Sunday, August 30, 2015

UZINDUZI CHADEMA


Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa. Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakionyesha furaha yao kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward
Lowassa.[/caption]
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
 Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakiwashangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, Agosti 29, 2015.
Sehemu ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali nchini wakiendelea kuchukua habari za Mkutano huo, uliofanyika jioni ya kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam na kuhudhulia na maelfu ya Wakazi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akimkabidhi, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Juma Duni Haji, Kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kwa mwaka 2015/2020 mara baada ya kuizindua, Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, Mgombea mwenza, Juma Duni Haji pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad wakionyesha vitabu cha Ilani ya Uchaguzi mara baada ya kuzinduliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Viongozi wa Vyama mbali mbali vinavyounda UKAWA wakionyesha Ilani hiyo mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam, Agosti 29, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kulia) akiwatambulisha baadhi ya Wagombea Ubunge katika Majimbo mbali mbali ya jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia akizungumza kwenye Mkutano huo.
Watu wa Msalaba Mwekundu wakiwa wamembeba mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar aliepoteza fahamu kwa kukosa hewa kutokana na uwingi wa watu uliofurika kwenye viwanja vya Jangwani, Jijini Dar es salaam Agosti 29, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye akitoa salamu zake kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam Agosti 29, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa akiteta jambo na Mgombea Mwenza wake, Juma Duni Haji, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika  Agosti 29, 2015. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Lowassa akihutubia katika Mkutano huo wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, uliofanyika Agosti 29, 2015.
Mmoja wa wanasiasa wakongwe waliotoka CCM, Tambwe Hiza akisalimia.
 PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

MSD Yazindua Rasmi Taarifa ya Mwaka 2013/2014

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani
   
 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Tehama  wa MSD, Issaya Mzolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Meneja wa Uhasibu wa MSD, Sako Mwakalobo.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto), akikata keki hiyo aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wakati wakimpongeza kutimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwake. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi wa MSD, Doreen Josia. Wafanyakazi hao waliamua kumpongeza Mwaifwani baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mwaifwani akimlisha keki, Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry.
Hapa ni zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia akilishwa keki.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry, akimlisha keki, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Hapa Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi MSD, Dinah Dileya (kushoto), akilshwa keki.
 
Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akigawa ripoti hiyo kwa wafanyakazi wa MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo na hafla ya wafanyakazi hao kumpongeza Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani kutimiza miaka 55 tangu azaliwe.
Viongozi wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hii ni timu ya wajumbe walioandaa ripoti hiyo ya mwaka 2013/2014. 'Big Up wajumbe kwa kazi nzuri'
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. 

Friday, August 28, 2015

ORODHA YA MAJINA YA WALIOMBA KUJINGA NA JESHI LA POLISI YATOKA



JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAJULISHA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KUWA WANATAKIWA KURIPOTI KWA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA TAREHE 28/08/2015 KWA AJILI YA MAANDALIZI YA USAFIRI WA KWENDA SHULE YA POLISI TANZANIA
TAREHE 29/08/2015.

KILA MMOJA ATATAKIWA KUWA NA NAULI YA KUMWEZESHA KUSAFIRI TOKA MAKAO MAKUU YA MKOA ANAKOANZIA KUSAFIRI HADI SHULE YA POLISI MOSHI NA ATAREJESHEWA NAULI ATAKAPOFIKA CHUONI BAADA YA KUWASILISHA TIKETI YA SAFARI. AIDHA TAREHE YA MWISHO YA KURIPOTI CHUONI NI TAREHE 05/09/2015 NA ATAKAYERIPOTI BAADA YA HAPO HATAPOKELEWA.

AIDHA VIJANA HAO WATALAZIMIKA KUFIKA SHULENI WAKIWA NA VITU VIFUATAVYO :
1.VYETI VYAO VYOTE VYA MASOMO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATES/RESULT SLIP PAMOJA NA LEAVING CERTIFICATES) KIDATO CHA NNE, SITA NA VYUO.
2.VYETI HALISI VYA KUZALIWA (ORIGINAL BIRTH CERTIFICATES). HATI YA KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIKA.
3. MASHUKA MAWILI RANGI YA BLUU BAHARI (LIGHT BLUE)
4.CHANDARUA CHENYE UPANA FUTI TATU
5.NGUO ZA MICHEZO (TRACK SUIT NYEUSI,T-SHIRT BLUE NA RABA)
6.PASI YA MKAA.
7.NDOO MOJA.
8.PESA ZA KULIPIA BIMA YA AFYA KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA MIA NNE TU (50,400/=).
9.PESA KIDOGO YA KUJIKIMU.

ZINGATIA: KWA MUJIBU WA KANUNI ZA SHULE YA POLISI NI MARUFUKU KUFIKA SHULENI NA SIMU YA MKONONI. ATAKAYEPATIKANA NA SIMU ATAFUKUZWA SHULENI HAPO. SHULE ITAELEKEZA NA KUSAIDIA KUFANYA MAWASILIANO.
MAJINA YA WAHITIMU YANAPATIKANA KUPITIA TOVUTI www.policeforce.go.tz au WAFIKE OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Thursday, August 27, 2015

Sanaa Fashion Show

Tamasha  
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show, linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa THT, Msami.
Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.
"Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.
Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia 'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa jina la Sanaa.".
Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.
Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.
Abdul AmadHusna Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!
Jonetha Peter
Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael..
Barnabas Lukindo
Barnabas Lukindo akifanyiwa make up..
Calisah Abdulhameed
Calisah Abdulhameed akifanyiwa make up
Husna Tandika wa Shearshen na Natasha Mohammed
Husna Tandika akimpaka Natasha Mohammed model make up
Calorine Benard
Calorine-Benard. akifanyiwa make up
Calorine Benard.jpge3
DSC_0024
DSC_0025

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...