Saturday, December 1, 2012

Harusi ya Richard Mllatie Assey na Bi. Jackline Hamson Ghika


Bwana Harusi Richard Mllatie Assey akimvisha pete mkewe Bibi. Jacline Hamson Ghikas wakati wa ndoa takatifu illiyofungwa leo jijini Dar es Salaam katika kanisa la St. Peters.
Maharusi wakipigana busu bashasha baada ya kuvishana pete.
Bwana Harusi Richard Mllatie Assey akiangusha saini katika gamba la kuhalalisha ndoa takatifu.
Bibi Harusi Jackline Richard Mllatie Assey naye akitia saini.
Maharusi wakionyesha vyeti vya ndoa.
Wapambe wa maharusi wakati wa ibada ya ndoa takatifu,
Wazazi wa Maharusi Mr & Mrs Assey na Mama mzazi wa Bwana harusi wakionyesha furaha baada ya watoto wao kufunga ndoa.
Pichani juu na chini baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika kushuhudia ndoa takatifu ya Bwana na Bibi Richard Mllatie Assey.
Bwana na Bibi Harusi Richard Mllatie Assey na Jackline Hamson Ghikas wakitoka kaniasani baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la St. Peters Oysterbay jijini Dar.
Wakionyesha nyuso za Furaha baada ya kuhalalisha ndoa yao.
Bwana Harusi Richard Mlatie Assey na mpambe wake wakishine na Suti matata zilizobuniwa na Sheria Ngowi.
Wapambe wa maharusi katika pozi.
Wapambe wakiume ndani ya suti zilizobuniwa na Sheria Ngowi.

Send Off ya Bi. Dorice Aloyce Tendewa

Send off ya Bi. Dorice Aloyce Tendewa Iliyofanyika katikqa Ukumbi wa New Msasani Beach Na ndoa inatarajiwa kufanyika Desemba 1,2012 KKKT Usharika wa Azania Front DSM Rangi ya Send Off: Orannge na White
 Biharusi mtarajiwa Bi. Dorice Aloyce Tendewa akiwa katika pozi meza kuu wakati wa tafrija maalum ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika maisha yake mapya ya ndoa ambayo anataraji kuifunga Jumamosi ya Desemba 1, 2012 katika Kanis la KKKT Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo iliyofana sana ilifanyika katika ukumbi wa New Msasani Beach Club. 
 Bi. Dorice Tendewa, Biharusi mtarajiwa (kushoto) akiwa na msimamizi wake na rafiki yake mkubwa, Betha Mwakapenda wakati wa tafrija yao maalum ya kumuaga.
 
 
 Bi.Dorice Tendewa akisaidiana na Msimamizi wake, Bi. Betha Mwakapenda kukata keki. 
  Bi Harusi Mtarajiwa Dorice Tendewa akitambulisha wageni mbalimbali ndugu zake kwa wageni waliofika katika tafrija yake.
Picha ya pamoja ya familia ya Bwana na Bibi Aloyce Tendewa. Picha kwa hisani ya FathervKidevu Blogu

Tuesday, November 13, 2012

Harusi ya Godfrey Monyo na Bi. Gadiosa Lamte

Harusi ya Godfrey Monyo na Bi. Gadiosa Lamte
Ilifanyika Jumamosi ya Novemba 10, 2012.
Ukumbi wa Mnazi Mmoja DSM

Rangi za Harusi: Nyeupe, Nyekundu na Nyeusi


Bwana harusi, Godfrey Monyo akiwa na Bi. harusi, Gadiosa Lamte katika Kanisa la Mt. Petro Dar es Salaam. Monyo ni mtangazaji wa kituo cha ITV jijini Dar es Salaam.

Godfrey Monyo akila kiapo cha ndoa dhidi ya mkewe Bi. Gadiosa Lamte wakiwa kanisani

 Bi. Harusi akimvisha mumewe pete kwa ishara ya upendo

 Ni raha kupendana....! Cheki hapa katika moja ya mapozi ya maharusi

 Pongezi toka kwa ndugu jamaa na marafiki..!

Picha ya pamoja ya maharusi na wapambe wao. Harusi na Matukio inawatakia kila heri katika ndoa yenu.

Thursday, October 25, 2012

Women in Balance Kitchen Party Gala

Women in Balance Kitchen Party Gala ilivyowafungua macho wakinamama na mabinti Dar, hata hivyo wakinamama na mabinti walioko mikoani  mamedai kuwa vitu hivyo vizuri hupatikana tu Dar es salaam na kumlalamikia Mratibu wa Shughuli hiyo na kumtaka kwa mwaka ujao kuipeleka mkoani mbeya, au hata ikiwezekana Mwanza ili iwe ikifanyika kikanda kuliko kufanyika sehemu moja na kuwafanya wao kukosa mambo mengi ya msingi yanayopatikana katika function hiyo ya aina yake.




Msemaji katika Hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Chris Mauki akitoa somo la Saikolojia kwa wakinamama na wasichana waliohudhuria hafla hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall jijini Dar.

Life Style Designer of Sex and Relationships kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai akitoa somo la kuhusiana na masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa wenye ndoa na wasiokuwa na ndoa ambapo amesema vipo vitu vingi vinavyochangia kuboresha ama kuharibu mahusiano hayo ambapo wahusika wanatakiwa kuvifahamu na kuvitilia mkazo ili kudumisha mahusiano yao.



Msemaji wa mwisho alikuwa ni Mama Veronica aliyewaacha hoi kwa vicheko wanawake waliohudhuria Kitchen Party Gala ambapo alizungumzia masuala ya uvumilivu katika ndoa sio tu kukosekana kwa kipato ndani ya nyumba bali hata mikimiki ya Unyumba kwa wanandoa.
Independent Sales Consultant wa bidhaa za Oriflame Bi. Jesca Mwakyulu akionyesha bidhaa ya Feminele Intimate Wash ya Oriflame ambayo ameisifia kuwa na Natural Lactic Acid ambayo inasaidia kutunza hali halisi ya sehemu za siri za Mwanamke.
Amefafanua kuwa kwa asili sehemu hizo zina hiyo Lactic Acid ambayo hutunza unyevu sahihi na Bacteria wazuri ambao husaidi kutoa ulinzi dhidi ya Fangasi, miwasho na harufu mbaya.
Mmoja wa wadhamini wa Women in Balance Kitchen Part Gala Mwakilishi kutoka TSN Super Market Lizbeth akitangaza zawadi kumi kwa wageni waliohudhuria Kitchen Party Gala zikiwemo Vocha za kufanya Shopping katika Super Market za TSN zilizopo jijini Dar es Salaam.

 Aunty Sadaka na Mwanasaikolojia Chriss Mauki.


Wakinadada wakionekana kufurahishwa na mambo yaliyokuwa yakizungumziwa kwenye Kitchen Party Gala hiyo.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (kushoto) na mdogo wake.
Mbunifu nguli wa mavazi nchini Khadija Mwanamboka (kulia) a.k.a Kubwa la maadui alikwa miongoni mwa waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Women in Balance Kitchen Party Gala ilikusanya wakina mama na kina dada kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya nje kama inavyoonekana picha na hii kudhihirisha jinsi gani wakimama wanavyopenda kupata Elimu ya kudumisha ndoa zao na familia kwa ujumla.
Palikuwa hapatoshi hakuna hata pakuhemea.
What a beautiful smile.
Salma Msangi wa Channel Ten na Magic Radio.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios akiteta jambo na Mama Veronica.
 Vicheko, nderemo na vifijo vilitawala.

Skylight Band walikuwepo kutumbuiza Hafla hiyo. Uzao wa Bongo Star Search Mary Lukas akitoa burudani.
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali kukonga nyoyo za kinamama waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Blogger Shamim Mwasha (kushoto) a.k.a Zeze wa 8020 Fashions katika pozi na Mshehereshaji wa Women in Balance Kitchen Party Gala Gea Habib.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios (kushoto) na Mgeni wake kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai.(Picha zote na Zainul Mzige).

Harusi ya Mr. Martina Nkurlu na Rachel Sindbard

Harusi ya Mr. Martina Nkurlu na Rachel Sindbard 
Rangi: Paple, Nyeusi na Njano.

 Bwana Harusi Martina Nkurlu na Bi. Rachel Sindbard 
Wakiingia Kanisani kutimiza ahadi ya ndoa.

 Bwana Harusi Mr. Martina Nkurlu akiweka saini kwenye Shahada ya ndoa pembeni ni biharusi

Bwana  na Bibi Harusi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kiapo cha ndoa


 Furaha ilioje kwa Mr.Martina Nkurlu na Bi. Rachel Sindbard




SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...