Sunday, June 12, 2016

Kampuni ya kigeni inapotumia mbinu chafu kuidhalilisha serikali

Gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris likiwa limeshikiliwa kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukutwa na shehena ya bangi.
Na Mwandishi Wetu

BIASHARA ya utalii imekuwa na ushindani mkubwa si nje bali hata ndani ya nchi yetu. Ushindani wa kibiashara unadhihirishwa na jinsi ambavyo makampuni ya ndani na nje yanavyopigana vikumbo kutafuta njia na mbinu za kuwapiku washindani wao.
Hilo ni jambo la kawaida kabisa.

Hakika pale ambako hapana ushindani basi ni wazi pia kwamba hapatakuwapo na tija kwani mama wa biashara huria ni ushindani na hilo hakuna wa kubishana. Hata hivyo, kuna mvutano ambao umeanzishwa na kampuni ya Wengert Windrose Safaris Limited, kampuni tanzu ya Friedkin Conservation Fund (Friedkin Family Tanzania) dhidi ya serikali ya Tanzania ambao hauna tija kwa pande zote mbili na ambao unahitaji kumalizwa kwa sababu umeendelea kuikosesha nchi mapato.

Kampuni nyingine ni Tanzania Game Trackers Safaris Limited na Mwiba Holdings Limited.
Kampuni hiyo imeingia katika mvutano na serikali kuanzia mwaka 2013 wakati msimu mpya wa uwindaji wa kitalii ulipoanza, hasa pale walipokosa moja ya vitalu walivyoomba katika utaratibu wa ushindani. Kitalu hicho kilijulikana kwa jina la Lake Natron Game Controlled Area (North). Baadaye kitalu hiki kilikuja kujulikana kama Lake Natron Game Controlled Area (East), ambacho kiligawiwa kwa Green Mile Safari Company Limited baada ya ushindani.

Kitalu hiki cha uwindaji wa kitalii ndicho kimekuwa luba na kufanya mahusiano kati ya kampuni hiyo na serikali kuyumba sana hadi leo takriban miaka mitatu baada ya kampuni hiyo kukosa umiliki katika mchakato wa ushindani. Katika mazingira ya kawaida kampuni ya kigeni inayofanya biashara hapa nchini kwa kutumia sheria za Tanzania haina budi kukubaliana na sheria, na kama kuna kutoridhika na chochote inatakiwa kwenda mahakamani kutafuta haki.

Hata hivyo, baada ya kampuni hiyo kwenda mahakamani mara kadhaa kutafuta haki ya kumilikishwa kitalu hicho ikashindwa kuipata imeamua kuendeleza vita dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vya habari. Tena vita hiyo ambayo inaendeshwa kwa kutumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ilihamishiwa hadi katika Baraza la Congress la Marekani.

Shehena ya bangi ikishushwa kwenye gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris katika kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukamatwa.
Baraza la Congress liliaminishwa na wamiliki wa kampuni hiyo ya Wengert ambayo ni ya Kimarekani kwamba Tanzania ni nchi ya hovyo ambayo sheria hazifuatwi hata kidogo.
Kampuni ya Wengert ikafikia hatua ya kuliaminisha Baraza hilo kwamba imetendewa ndivyo sivyo nchini kwa kunyang'anywa kitalu kinyume cha sheria na kwamba kitendo hicho kimefanyika kinyume cha sheria.

Katika kulighadhibisha Baraza hilo Wengert wakadai kwamba imenyang'anywa kitalu na kupewa kampuni nyingine ya kigeni. Hiyo ya kudai kwamba imenyang'anywa kampuni ya Kimarekani na kupatiwa kampuni nyingine ya kigeni ni katika ile ile tabia ya kutaka kuwachochea watunga sheria hao wa Marekani kwa kutumia kigezo cha kwamba wao ni bora zaidi hivyo haiyumkiniki akanyang'anywa Mmarekani halafu apewe mgeni mwingine!
Uchochezi huo ukatumika kwa malengo ambayo kampuni ya Wengert ilitaka.

Baraza la Congress la Marekani lilimwandikia Rais wa Marekani, Barack Obama, barua likiituhumu Idara ya Wanyamapori kwa kuinyanga’anya kampuni ya Wengert kitalu na kukitoa isivyo halali kwa Kampuni nyingine, jambo ambalo halikuwa kweli. Hata hivyo, ukweli ni kwamba kampuni iliyogawiwa kitalu hicho ni ya Kitanzania.
Kampuni hiyo haikutaka kusema ukweli kwamba uamuzi wa kutogawiwa  kitalu ulitokana na maamuzi ya kamati ya ugawaji wa vitalu na kamwe sio kutokana na uamuzi wa Idara ya Wanyamapori.

Vitalu hugawiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii baada ya kushauriwa na kamati ya ugawaji wa vitalu. Tuhuma hizo za uongo zilipelekwa mbele ya Baraza la Congress baada ya rufaa yao waliyokata kupinga ugawaji wa vitalu kukataliwa. Ni wazi kabisa kwamba ushawishi uliofanywa kwa Baraza la Congress kwa kutumia mbinu chafu na uongo uliokithiri ulilenga katika kuiweka katika shinikizo serikali ya Tanzania ili iende kinyume na maamuzi yake halali yaliyofanayika kwa mujibu wa sheria.

Wengert walikwenda mahakamani mara kadhaa kupinga maamuzi hayo ya serikali na mara zote wamegonga ukuta. Wiki iliyopita walishindwa kwa mara ya nne mahakamani katika jitihada zao za kutaka kuthibitisha kwa kutumia vielelezo wanavyodai ndivyo halali kwamba kuna makosa katika ugawaji wa vitalu katika eneo la Lake Natron Game Controlled Area. Imefikia hatua kampuni ya Wengert inadai kwamba nyaraka rasmi za Serikali ya Tanzania ni batili na kwamba yenyewe ndiyo ina ramani halali na nyaraka mbalimbali kutoka serikalini.

Inachekesha sana kwamba kampuni ya kigeni inakuja nchini na kuamua kupambana na serikali yetu kwa ajili ya kulazimisha umiliki wa kitalu cha uwindaji wa kitalii kwa kila njia ikiwa ni pamoja na kuvifunga midomo vyombo vya habari kwa kutumia mbinu chafu. Kwa taarifa rasmi za kiserikali ni kwamba kampuni hiyo, pamoja na kampuni nyingine za Friedkin Family Tanzania, zimekuwa zikiwatumia watumishi wake na mawakala mbalimbali kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya makampuni mengine ya uwindaji wa kitalii.

Aidha, kampuni hiyo pia imekuwa ikiendesha kampeni chafu dhidi ya viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kutaka kuthibitisha kwamba viongozi hao wanafanya maamuzi yasiyozingatia sheria. Ukweli ni kwamba kampuni hizo ndiyo zimekuwa mstari wa mbele kutotii sheria za nchi.

Tabia hii ilishamiri sana wakati wa awamu iliyopita. Kumekuwapo na jitihada za kuitaka kampuni hiyo iendelee kufanya shughuli zake za kitalii katika maeneo halali iliyokabidhiwa na serikali ya Tanzania lakini kila uchao kumekuwapo na tuhuma za kila aina dhidi ya wadau wengine wa sekta ya utalii na serikali kutoka kwa kampuni hizo.

Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari hiyo akiwa ameshikiliwa na polisi.
Inasikitisha kwamba kampuni hizo hazioni kwamba ni bora kuachana na malumbano yasiyokuwa na tija na badala yake kuendelea na kazi kama zinapenda kuendelea kuwekeza Tanzania vinginevyo kama zinafikiri zinaonewa ziondoke nchini kwa sababu Tanzania sio nchi pekee ambayo wanaweza kufanya biashara ya uwindaji wa kitalii. Katika kuthibitisha kwamba kampuni hizi hazina hata chembe ya ustaarabu, wamediriki kuwafuata wageni wa kampuni shindani na kuwafanyia fujo jambo ambalo liliripotiwa serikalini.

Aidha, katika kuthibitisha uwezo wake wa kufanya mambo ya hovyo upo ushahidi kwamba watumishi au mawakala wa kampuni hiyo walichimba mashimo katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kwenye moja ya vitalu vya washindani wao eti tu kwa sababu uwanja huo waliutengeneza wao wakati wanamiliki kitalu hicho.

Swali kubwa linalojitokeza katika vurugu hizi za makampuni haya ya Kimarekani ni kwamba nani anayewachochea na kuwavimbisha kichwa kiasi cha kuidhalilisha serikali ya Tanzania huku wakiwa nchini? Kwa nini hadi leo hatusikii hatua za kinidhamu na hata kisheria dhidi ya kampuni hizii ambayo inaonekana kila uchao yanazidisha mapambano dhidi ya serikali yetu? Tusiruhusu mwekezaji yeyote yule kutupanda kichwani, hata kama anatoka taifa linalojigamba kuwa taifa kubwa duniani! Tunachohitaji kwa wawekezaji ni wao wanufaike na sisi pia tunufaike.

Serikali Kuwatumbua Wanaopokea Rushwa Kwenye Mizani

Muonekano wa ujenzi wa kituo cha Mzani Itigi, kinachojengwa katika barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya, mkoani Singida.

SERIKALI imesema itachuku hatua kali ikiwemo kumfukiza kazi na kumfikisha mahakamani mfanyakazi wa Mizani atakayebainika anajihusisha na vitendo vya kupokea rushwa ili kuruhusu magari kupita bila kupimwa uzito.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga wakati alipokagua huduma za upimaji uzito wa Magari katika Mzani wa Njuki Mkoani Singida. Alisema hadi sasa kuna baadhi ya wafanyakazi wa Mizani wameachishwa kazi kutokana na kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa madereva wa magari ya Mizigo na abiria.

“Hatutasita kuchukua hatua kwa mfanyakazi yeyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa, hatua kali tutachukua dhidi yake ikiwemmo kumfikisha mahakamani”. Amesema Eng. Nyamhanga.

Badala yake Eng. Nyamhanga amewataka wafanyakazi wote wa Mizani nchini kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa Mizani ili kuweza kuleta ufanisi katika vituo vya kazi.

Pia amewataka madereva wa magari na abiria nchini kushirikiana na Wizara hiyo kwa kutoa taarifa za Wafanyakazi wa Mizani wanaowaomba rushwa ili kuweza kuondoa kero hiyo kwa wananchi wanaotumia hudum za Mizani nchini. Vile levile amewaasa madereva wa magari ya mizigo kutozidisha uzito wa mizigo kwenye magari ili kuepusha uharibifu wa barabara ambazo hujengwa kwa kutumia kodi za wananchi.

“Madereva mnawajibu wa kulinda barabara hizi kwa kutozidisha uzito wa mizigo kwenye magari yenu ili kuziwezesha barabara zetu zidumu kwa muda mrefu”. Amesisitiza Eng. Nyamhanga.

Aidha, Eng. Nyamhanga amesema Wafanyabiashara na madereva wa magari makubwa ya mizigo yaendayo nje ya nchi kuchangamkia fursa ya kuwapo kwa stika maalum za magari hayo kwani kutapunguza idadi ya vizuizi vya upimaji wa uzito na hivyo kuharakisha safari zao.

Naye Msimizi wa Mzani wa Njuki Mnanka Chile amewaomba madereva wa magari kuzingatia sheria na kanuni za alama za barabarabi na kuwa makini pindi wanapokaribia seheme za Mizani ya kupimia uzito wa Magari.

Katibu Mkuu Eng. Josph Nyamhanga yupo katika ziara ya kukagua Miradi ya Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, Vivuko na huduma za Mizani katika Mikoa ya Dodoma, Manyara Singida na Mara.

Imetolewa na kitenga cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kampuni ya Tigo yampa kongole msanii Christian Bella


Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga akiongea na waandishi (Hawapo pichani )kuhusu udhamini wa Tigo kwenye tamasha la kutimiza miaka 10 ya Christian Bella zilizofanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita katika viwanja vya Escape One kushoto kwake ni Mwimbaji wa mahiri wa dansi nchini Christian Bella .


Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe ya kutimiza miaka kumi katika tasnia ya muziki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita , kushoto kwake ni William Mpinga Meneja Chapa wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo.


Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga akimkabidhi simu aina ya Iphone 6 Msanii Christian Bella ikiwa ni  kumpongeza kwa kutimiza miaka 10 katika tasnia ya muziki  mapema mwisho wa wiki iliyopita  ambapo tigo pia walidhamini tamasha hilo 

Saturday, June 4, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Azinduwa Jengo la Upasuaji Kituo cha Afya Mwera, Pangani



MKUU WA MKOA WA TANGA,MH.MARTINE SHIGELLA AKIZUNDUA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI (OPERATING THEATRE) KATIKA KITUO CHA AFYA MWERA LEO IJUMAA JUNE 3 WA KWANZA KULIA NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI AMBAYE PIA NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA ESTERINA KILASI




KULIA NI MGANGA MFAWIDI WA KITUO CHA AFYA CHA MWERA WILAYANI PANGANI DR.MADARAKA RAPHAEL AKISISITIZA JAMBO KWA MKUU WA MKOA WA TANGA, MH., MARTINE SHIGELLA WAKATI ALIPOTEMBELE UJENZI HUO KUSHOTO NI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA PANGANI,




MH.MKUU WA MKOA WA TANGA,MARTINE SHIGELLA AKISOMA JIWE LA MSINGI WA PILI KULIA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA MHANDISI ZENA SAID





MKUU WA MKOA WA TANGA,MH MARTINE SHIGELLA AKIZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA





BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MKUU WA MKOA WA TANGA,MH,MARTINE SHIGELLA ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NAO LEO











KATIKATI NI MKUU WA MKOA WA TANGA,MH,MARTINE SHIGELLA AKIVUKA NG'AMBO YA PILI YA PANGANI KWA KUTUMIA KIVUKO LEO WA MBELE YAKE NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI,MH,ESTERIA KILASI











MKUU WA MKOA WA TANGA,MH.MARTINE SHIGELLA KATIKATI AKISHUKA KWENYE KIVUKO CHA MTO PANGANI KUSHOTO KWAKE NI KAIMU MKUU WA WILAYA YA PANGANI, ESTERIA KILASI AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA MUHEZA NA KULIA NI KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA, MHANDISI ZENA SAID.
 Picha kwa Hisani ya Blog Tanga Raha.


Unyayo Wangu; David Manoti Azungumzia Adhabu ya Wabunge wa Upinzani Bungeni...!

Unyayo wangu; Kipindi kipya cha Tone Tv:-
 


Wednesday, June 1, 2016

USAID wahaidi kuendelea kuisaidia miradi anuai Tanzania




Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya serikali ya Marekani katika mkutano wa hitimisho wa mradi wa SCMS.

Na Rabi Hume, Dar

BAADA ya mradi wa SCMS kufanyika nchini kwa miaka 10, huku ukisimamiwa na taasisi ya John Snow Incorporated (JSI) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) limeiahidi serikali ya Tanzania kuwa litaendelea kuisaidia katika misaada mbalimbali ya afya licha ya kumalizika kwa mradi huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa USAID nchini, Tim Donnay katika mkutano ambao ulikutanisha wadau mbalimbali wa afya ili kujadili mradi wa SCMS ambao umefikia tamati baada ya kufanyika nchini kwa miaka 10.

Bi. Donnay alisema serikali ya Marekani kupitia USAID imejipanga kuendelea kuisaidia Tanzania katika sehemu mbalimbali ambazo zinahusu Afya.

“USAID itaendelea kuisaidia Tanzania ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya upatikanaji wa huduma bora wa kiafya ... kumalizika kwa mradi huu hukutafanya kusitishwa kwa huduma ambazo zinatolewa kwa sasa,” alisema Bi. Donnay.

Naye mgeni rasmi katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Mpoki Ulisubya alisema kufanyika kwa mradi huo nchini kumewezesha kusaidia kuboreshwa kwa kasi huduma za afya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Mradi huu umetusaidia sana awali hata utolewaji wa dawa kwa waathirika wa UKIMWI ulikuwa ni laki na nusu kwa mwaka ila kwa sasa kuna upatikanaji wa dawa hadi laki nane kwa mwaka,

“Mbali na hiyo pia wametujengea maghala ambayo yanatumika kuhifadhi dawa na hata kusaidia kuweza kuwasogezea huduma wananchi ambazo awali hazikuwa zikitolewa,” alisema Ulibusya.

Happy Birthday to You Josephat Lukaza...!

Kwanza Napenda kuchukua Nafasi hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuniwezesha kuiona siku ya Leo maana Si kwa uwezo wangu bali ni kwa Uwezo wake Muumba wetu aliye Juu.
Leo ni siku muhimu sana kwangu maana inanikumbusha siku niliyoletwa Duniani na Mungu kupitia Mama yangu kwa kusudi maalumu hapa duniani.
Napenda Kumshukuru Mungu kwa maana neema na rehema zake ni Za milele. Nasema asante kwa kunifanya kuongeza mwaka mwingine huku nikiwa na afya njema. Kiukweli Sina cha Kumlipa Mwenyezi Mungu zaidi ya Kumsifu na Kumwabudu yeye kwa maana Sio kwa uwezo wangu.Napenda kuwashukuruni wote Ambao Mmekuwa mkiniombea na kunitakia heri ya kuzaliwa kwangu Nasema asante na Mungu awabariki sana.
Nakukabidhi wewe bwana njia zangu na kukutumainia kwasababu umeagiza kila akukabidhie njia zake na kukutumainia unaenda kumtendea. Zaburi 37: 5 Leo nasema asante sana kwa Maana kila napokuita Wewe unaitika.
Naomba pia uendelee kuziimarisha hatua zangu kwa maana uliagiza katika Zaburi 37:23 Kuwa "Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake"
Hakika wewe ni Mungu wa Wote.
Nachukua fursa hii kuwa shukuruni wote Ambao mmenitakia baraka na heri katika siku hii muhimu sana kwangu ambayo inanifanya nitafakari matendo yangu hapa duniani, Uhusiano wangu na Mungu wangu, Uhusiano wangu na Ndugu zangu, Uhusiano na Jamii yangu pamoja na rafiki zangu hakika Namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kupatana na Ndugu zangu, jamii yangu na hata marafiki zangu. Kiukweli Namshukuru Mungu kwasababu Ni kwa neema zake na Rehema zake ndio zimenifikisha hapa wala sio kwa ujanja wangu wala mimi sio mwema sana kuzidi wengine.
Wewe Ni Mungu wa wote, Huchelewi wala Huwahi Hakika nitakusifu na kukuabudu siku zote za maisha yangu kwa maana matendo yako makuu uliyonitendea Nayaona na kuyafurahia.
Asante sana Mungu wangu naomba uendelee Kutimiza haja za Moyo wangu. Nitaendelea Kukushangilia na Kukusifu kwa maana kila napokuita unaitika.
Happy Birthday to You Josephat Lukaza - Lukaza Blog

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...