Monday, August 24, 2015

TANAPA Yatangaza Kampeni Kuhamasisha Utalii wa Ndani

span style="font-size: large;">
Kaimu Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketansi akizungumza na wanahabari(hawako pichani) juu ya Kampeni ya uhamasishaji wa utalii wa ndani kwa wazawa itakayodumu kwa muda wa miezi sita.

Baadhi ya Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wanahabari (hawako pichani ) juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miezi sita watakao tembelea zaidi ya Hifadhi nne watapata ofa ya kutembelea Serengeti ikiwa ni pamoja na kugharamiwa maradhi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano.
Kaimu Meneja Mauzo wa TANAPA,Victor Ketansi akisisitiza jambo.

Mkuu wa Idara ya Utali katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akizungumza vivutio mbalimbali vunavyopatikana katika hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni afisa utalii mfawidhi na mkuu wa kanda ya utalii Kaskazini,Lauriano Munishi akizungumza jambo mbele ya wanahabari(hawako pichani)juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha utali wa ndani.
Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha,(ANAPA) Neema Philip akizungumzia vivutio mbalimbali vinayopatikana katika hifadhi ya Arusha.
Afisa Utalii Mwandamizi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ,Pellagy Marandu akizungumzia vivutio mbalimbali vinavyoopatikana katika hifadhi hiyo.
Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Catherine Mbena akiwa na mwandishi wa habari wa TBC Kilimanjaro,Sauda Shimbo wakati wa kikao cha maofisa wa TANAPA na wanahabari kuzungumzia juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini..

PSPF Wadhamini Ligi ya Bodaboda Kipunguni "B"

 div style="text-align: center;">

 
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na madereva bodaboda wa Kipunguni 'B' kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga
  Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akizungumza na wananchi mbalimbali waliofanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wakiume maeneo ya Kipunguni 'B' katika manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma  akitoa maelezo ya kina kuhusu faida na huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF), akiongea na madereva wa bodaboda wa Kipungunu 'B' wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva hao.
  Delphin Richard Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,  akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Madereva wa Bodaboda wa Kipunguni 'B' ambapo mfuko wa PSPF imedhamini mashindano hayo. Katikati ni Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa.

 
 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa akitambulishwa wachezaji
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy akisalimiana na wachezaji katika ufunguzi wa ligi ya madereva bodaboda.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza mmoja wa wazee kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari, ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga na kunufaika na huduma mbalimbali zilizo katika hifadhi ya jamii ya (PSPF)
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma akimjazia fomu ya Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wilaya ya Ilala jijini Dar mara baaada ya kupata elimu na kuridhia na huduma za mfuko huo.

 Madereva bodaboda wawana mwitikio mkubwa wa kujiunga na mfuko wa PSPF kupitia (PSS) kwakujaza fomu za Uchangiaji wa Hiari
 Afisa wa mfuko wa pensheni, Delphin Richard(kushoto) akimuonesha sehemu ya kuweka alama ya dole gumba mmoja wa madereva wakati wa ujazaji  fomu za Uchangiaji wa Hiari
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliachi Remmy(kulia) akiwajazia fomu za Uchangiaji wa Hiari mmoja wa madereva wa Bodaboda wa Kipunguni B wakati wa mashindano ya mpira wa miguu katika eneo la Kipunguni B 

Madereva bodaboda wa mtaa wa Kipunguni 'B' kata ya Kivule manispaa ya Ilala wameanzisha ligi  ya mpira wa miguu kwaajiri ya kuendeleza kujenga afya zao kwa michezo kwani michezo ni afya kwa wote, wakati wa ufunguzi huo wa ligi hiyo ya madereva bodaboda wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Mfuko wa pensheni wa (PSPF)nao hawakuwa mbali kwaajiri ya kuwawezesha madereva hao kwa kipindi chote cha ligi hiyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi hiyo mgeni rasmi ambaye ni mkaguzi msaidizi wa polisi kanda maalumu ya dare s salaam Josephat Sylvery Tirumanywa amewaasa madereva hao kuwa waweze kucheza kwa amani michezo yote na pia waweze kuwa ni miongoni mwa watu watakao jiunga na na mfuko wa (PSPF) ka kupitia (PSS) kwaajiri ya kuendelea kupata huduma zilizo bora na  zenye uhakika .

Pia Afisa masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Ismail Juma amesema wameamua kuungana na madeeva boda boda hao ili kuweza kuwapa elimu katika suala la kuwekeza na kufaidika na mafao mbalimbali yanayo tolewa na PSPF kwani Pindi watakapo jiunga na mfuko huo wataona matunda mengi hasa kutokana na kuwa ni watu ambao wanategemewa na familia zao hivyo kama Pspf wana mafao ambayo wataweza kujikwamua kama mafao ambayo wanaweza kuwasomesha watoto,vilevile fao la uzazi hata fau la nyumba pia ujiungapo na mfuko huu utafaidika na wala hauto jutia 

Naye Bw.Delphin Richard ambaye pia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) amewasisitiza madereva kutii sheria za barabarani na pia kuweza kucheza ligi hiyo kwa amani maana wamepewa dhamana ya kuwasafirisha abiria kwa amani na upendo ,hivyo kati ya jeshi la polisi na madereva husaidiana kufanya kazi kwa umoja na hivyo kuweka mahusiano mazuri katika kufanikisha nchi yetu inajengwa na sisi watanzania kwa kuendeleza upendo na amani pindi tuwapo barabarani,aliongeza kwa kuwapa shukrani madereva ya kuweza kuchagua mfuko wa pensheni wa Pspf kuwa wadhamini wa michuano hiyo kwani PSPF ipo kwaajiri ya kila mmoja  na kuweza kuwaasa  waweze kuwahamasisha watu mbalimbali kuweza kujiunga na mfuko huo ili kuhakikisha mabadiliko ya wananchi mbalimbali yanatokea kimaisha ,elimu,afya na mengine mengi.

Mfuko wa pensheni wa PSPF unafuraha ya kuwa kwa sasa wananchi wanajua kile kilicho sahihi nakuongeza kuwa wananchi mbalimbali waweze kufika maeneo ya kipunguni B ilikuweza kushirikiana na madereva hao kwa kuwashangilia wakati ligi ikiwa inaendelea na ligi hiyo itakayo dumu kwa takibani wiki moja.

PSPF Yakabidhi Magodoro 118 UDSM


 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David Mfinanga, (Watatu kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (watatu kulia), wakati akipokea msaada wa magodoro 118 yaliyotolea wan Mfuko huo kwenye hafla fupi iliyofanyika chuon I hapo, Agosti 24, 2015. Magodoro hayo ni kwa ajili ya wanafunzi walioathiriwa na mogto uliozuka kwenye bweni kitalu B kule hosteli za Mabibo, Aprili mwaka huu 2015.

NA K-VIS MEDIA
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, leo Agosti 24, 2015, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa wanachuo walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli ya chuo hicho Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.
Akikabidhi msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala), Profesa David A. Mfinanga, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na ajali hiyo ya moto ambayo iliyotokea  kwenye bweni kitalu namba B na kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.
“Kwa kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni wanachama watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili wanafunzi waweze kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.
Akitoa shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF, kwa msaada huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo yatapelekwa kwa walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu waliyoyapata kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.
Kwa mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jingo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo 788, wakati linawaka moto.

 Profesa mfinanga (wapili kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya chuo mbele ya maafisa wa PSPF,  viongozi wa wanachuo na wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa hafla hiyo
 Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, baada ya kukabidhi msaada huo, Agosti 24, 2015
 Paulina Mabuga, mfanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaa, (wapili kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo. Wakwanza kushoto ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Denis Bashulula
 Profesa Mfinanga na Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya wanafunzi UDSM
Mfanyakazi wa UDSM, akipita jirani na magodoro hayo


Tuesday, August 18, 2015

Maafali ya Darasa la Saba Shule ya St.Marrys Forest ya Jijini Mbeya

Wanafunzi wa shule ya Kimataifa ya St.Marrys Forest jijini Mbeya wakitoa burudani katika mahafali ya Darasa la saba katika shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
 
 
 
 
Wahitimu wa Elimu ya Msingi katika shule ya Kimataifa ya St.Marrys Forest Jijini Mbeya
 
 
 
 
Wazazi na walezi
 
 
Uongozi wa shule ukitoa zawadi kwa wanafunzi walifanya vizuri katika masomo yao kwa upande wa wanafunzi wote kwa ujumla waliobaki shuleni hapo.
 
 
Wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao wakipatiwa zawadi nauongozi wa shule hiyo.
 
 
 
 
 
Baadhi ya wazazi wakitoa pongezi zao kwa watoto wao ambao wamehitimu elimu ya msingi darasa la saba katika shule hiyo ya kimataifa ya St.Marys Forest jijini Mbeya
 
 
 
 
 
 

Salam na pongezi kwa wazazi. Picha zote kwa hisani ya Jamiimoja Blog.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...