi ya watoto wao ni wahusika wa matukio hayo na kuwa polisi hawafiki kwa wakati wakipatiwa taarifa na upelelezi wa kesi kuhusu matukio hayo unachelewa hivyo kuwazidishia hofu wananchi.

Alitaja maeneo wanayopenda kukaa vijana hao kuwa ni karibu na nyumba moja isiyoisha ujenzi wake - pagala - iliyopo karibu na nyumba ya mjumbe aliyetajwa kwa jina la baba Elia na eneo la karibu na ghara la pikipiki la Masawe na nyuma ya maabara moja ya Mama Gema.

Wananchi hao wamemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro, kuwasaidia katika jambo hilo linalorudisha maendeleo yao nyuma ikiwezekana wawekewe kituo kidogo cha polisi eneo hilo ukizingatia kile wanachokitegemea cha Kibamba CCM kufungwa kuanzia saa 12 jioni hivyo kutoa mwanya kwa wahalifu kufanya matukio yao bila ya woga.

Vijana wanaofanya matukio hayo wamedaiwa kuvaa mavazi ya kike madera ili waweze kuficha siraha zao na kupita kirahisi barabarani bila ya kutambuliwa na kushukiwa kiurahisi.

"Tunaomba viongozi wa serikali kuingilia kati baadhi ya maeneo ambayo hayajaendelezwa maana yamekuwa vichaka vya kujificha wahalifu kabla na baada ya matukio," alisema mzee huyo.

Alisema hapo Kibwegere kunamaeneo mengi ambayo hayajaendelezwa zikiwepo nyumba ambazo hajijaisha ujenzi wake hivyo wanamuomba waziri mwenye dhamana kutembelea eneo hilo ikiwezekana kuyarudisha serikalini ili kusaidia kuondoa kero hiyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Kibwegere CCM, aliyejulikana kwa jina moja la Nyingi, alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kueleza kuwa wananchi wamekuwa wagumu katika ushirikishwaji wa ulinzi katika eneo hilo.

"Tulijaribu kuwashirikisha wananchi katika suala zima la ulinzi na usalama katika eneo letu kwa kufuata muongozo wa Jeshi la Polisi lakini muitikio ulikuwa mdogo kwani kuna baadhi yao walidai wao hawana vitu vya thamani hivyo walio na uwezo ndio washiriki mchakato huo.

"Hatujui ni nini kilichowafanya washindwe kujitokeza katika jambo hili lakini hapa kwetu kunachangamoto kubwa ya wananchi kujitokeza katika shughuli za maendeleo kwa mfano ujenzi wa hata madarasa ya shule watu hawajitokezi licha ya kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi kwa kukosa madarasa," alisema Mwenyekiti huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo, alisema kuwa mfumo wa ulinzi uliopo kuanzia kamati ya ulinzi na usalama ngazi ya kata unawasaidia polisi kujua changamoto za wizi zilizopo katika maeneo hayo hivyo hata tukio la uhalifu linapotokea polisi hufika kwa wakati eneo la tukio.

"Katika kila kata Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa husika na wao ndio wanatoa taarifa polisi ya tukio lolote la uhalifu na katika maeneo hayo unayoyataja sijapata taarifa zozote za uhalifu nakuomba wasiliana na viongozi hao kwanza halafu unipe mrejesho," alisema Kamanda Muliro.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Werema Werema hakutofautia na maelezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibwegere CCM kuhusu changamoto iliyopo ya wananchi kushiriki katika suala zima la ulinzi na usalama katika eneo hilo.

"Kama ulivyoongea na mwenyekiti na mimi siwezi kuwatofauti naye kwani aliyoongea ndio niliyonayo hivyo kama ni kupata ya nyongeza karibu ofisini tuzungumze," alisema Werema. 

Sunday, September 24, 2017

IGP Sirro awataka vijana kutokimbilia nje ya nchi na kuacha fursa

  Kamishna wa Polisi Mussa Ali Mussa, akiwa amebeba mfano wa picha ya ndege wa kuashiria amani, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.


 Maandamano ya kuadhimisha siku hiyo yakifanyika.

 Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.

 Wawakilishi mbalimbali na viongozi wa dini  wakiwa wamebeba mfano wa ndege huyo.

 Maadhimisho yakiendelea.

 Sheikh Hemed Bin Jalala akizungumzia umuhimu wa amani nchini

 Afisa Habari Kitengo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo, akizungumzia ushiriki wa UNIC katika kudumisha amani.

 Wanahabari wakiwa kazini katika maadhimisho hayo.

 Wananchi wakishuhudia maadhimisho hayo.

 Wasanii wakionesha umahiri wa kucheza na nyoka katika maadhimisho hayo.

 Kiongozi wa Chama cha Scout Tanzania, Kamishna Mkuu Msaidizi Kazi Maalum, Mary Anyitike akiwa na vijana wake kwenye maadhimisho hayo.

 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi, akihutubia. Kutoka kulia ni Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Suzan Kaganda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam SACP, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi (ACP), Emanuel Lukuya na  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa.

  Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa, akihutubia.

 Maadhimisho yakifanyika


Scout wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi mbalimbali.

Na Dotto Mwaibale

VIJANA wametakiwa wasipishane na fursa kwa kwenda nchi ya nchi kuzitafuta wakati wenzao wa nchi hizo wakija kunufaika nazo hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na Kamishina wa Polisi Mussa Ali Mussa wakati akihutubia kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani-Tanzania yaliyofanyika leo Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

"Vijana acheni mipango ya kwenda kuzitafuta fursa nje ya nchi kwani wenzenu kutoka nchi hizo wamekuwa wakija kunufaika nazo hapa nchini" alisema Mussa.

 Alisema serikali imeweka mazingira mazuri hivyo ni vizuri hali hiyo ikatumika kwa ajili ya kufanya shughuli za maendeleo hasa katika wakati huu nchi ikiingia katika uchumi wa viwanda.

Aliwataka wazazi na walezi kutoa malezi bora kwa watoto wao ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi yasiofaa.

Katika hatua nyingine Kamishna Mussa alisema amani ya nchi itadumishwa na kila mtu na kuwa watu waondoe dhana ya kuwa amani hiyo italetwa na vyombo vya dola ikiwemo polisi.

Alisema suala la amani si la mtu mmoja bali ni la kila mtu jeshi la polisi kazi yake ni kuilinda na kumkamata mtu yeyote anayeonekana kusababisha viashiria vya kutoweka kwa amani hiyo.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Shirika la UN linaloshughulikia wahamiaji la IOM,  Dk. Quasim Sufi alisema amani ni jambo la muhimu kwa nchi na mustakari wa maendeleo.

Alisema bila ya amani hakuna kitu kitakacho weza kufanyika na ndio maana UN imekuwa ikisisitiza amani duniani kote.

Sheikh Hemed Bin Jalala alisema amani ndiyo msingi wa dini zote ya kiislam na kikristo na kuwa amani haipaswi kuchezewa kwani ndio neema tuliyopewa na mwenyezi mungu.

Jalala alisema amani ni msingi wa dini uliojengwa kiimani na kutakiwa kuihubiri na kuwa wale wanaohubiri vita na machafuko wanatoka katika dini ya mashetani.

Afisa Habari Kitemgo Cha Habari cha Umoja wa Mataifa-UNIC, Stella Vuzo aliwataka vijana kuendelea kuidumisha amani iliyopo nchini kwani wao ndio rahisi kurubuniwa kutokana na kuwa wengi.

"Katika maadhimisho ya siku ya amani duniani tunapenda kuwashirikisha vijana kutokana na wingi na umuhimu wao katika kutunza amani" alisema Vuzo.

Alisema vijana watumie fursa ya amani iliyopo nchini katika kufanya shughuli zao za  maendeleo badala ya kukaa bure.

Vuzo alisema Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni  " Pamoja Katika Kudumisha Amani: Heshima, Usalama na Utu kwa wote"

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na taasisi mbalimbali kama  Global Peace Tanzania, Global Network of Religions for Children- GNRC, Chama cha Scout Tanzania, Asasi ya Vijana wa Umoja wa mataifa YUNA Tanzania, wanafunzi na wananchi.

Saturday, September 23, 2017

TCRA yawataka wamiliki mitandao ya kijamii kuitumia kwa manufaa

 Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jones Kilimbe akifungua rasmi warsha ya vyombo vya Habari Mtandaoni iliyo wahusisha Blogu na 'Online Tv' katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa J.K Nyerere Jijini Dar es salaam.

 Bw. Thadeus Lingo kutoka TCRA akiendesha mada kuhusu Matumizi Salama ya Mitandao ya Kijamii.

 Mwakilishi wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Maxence Melo akiwasilisha mada juu ya Maudhui ya Mtandaoni na Changamoto zake.

 Mratibu Msaidizi wa Polisi Joshua Mwangasa akitoa mada juu ya Hali ya Usalama Mtandaoni.



 Mzee Abdul Ngarawa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka TCRA akitoa neno la Busara wakati wa warsha hiyo ambapo alisisitiza kuzingatia uzalendo umuhimu wa kutazama utu na staha ya mtu



 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (Kushoto) akiongoza majadiliano kwa ujumla ambapo wadau walichangia mawazo na kuuliza maswali mbalimbali.



Bwana Daniel Mbega Mmiliki wa Blogu ya Maendeleo Vijijini akichangia mawazo yake wakati wa warsha hiyo.



 Bw. William Malecela Maarufu kwa jina la Le Mutuz mmiliki  Blogu ya Wananchi na Le Mutuz Tv Onine akichangia mambo mbalimbali na kutoa maoni yake wakati wa Warsha hiyo

 Mwenyekiti wa  Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Joachim Mushi (kulia) akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya waendeshaji wote wa mitandao kwa TCRA kuendesha warsha hiyo.



  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba pamoja na wadau wengine wakizindua Rasmi Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii awamu ya Pili ambapo Kauli mbiu inasema "Usinitumie Sitaki na Simtumii Mwengine Nitakuripoti"




 Baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo.




 Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. Valerie Msoka akitoa neno la kufunga wakati wa Warsha hiyo.





 Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo




Na Paschal Dotto-MAELEZO

Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasiliano kwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzania kupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi uliobora.

Haya yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas Kilimbe  alipokua akihutubia hadhara ya wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii”  iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Katika hafla hiyo, Dkt. Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya mitandao kuwa makubwa.

“Sekta ya mawasiliano kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema Dkt.Kilimbe.

Aidha Dkt.Kilimbe alisema kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.

“Tuna jukumu zito na ni kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyo waandishi mitandaoni tumieni weledi  mkubwa kwa habari za maendeleo.”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.
Dkt.Kilimbe alisema kuwa katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa  kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.

Aidha Dkt. Kilimbe amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umilikajia wa vyombo hivyo kwa kuwahabarisha wananchi.

Naye mtoa mada na mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika katika kuhabarisha umma kwa njia hii.

Picha zote na Fredy Njeje.
 

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...