Thursday, July 5, 2012

Siku Angaza Mwipopo alipoungana maisha na Chivanenda

 Hapa Jaji Mkwawa Akimkabidhi mkuki Bwana Harusi Angaza Mwipopo ikiwa ishara ya kujilinda pamoja na mkewe Chivanenda Luwongo


 Bwana Harusi Angaza Mwipopo na Mkewe Chivanenda Luwongo wakiwa na wasimamizi wao siku ya harusi yao.


Katibu mkuu kiongozi mstaafu Phillemon Luhanjo akiteta jambo na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora katika serikali ya awamu ya tatu, Wilson Masilingi pamoja na waheshimiwa majaji

Tuesday, May 15, 2012

Harusi ya Christopher na Jannifer


 Christopher na Jennifer wakiwa katika pozi la picha mara baada ya kufunga pingu za maisha.


 Bwana Harusi Christopher (kulia) akimvisha pete mkewe Jannifer katika ibada ya ndoa yao iliyofanyika Jumamosi ya Februari 18 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.


 Wapambe wa maharusi wakiwa katika picha pambo ya maharusi mara baada ya ibada ya ndoa yao.


 Christopher na Jennifer katikati wakiwa na mama mzazi wa Jannifer (kulia) pamoja na mjomba Sumi kushoto.


Bwana Harusi Christopher akiwa na mkewe Jannifer. Picha zote kwa Hisani ya Fullshangwe Blogu.

Friday, March 16, 2012

Harusi ya Godluck na Neema


Neema akimvisha pete mumewe Godluck kanisani


Godluck na mkewe Neema wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wasimamizi wao baada ya kutoka kanisani.


Maharusi Godluck na Neema wakiingia ukumbini tayari kwa hafla ya harusi yao. 


Wapambe wa maharusi wakiwa katika pozi. (Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog)

Tuesday, February 21, 2012

Harusi ya Fredy na Ephracia jijini Dar es Salaam

Januari 21, 2012 itabaki kuwa siku kubwa ya kumbukumbu kwa maharusi Fredy pamoja na mkewe Ephracia baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la Mwenge jijini Dar es Salaam, na kufuatia na tafrija kubwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Mbezi Garden Hotel - Dar es salaam.

Maharusi Fredy (kulia) pamoja na mkewe Ephracia (kushoto) wakipozi na watoto wazuri waliosimamia harusi yao.


Mvinyo rasmi wa sherehe hiyo tulifungua wenyewe!


Fredy pamoja na mkewe Ephracia


Kwa ishara ya upendo tuliwatembelea na kuwapa zawadi watoto yatima kusherehekea pamoja (Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog)

Wednesday, February 1, 2012

Harusi ya Samwel Daniel na mkewe Kaindi Taratibu



Wakiwa na nyuso za furaha pichani ni Bwana harusi Samwel Daniel na mkewe Kaindi Taratibu wakiwa kwenye pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofanyika katika Ukumbi wa Mbezi Luxury jijini Dar es Salaam.


“Hawa si wawili tena bali ni mwili mmoja,”; Bwana harusi Samwel akiwa na mkewa Kaindi wakishuka kutoka katika Mlima Kilimanjaro uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kutalii wa baada ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28, 2012.

Makaka wa maharusi wakiwa katika picha ya pamoja wakisherehekea harusi ya mdogo wao. Picha kwa hisani ya wanafamilia.

Saturday, January 14, 2012

Harusi ya Amani Adam na Felister Kiungulia


Bi. Felister Kiungulia (kulia) akiwa na mumewe Amani Adam kwenye hafla ya utambulisho wa mumewe katika ukoo na familia ya Mzee Kiungulila Lushoto mkoani Tanga. Ndoa ya maharusi hawa ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mkoani Arusha.


Bi. Felister Kiungulia akiwa na mumewe Amani Adam

Bi. Felister

Bw. Adam


Kutoka kushoto ni Mzee Kiungilia akiwa na mkewe kwenye hafla ya kutambulishwa mkwe wao Amani Adam iliyofanyika nyumbani kwa Kiungulia Soni Lushoto Desemba 31, 2011.


Ndugu jamaa, majirani na marafiki wa Mzee Kiungulia wakitambulishwa kwa mumewe Felister katika hafla hiyo, wa pili kulia ni kaka mkubwa wa Felister Henry Kiungulia, wa kwanza kulia kwake ni mkewe Grace Mushi Kiungulia.  Picha kwa hisani ya wanafamilia.

Harusi ya Bw. Joseph na Bi. Sylvia



Joseph akiwa na Mkewe Sylvia baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la St. Joseph Jumamosi ya Novemba 26, 2011 jijini Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na hafla kabambe iliyofanyika katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Maharusi Joseph na Sylvia wakigongesha glasi zenye mvinyo kwa ishara ya upendo kabla ya kunyweshana katika hafla yao iliyofanyika katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Joseph akiwa na Mkewe Sylvia wakipiga picha za kumbukumbu ya tukio lao na ndugu jamaa na marafiki katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Joseph na Mkewe Sylvia wakiwapungia mkono wageni waalikwa katika hafla yao huku wakiondoka katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo' baada ya hafla yao. Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...