Thursday, April 28, 2016

WANAKIJIJI ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wanakijiji cha Itobo, Itirima.

 Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu.

 Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania.

Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini. "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia,

" alisema Meena. Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.

Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo, akifunga rasmi Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) leo jijini Dar es Salaam.  

Mwenyekiti wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Geofrey Semu akizungumza katika mkutano wa THERIA leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioshirikisha wanachama wa THERIA kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania umefanyika kwa siku mbili mfululizo, Aprili 27 na 28, 2016 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili.

Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wake kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa THERIA uliofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akimkabidhi cheti cha shukrani mmoja wa wanachama waanzilishi wa THERIA kwa kufanikisha mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akikabidhi cheti cha shukrani kwa baadhi ya wanachama waliojitoa kufanikisha mkutano wa THERIA.


Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.
  
Sehemu ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa katika mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS)leo jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (hayupo pichani) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es Salaam.

Picha ya pamoja kati ya Wanachama wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) wakiwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (katikati mwenye suti ya kijivu) pamoja na viongozi wa chama hicho na wageni wengine waalikwa.

Picha ya pamoja kati ya meza kuu, mgeni rasmi na viongozi na kamati ya mkutano huo.

DC Moshi Atembelea Maeneo Yaliyozungukwa na Mafuriko...!

Maeneo mbalimbali, zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharibika.

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.


Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali.


Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka.


Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko.


Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya.


Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya.


Maashamba yamejaa maji.


Maeneo mengine barabara hazipitiki hali inayochangia wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kushindwa kupata huduma za kibinadamu.


Eneo la Mabogini pia liliathirika na mafuriko ingawa yalikuwa ni ya muda mfupi.


Sehemu ya mji wa Moshi unavyoonekana kwa juu. Picha na Dixon Busagaga, Kilimanjaro.

Tuesday, April 26, 2016

Tumbuatumbua ya Rais Dk Magufuli Yatua TCRA Mkurugenzi Mkuu, Bodi Nje

Muonekano wa Jengo la Makao Makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016

Polisi Kilimanjaro Yakamata Shehena Kubwa ya Dawa za Kulevya na Silaha

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, kamishna msaidizi, Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.

Kamnad wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto 4500 pamoja na kilogramu 10 za bhangi ambayo haijasokotwa iliyokamatwa wilaya ya Siha baada ya wahusika kuitelekeza.

Sehemu ya Bhangi iliyokamatwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha vifaa mbalimbali yakiwemo mapanga na mashoka yaliyokuwa yakitumika katika utekaji wa magari wilayani Mwanga.

Baadhi ya vitu mbalimbali walivyokamtwa navyo watuhumiwa wa ujambazi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha bastola ambayo inadaiwa kutumika katika kufanyia uharifu.

Kamanda wa Polisi akiwaonesha watuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi namna ambavyo wamebuni mbinu mpya ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa za kamanda Mutafungwa.

Baadhi ya askari Polisi pia walikuwepo kuimarisha usalama katika chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro. Picha na Dixon Busagaga, Kilimanjaro.

Friday, April 15, 2016

Magari Kuanza Kuvuka Bure Aprili 16, 2016 Daraja la Kigamboni...!

Daraja la Kigamboni


MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.  Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni.  Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.

Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.  Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.

Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
1)     Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
2)     Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3)     Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
4)     Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5)     Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.

Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.

Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

14 Aprili, 2016

Uzazi Bila Mpango Unavyoathiri Nguvu Kazi ya Taifa...!

Thursday, April 14, 2016

NMB Yasaini Mkataba na MCFKutoa Mikopo kwa Hospitali Binafsi

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Ukopeshaji Vifaa vya Afya Hospitalini (MCF), Bi. Monique Dolfing- Vogelenzang (kushoto) kwa pamoja wakisaini mkataba wa makubaliano na kushirikiana kuzikopesha Hospitali na Vituo vya Afya Binafsi vifaa kwa ajili ya kuviwezesha kutoa huduma. Katika Makubaliano hayo NMB itatoa mikopo nafuu kwa Hospitali zinazohitaji baada ya kuratibiwa na MFC. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Ukopeshaji Vifaa vya Afya Hospitalini (MCF), Bi. Monique Dolfing- Vogelenzang (kushoto) wakibadilishana nakala za mikataba mara baada ya hafla ya kusaini mikataba hiyo kumalizika, Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna ambavyo Hospitali Binafsi ziotakavyonufaika na mikopo nafuu ambayo itatolewa kwa wahitaji mara baada ya kupata mafunzo na ushauri toka kwa mfuko wa MCF. Kulia ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja wadogo Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa MCF, Bi. Dolfing- Vogelenzang. Mikopo inayotolewa itaanzia USD 15,000/- hadi USD 1,000,000/- kulingana na mahitaji ya kituo au hospitali yenyewe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Ukopeshaji Vifaa vya Afya Hospitalini (MCF), Bi. Monique Dolfing- Vogelenzang (kushoto) wakibadilishana nakala za mikataba mara baada ya hafla ya kusaini mikataba hiyo kumalizika, Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja wadogo Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela akishuhudia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna ambavyo Hospitali Binafsi ziotakavyonufaika na mikopo nafuu ambayo itatolewa kwa wahitaji mara baada ya kupata mafunzo na ushauri toka kwa mfuko wa MCF. Kulia ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja wadogo Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa MCF, Bi. Dolfing- Vogelenzang. Mikopo inayotolewa itaanzia USD 15,000/- hadi USD 1,000,000/- kulingana na mahitaji ya kituo au hospitali yenyewe.

Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja wadogo Benki ya NMB, Abdulmajid Nsekela kizungumza na wanahabari kuelezea namna hospitali binafsi zinavyoweza kunufaika na mkataba wao na MCF. Kushoto akifuatilia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker. Mikopo inayotolewa itaanzia USD 15,000/- hadi USD 1,000,000/- kulingana na mahitaji ya kituo au hospitali yenyewe.

Maofisa wa Benki ya NMB na Mfuko wa MCF wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mikutano wa NMB baada ya kumaliza kusaini hati za makubaliano.  Katika utaratibu huo NMB itatoa mkopo kuanzia USD 15,000/- hadi USD 1,000,000/- kulingana na mahitaji ya kituo au hospitali yenyewe.


SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...