Sunday, September 16, 2012

Harusi ya Mr Pascal na Florence Ernest

Harusi: Mr. Pascal na Florence
Kanisa: Moyo safi wa Bikira Maria Bagamoyo
Rangi: Orange na Chocolate
Sherehe: Ukumbi Kiramuu Mbezi Beach-Dar es Salaam
Tarehe: 14,September,2012.

Maharusi Bw. Pascal na Bi Florence wakiwasili ukumbini wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Moyo wa Bikira Maria, Bagamoyo mkoani Pwani na kufuatiwa na tafrija iliyofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu,Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.


 Maharusi Bw. Pascal na Bi Florence wakiwa pamoja na wasimamizi wao tayari kwa kupata mvinyo wa makaribisho.

 Bi harusi Florence akifurahia mvinyo ulioandaliwa kwa ajili yao katika ukumbi wa Kiramuu Septemba 14, 2012.

 Mtaarishaji maalumu wa ndafu akikatakata kwa ajili ya maharusi.

 Wazazi wa Bwana Harusi wakimlisha Bi. Harusi kipande cha ndafu ikiwa ni ishara ya kumkaribisha katika familia yao.

 Mjomba wa Bw. Harusi, Lenny Kisarika (katikati) kulia ni mkewe na kushoto ni dada wa mjomba huyo.


Muandaaji Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio akisalimiana na mjomba wa Bw. Harusi, Mr. Kisarika na mkewe.


 Muandaaji Mkuu wa Blogu ya Harusi na Matukio akifurahia jambo na mjomba wa Bw. Harusi Mr. Kisarika na mkewe.

 Kaka wa Bi. Harusi (katikati) akiwa pamoja na familia yake na wanandugu wakipata kilaji.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio kwa makini!

 Muandaaji Mkuu wa Blogu ya Harusi na Matukio akifurahia jambo na Bi. Harusi Florence Ernest.

 Bi. Harusi akiselebuka pamoja na wageni waalikwa.


Wageni waalikwa wakeselebuka kwa mitindo mbalimbali ukumbini hapo.


Flowers wameremetile

Saturday, September 15, 2012

Harusi ya Mr Joachim Mushi na Hilder Mwaipopo

Ndoa kati ya :Mr Joachim Mushi na Hilder Mwaipopo
Ilifungwa  Kanisa : Kristu Mfalme Tabata
Rangi ya Harusi: Gold, Off white na Black
Ukumbi: King Palace Makuti hall Sinza
Tarehe: 25/08/2012.


 Kanisa la Kristu Mfalme Tabata ambalo ndilo maharusi hawa walifunga ndoa tarehe 25/08/2012 saa kumi alasili




Bwana harusi Bw. Joachim Mushi (Kulia) na Bi Hilder Kushoto wakiwa katika nadhili ya milele




 Pichani Maharusi wakivishana pete  ikiwa ni ishara ya uaminifu mpaka kifo kitakapo watenganisha.

 Maharusi Bw.Joachim Mushi na Bi. Hilder Mwaipopo wakiwa na nyuso za furaha na wakionesha shahada za ndoa







 Maharusi wakiwa katika Pose mbalimbali baada ya Kufunga ndoa katika kanisa la Kristu Mfalme Tabata Jijini Dar es salam



Maharusi wakiwa na wasimamizi wao  wa kwanza kulia ni Bw. Gide Magila na wa kwanza  kushoto ni Bi Adelgundis Magila.


 Maharusi wakiwa na nyuso za furaha wakiingia  ukumbini King Palace Makuti Hall Sinza


 Maharusi wakiwa na mvinyo na kushiriki na wageni waalikwa usiku wa tarehe 25/08/2012


 Maharusi wakifuatilia matukio katika hafla yakuwapngeza

 Flowers wakifurahia

Send off ya Bi Hilder Mwaipopo

Send off ya : Hilder Mwaipopo
Ilifanyika: Ukumbi wa Anglikana Iringa
Rangi ya Send off : Paple na Silva
Tarehe: 18/08/2012

Bi harusi mtarajiwa Hilder.


 Bi harusi  mtajajiwa (kushoto) akiwa na mpambe wake Bi Nuru.
 
 

 Pichani juu ni Bi harusi  mtajajiwa Hilder (kushoto) akiwa na mpambe wake Bi Nuru baada ya kuwasili ukumbini.




Bi harusi mtarajiwa Hilider wa pili kushoto akijiaandaa kufungua mvinyo.

Bi harusi  mtajajiwa (kushoto) akiwa na mpambe wake Bi Nuru wakinywa kwa furaha mvinyo ulioandaliwa kwa ajili yao.



 Bi harusi  mtajajiwa (kushoto) akiwa na Bwana harusi mtarajiwa Bw. Joachim Mushi baada ya kumtambulisha.

Hatimaye ukawadia wakati wa msosi uliandaliwa kwa mtindo wa kinyakyusa zaidi.



Harusi ya Mr Magila na Adelgundes



 Pichani juu ni maharusi Gide Magila na mkewe Bi. Adelgundis wakigonganisha glasi za mvinyo kabla ya kunyweshana katika harusi yaoiliyofanyika jijini Dar es Salaam Julai 27, 2012 kwenye Ukumbi wa Flamingo Mbezi Makonde.

 Maharusi Gide Magila na mkewe Bi. Adelgundis (katikati) wakiwa na glasi za mvinyo pamoja na wasimamizi wao.

 

 Wageni waalikwa katika harusi ya Bw. Gide Magila na mkewe Bi. Adelgundis wakicheza miondoko ya kwaito.


 Bi. Adelgundis (kulia) na mpambe wake wakicheza miondoko ya kwaito pamoja na wageni waalikwa.


Mama mzazi wa Bwana harusi (mwenye suti) akiwa pamoja na marafiki.  

 Mama mzazi wa Bwana harusi (mwenye suti) akiwa pamoja na wanandugu. 


 Flowers wakipokea zawadi za maharusi.

Dada wa Bwana harusi (Kulia) akiwa na mmoja wa marafiki.

Thursday, July 5, 2012

Harusi ya Oltesh Eliguard na Ssanyu Sylvia jiji Dar

 
 Maharusi, Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi wakiaga watu mbalimbali waliofika ndani ya Kanisa la Azania Front, mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu, katika kanisa hilo la jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu, Dk. Alex Malasusa akizibariki pete za ndoa za maharusi kabla ya maharusi hao kuvishana.



Maharusi wakilishana kiapo cha ndoa mbele ya umati mkubwa (haupo pichani) uliofika kanisani hapo mapema leo mchana kuishuhudia ndoa hiyo ya Oltesh Eliguard Metili na Ssanyu Sylvia Nyinondi, iliyofanyika ndani ya kanisa la Azania Front.
 
 Maharusi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa na kuwa mwili mmoja mapema leo ndani ya Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Pichani kushoto ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakishuhudia pia tukio hilo adhimu na la kihistoria kwa Wanandoa.

Siku Angaza Mwipopo alipoungana maisha na Chivanenda

 Hapa Jaji Mkwawa Akimkabidhi mkuki Bwana Harusi Angaza Mwipopo ikiwa ishara ya kujilinda pamoja na mkewe Chivanenda Luwongo


 Bwana Harusi Angaza Mwipopo na Mkewe Chivanenda Luwongo wakiwa na wasimamizi wao siku ya harusi yao.


Katibu mkuu kiongozi mstaafu Phillemon Luhanjo akiteta jambo na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora katika serikali ya awamu ya tatu, Wilson Masilingi pamoja na waheshimiwa majaji

Tuesday, May 15, 2012

Harusi ya Christopher na Jannifer


 Christopher na Jennifer wakiwa katika pozi la picha mara baada ya kufunga pingu za maisha.


 Bwana Harusi Christopher (kulia) akimvisha pete mkewe Jannifer katika ibada ya ndoa yao iliyofanyika Jumamosi ya Februari 18 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.


 Wapambe wa maharusi wakiwa katika picha pambo ya maharusi mara baada ya ibada ya ndoa yao.


 Christopher na Jennifer katikati wakiwa na mama mzazi wa Jannifer (kulia) pamoja na mjomba Sumi kushoto.


Bwana Harusi Christopher akiwa na mkewe Jannifer. Picha zote kwa Hisani ya Fullshangwe Blogu.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...