Friday, February 19, 2016

VIJANA WASHAURIWA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI

Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez. Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.[/caption]
Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.
Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.
Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.
“Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,
“Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.
Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.
Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
IMG_3639
Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.
    Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez. Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa. Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana. Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio. Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata. “Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi, “Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.    

TIGO YATOA MILLIONI 10 WAATHIRIKA WA MAFURIKO IRINGA

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana .  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana . [/caption]
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro  kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana .

 
Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .


Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana


Iringa, Februari 17, 2016: Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga
Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na mashuka 35.
Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.
Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.

Tuesday, February 16, 2016

NMB Wadhamini Mkutano wa Maofisa Waandamizi Jeshi la Polisi

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akimkabidhi Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (kulia) msaada wa mabegi yaliyotolewa na NMB leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. vifaa hivyo vinatarajiwa kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam. 

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akimkabidhi Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (kulia) moja ya mabegi ya msaada yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Mabegi hayo yanatarajia kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Utumishi Jeshi la Polisi, DCP, Gabriel Semiono akishuhudia tukio hilo. 




Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akijiandaa kumkabidhi Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (kulia) mabegi yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akimkabidhi Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (kulia) moja ya mabegi ya msaada yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Mabegi hayo yanatarajia kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Utumishi Jeshi la Polisi, DCP, Gabriel Semiono akishuhudia tukio hilo.

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baaadhi ya maofisa waandamizi wa jeshi la polisi na NMB walioshiriki zoezi la makabidhiano ya mabegi ya msaada yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Mabegi hayo yanatarajia kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki (kulia) akimshukuru Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo Benki ya NMB PLC, Abdulmajid Nsekela (kushoto) mara baaadhi ya zoezi la makabidhiano ya mabegi yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Mabegi hayo yanatarajia kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo yakifanyika ndani ya Ofisi ya Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Abdulrahman Kaniki kabla ya zoezi la makabidhiano ya mabegi yaliyotolewa na Banki ya NMB jana Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam. Mabegi hayo yanatarajia kutumika katika Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania utakaofanyika kesho kutwa jijini Dar es Salaam.

BENKI ya NMB imedhamini Mkutano Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania unaotarajia kufanyika kwa Siku mbili jijini Dar es Salaam, yaani Februari 18 na 19, 2016. Benki ya NMB jana ilikabidhi mabegi ambayo yanatarajia kutumika katika Mkutano huo Mkuu wa Makamishna na Maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania.
Benki ya NMB imetoa vifaa hivyo pamoja na kugharamia sehemu ya gharama za mkutano huo ikiwa kama mdau wa Jeshi la Polisi, ambapo pia katika mkutano wa maofisa hao kwa mwaka jana ilitoa takribani kiasi cha shilingi milioni 75 pamoja na msaada wa pikipiki tano ili kulisaidia jeshi katika kutimiza majukumu yake na kudumisha ushirikiano na kampuni hiyo.

Thursday, February 11, 2016

LUHAGA MPINA ATEMBELEA UJENZI WA MTARO UWANJA WA MNAZI MMOJA

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo.  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akizungumza wakati alipofika katika mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja akiwa katika ziara yake kisiwani Zanzibar. na kumalizia Kisiwani Pemba kutembelea Miradi ya Mazingira kisiwani humo. [/caption]
Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
 

YOUNG DEE ATEMBELEA MADUKA YA TIGO NA KUGAWA ZAWADI MBALIMBALI KWA WATEJA NA MASHABIKI ZAKE

Msanii wa kizazi kipya Young Dee akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mmoja wa wateja wa Tigo wa tawi la  Makumbusho mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii .
Msanii wa kizazi kipya Young Dee akifurahi jambo na mmoja wa wateja wa tawi zawadi ya tisheti kwa mmoja wa wateja wa Tigo wa tawi la  Makumbusho mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii. 
Msanii wa kizazi kipya Young Dee akifurahi jambo na mmoja wa wateja wa Tigo tawi la Makumbusho baada ya kumkabidhi  zawadi ya tisheti mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii .



Wafanyakazi wa  Tigo wa tawi la  Makumbusho wakiwa katika picha ya pamoja na msanii wa kizazi kipya Young Dee akiwa  mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii .

Msanii wa kizazi kipya Young Dee akihojiwa na mwandishi Emmanuel Onyango   katika  Tigo wa tawi la  Makumbusho mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii 

Msanii wa kizazi kipya Young Dee akitazama simu zinazouzwa katika duka la  Tigo tawi la Tegeta mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii 

Wafanyakazi wa Tigo tawi la Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja na msanii wa kizazi kipya Young Dee mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii .

Msanii wa kizazi kipya Young Dee akitoa zawadi ya tisheti kwa mmoja wa wateja wa tawi la Manzese   simu zinazouzwa katika duka la  Tigo tawi la Tegeta mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii 

Msanii wa kizazi kipya Young Dee akikabidhi zawadi ya tisheti kwa  mmoja wa wateja wa tawi la Manzese zawadi ya tisheti mapema leo alipofanya ziara ya kutembelea maduka matatu ya Tigo ya Makumbusho ,Tegeta na Manzese  na kugawa zawadi na kupiga picha na mashabiki wake kuelekea sikukuu ya wapendanao mwishoni mwa wiki hii 

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ASHATU KIJAJU AFUNGUA MKUTANO WA WANACHAMA NA WADAU WA PPF

Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF. Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.[/caption]
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaju akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaa
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...