![]() |
| Picha ya pamoja kati ya meza kuu, mgeni rasmi na viongozi na kamati ya mkutano huo. |
Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Thursday, April 28, 2016
Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar
DC Moshi Atembelea Maeneo Yaliyozungukwa na Mafuriko...!
![]() |
| Maeneo mbalimbali, zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharibika. |
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.
Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.
Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.
Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.
Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.
Maashamba yamejaa maji.
Maeneo mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.
Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.
Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu. Picha na Dixon Busagaga, Kilimanjaro.
Tuesday, April 26, 2016
Tumbuatumbua ya Rais Dk Magufuli Yatua TCRA Mkurugenzi Mkuu, Bodi Nje
![]() |
| Muonekano wa Jengo la Makao Makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam. |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.
Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.
“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016
Polisi Kilimanjaro Yakamata Shehena Kubwa ya Dawa za Kulevya na Silaha
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, kamishna msaidizi, Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.
Kamnad wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto 4500 pamoja na kilogramu 10 za bhangi ambayo haijasokotwa iliyokamatwa wilaya ya Siha baada ya wahusika kuitelekeza.
Sehemu ya Bhangi iliyokamatwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha vifaa mbalimbali yakiwemo mapanga na mashoka yaliyokuwa yakitumika katika utekaji wa magari wilayani Mwanga.
Baadhi ya vitu mbalimbali walivyokamtwa navyo watuhumiwa wa ujambazi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha bastola ambayo inadaiwa kutumika katika kufanyia uharifu.
Kamanda wa Polisi akiwaonesha watuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi namna ambavyo wamebuni mbinu mpya ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa za kamanda Mutafungwa.
Baadhi ya askari Polisi pia walikuwepo kuimarisha usalama katika chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro. Picha na Dixon Busagaga, Kilimanjaro.
Friday, April 15, 2016
Magari Kuanza Kuvuka Bure Aprili 16, 2016 Daraja la Kigamboni...!
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI
YA DARAJA LA KIGAMBONI
WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la
kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia
saa 12:00 asubuhi.
Katika
siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali
itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia. Aidha, watembea kwa miguu na waendesha
baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni. Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa
kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.
Magari
yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo
ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo
wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo
la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika
daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela,
Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.
Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito
unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo
muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia
ni:-
1)
Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na
kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu
miundombinu ya daraja
2)
Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’
ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3)
Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo
cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo
hicho.
4)
Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha
uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au
kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5)
Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la
daraja.
Aidha,
Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo
wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini
watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.
Msongamano
wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa
watumiaji wa barabara katika eneo hilo.
Imetolewa
na;
Eng.
Joseph M. Nyamhanga
Katibu
Mkuu (Ujenzi)
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14
Aprili, 2016
Thursday, April 14, 2016
NMB Yasaini Mkataba na MCFKutoa Mikopo kwa Hospitali Binafsi
Subscribe to:
Posts (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akishirikiana na wakulima wa Kijiji cha Itinje Wilaya y...







































