Friday, April 8, 2011

Maandalizi ya Fiesta, mapambano ya mashabiki wa timu nane kubwa za Ulaya

Serengeti Fiesta Soccer Bonanza katika picha


Brass Bend ya Polisi Dar es Salaam ikiongoza maandamano ya mashabiki mbalimbali wa timu nane kubwa Ulaya yakielekea kwenye viwanja vya Leaders Dar es Salaam Aprili 8, 2011.



Mashabiki wa Manchester United wa Dar es Salaam wakishangilia moja ya ushindi wa awali walioupata katika viwanja vya Leaders, kwenye Bonanza la Soccer (Serengeti Fiesta Soccer Bonanza)



Mashabiki wa timu mbalimbali katika bonanza hilo wakiangalia mipambano anuai, hapa wamezunguka moja ya viwanja vilivyotumika kwenye mpambano huo.



Baadhi ya mashabiki wa Real Madriad wakishangilia timu yao katika viwanja hivyo.



Baadhi ya mashabiki wa Barcelona wakiwa wamekula pozi na na shabiki wa Chelsea (wa pili kushoto).








Vikao vya bunge vyaendelea Dodoma


Spika wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Clement Mshana baada ya kuzungumza na maofisa habari, Elimu na Mawasiliano wa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Mikoa na wakala mjini Dodoma.

Thursday, April 7, 2011

Ujenzi daraja la Kigamboni kuanza


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemo (kulia) katika eneo la Kurasini Vijibweni Dar es Salaam,  kuhusu ujenzi wa Daraja la Kigamboni eneo hilo. NSSF  inatarajia kuanza ujenzi wa Daraja hilo mapema mwaka huu baada ya zabuni kutangazwa na kumpata mhandisi. Daraja hilo litagharimu zaidi ya bilioni 130 hadi kukamilika kwake. (PICHA NA MDAU TIGANYA VICENT WA MAELEZO)

Tuesday, April 5, 2011

Mchungaji Mwasapile afanya maajabu kwa kibaka


Mchungaji Mwasapile


Na Mwandishi Wetu,
Loliondo


MIUJIZA ya Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro juzi Ilijidhihirisha kijijini hapa baada ya mmoja wa wezi aliyechomoa pochi ya mgonjwa raia wa Kenya kusalimisha pochi hiyo kwa Mchungaji huku akidai anapigwa na watu asiowaona na kushindwa kuona.

Aprili 2, 2011 mmoja wa raia kutoka nchini Kenya aliibiwa pochi iliyokuwa na fedha za Kenya sh. 20,000, simu, hati ya kusafiria na vitambulisho mbalimbali hali iliyomlazimu kutoa taarifa ya wizi huo kwa Mchungaji Mwasapile akiomba msaada.

Baada ya kutoa taarifa hiyo Aprili 3, majira ya saa saba mchana mchungaji Mwasapila alitangaza kwa watu waliokusanyika kijijini hapo na kutaka aliyeiba arejeshe vitu hivyo  na kwamba  asipofanya hivyo fimbo ya Mungu itamuadhibu.

“Ndugu zangu wagonjwa, Kijiji cha samunge kimevamiwa na majambazi na wezi ambao wameanza kuwaibia watu, nawaomba walioiba vitu hivyo wavirejeshe na waondoke kwa amani katika Kijiji hiki haraka kabla Mungu hajaanza kuwaadhibu kwa mkono wake,” alisikika akiwatangazia wananchi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati watu waliokuwa wamefurika wakianza kupata dawa ghafla vijana wawili wakiwa wamefuatana na mama mmoja ambae jina lake halikufahamika mara moja walifika eneo la Mchungaji Ambilikile anakotolea dawa na kuomba msaada wake kuhusu kijana aliyekuwa analalama kuwa anapigwa na ambao hawaoni.

Kufutia hali hiyo, mchungaji Mwasapile alimwambia Kijana huyo aliyejulikana kwa jina moja la Joseph asalimishe vitu vyote alivyoviiba na kisha ampe dawa na baada ya kutoa simu aina Black Berry, fedha Sh. 20,000 za Kenya, hati ya kusafiria sh. 80,000 za Tanzania mchungaji alimmwagia dawa na ghafla alianza kuona na kuacha kupiga kelele.

Imebainika kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Joseph (28) alikuwa ametokea mkoani Singida na Mama yake ambaye ni mchuuzi wa Chakula eneo hilo.

Monday, April 4, 2011

Dk. Migiro amtembelea JK Ikulu kwa mazungumzo


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akipeana mkono na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam. Dk. Migiro alifanya mazungumzo na Kikwete ikulu Aprili 4, 2011. Picha na Mdau Fredy Maro.


Naibu Katibu Mkuu wa UN, Dk. Migiro akiwa katika picha ya pamoja na Rais Kikwete Ikulu ya Dar es Salaam,  Dk. Migiro aliambatana na maofisa wengine kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa. 

Wanaooteshwa kuvumbua dawa ya magonjwa sugu waendelea kujitokeza



Haya makubwa: Huyu naye ameibuka mjini Morogoro yeye anatoa kikombe kimoja kama dawa ya magonjwa sugu, anajulikana kama Fatma Said Senga (41) mkazi wa Kata ya Kichangani Morogoro. Hapa katembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Said Mwambungu na viongozi wengine, kikombe chake anauza kwa sh. 200. Haya kazi Kwenu wadau, geuzeni msafara kuelekea Mji kasoro Bahari.

Friday, April 1, 2011

Wakumbuka vita vya Tanzania na Uganda?


Miongoni mwa majengo ya awali ambayo Nduli Iddi Amin Dada aliyalipua nchini Tanzania kabla ya kuzuka kwa vita vya Tanzania na Uganda. Jengo hili lilikuwa kanisa eneo la Kagera, Tanzania. Mdau Mkuu wa HM alitembelea maeneo hayo hivi karibuni.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...