Thursday, March 31, 2016

TCRA Waipa Leseni Kampuni ya Agano Safi

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao 'malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya leseni.

Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.

Alisema kampuni hiyo inayoundwa na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake nchini Namibia.

Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu kibiashara.


Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi (kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kukabidhi leseni ya biashara kwa Kampuni ya Agano Safi itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali' (Digital Payment Services). 

Picha ya pamoja baina ya viongozi wa pande zote mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi.

Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu, Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria, Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka, Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba pamoja na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.

Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo.

Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Agano Safi, Cuthbert Mhilu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MobiPay, Amos Shiyuka (kulia).

Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.

Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika.







Tuesday, March 29, 2016

Waziri Prof Mbarawa Ahimiza Taasisi Kutumia Kituo cha Taarifa cha Taifa

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao.

Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Adin Mgendi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa usalama mkubwa wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumza na wadau hao juu ya matumizi ya kituo hicho kuhifadhia taarifa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya matumizi ya 'National Information Data Centre'

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali juu ya kukitumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ili kuhifadhia taarifa zao. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura pamoja na Ofisa Mkuu Idara ya Ufundi TTCL, Senzige Kisonge wakifuatilia mazungumzo hayo. 

Mkuu wa Idara ya Compyuta NSSF, Yahaya Madenge (kulia) akiuliza swali kupata ufafanuzi juu ya usalama wa Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi akiuliza kupata ufafanuzi juu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi na kumlinda mteja wake.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye tai ya mistari miekundu) akizunguka na baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali vitengo vya IT kuwaonesha miundombinu ya Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' ilivyojengwa kisasa kumlinda mteja wake na taarifa zinazohifadhiwa katika kituo hicho.

Baadhi ya mashine kubwa za kisasa za kufua umeme katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Baadhi ya mitungi ya gesi ya kuzimia moto endapo ukitokea inayofanya kazi kwa kujiongoza yenyewe mara tukio la moto linapojitokeza katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi moja ya vyumba maalumu vya usalama katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (katikati) akimuonesha Meneja Uendeshaji Mifumo ya Taarifa toka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Injinia Suzanne Kyaruzi (kulia) moja ya mitambo ya kisasa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Baadhi ya mitambo ya kuhifadhia taarifa katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre'.

Baadhi ya mashine zinazofanya kazi ya kupooza mitambo katika Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam wakati Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipozungumzia wadau hao kutumia Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kuhifadhia taarifa zao.

Friday, March 18, 2016

MWENYEKITI UWT DAR ES SALAAM AWANYOSHEA KIDOLE WALIOKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi, akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana, katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Maliaga.
 Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.

Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

"Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.

Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.

Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA DULA LA MSD WILAYANI CHATO


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.


Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato. 

MRATIBU MKAZI UN ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO RUFIJI

Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa shamba la muhogo huku wakiangalia shina la muhogo mchanga kabla ya kukomaa. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa shamba la muhogo huku wakiangalia shina la muhogo mchanga kabla ya kukomaa.Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (kushoto) wakiangalia sehemu ya tawi la mmea wa muhogo uliopo shambani walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wa mihogo Wilaya ya Rufiji jana. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (kushoto) wakiangalia sehemu ya tawi la mmea wa muhogo uliopo shambani walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wa mihogo Wilaya ya Rufiji jana.[/caption] MRATIBU Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania (UN), Alvaro Rodriguez amefanya ziara ya kutembelea mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani kuangalia namna kiwanda hicho kinavyo ongeza thamani za zao la muhongo na kuboresha kipata cha wakulima. Katika ziara hiyo, Bw. Alvaro Rodriguez aliongozana na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika ambaye shirika lake limekubali kusaidia kukiendeleza kiwanda hicho kupata mashine ya kisasa pamoja na uwezo wa nguvu kazi kuongeza ufanisi wa kiwanda. Akizungumza katika kiwanda hicho, Bw. Malika alisema UNCDF imekubali kukisaidia kiwanda hicho ili kuinua hali ya kipato cha wakulima wa zao la muhogo wa Wilaya ya Rufiji ambao tayari walianza kuzalisha mazao hayo kwa kukitegemea kiwanda cha 'African Starch Project' ambacho kilisimamisha uzalishaji kutokana na uwezo mdogo wa mashine zake. "...UNCDF tumekubali kutoa mtaji wa kuanzia pamoja na kuwezesha nguvu kazi ili kiwanda kiweze kujiendesha kibiashara na kuendelea kuwanufaisha wakulima wa zao la muhogo eneo hili...tayari wamehamasika na kilimo hiki baada ya kuletwa kwa mradi huu sasa tunataka kuuongezea nguvu zaidi," alisema Kiongozi na Mshauri wa Ufundi wa Shirika la UNCDF, Malika. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana. Kulia ni Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana. Kulia ni Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika.Mtaalamu wa Mawasiliano, Ushirikiano na Utafutaji Mitaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Jacqueline Namfua akiwatambulisha Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana. Mtaalamu wa Mawasiliano, Ushirikiano na Utafutaji Mitaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Jacqueline Namfua akiwatambulisha Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana.[/caption] Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape waendeshaji wa mradi huo alisema kwa sasa wakulima zaidi ya 500 wa zao la muhogo wameanza kunufaika na mradi huo ambao wamekuwa wakitegemea kukiuzia kiwanda muhogo wa kuchakata jambo ambalo limekuza kipato chao. Alisema ufadhili wa UNCDF utakapokamilika kimtaji katika kiwanda chao zaidi ya wakulima 7000 watakuwa wakinufaika ndani ya miaka miwili, ambapo zao wanalolilima litaitajika kwa wingi kiwandani hivyo kuboresha hali za kiuchumi kwa jamii, lakini lengo kwa hapo baadaye ni kuhakikisha wakulima 10000 wananufaika na shughuli nzima za mradi huo wa kiwanda. Aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya vijiji 20 wilayani Rufiji vinavyozunguka kiwanda hiko wananchi wake wapo tayari kufanya biashara ya kilimo kukipatia kiwanda muhogo wa kuchakata, ambapo watakuwa wakishiriki kuwawezesha wananchi katika vikundi ili waweze kufanya uzalishaji wa kutosha kiwandani. Kwa upande wao baadhi ya wakulima wakiwemo akinamama waliozungumza katika ziara hiyo wamelishukuru shirika la UNCDF kwa kufadhili kiwanda hicho kwani tendo hilo limewahakikishia upatikanaji wa soko la uhakika kwa zao la muhogo, ambalo hapo awali lilikuwa likilegalega kutokana na kupoteza kiasi kikubwa cha mabaki ya zao hilo. UNCDF inategemea kutumia takribani shilingi milioni 400 kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo eneo hilo. Ziara ya viongozi hao ambao waliambatana na wajumbe wa manamawasiliano wa mashirika ya umoja wa mataifa iliwafikisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji na kufanya mazungumzo na viongozi wa halmashauri kujua changamoto anuai za kijamii. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda.Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezio. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezio.Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezio. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezio.Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda.Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (kushoto) akielezea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kutoka kulia wanaomsikiliza ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja, Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez. Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (kushoto) akielezea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kutoka kulia wanaomsikiliza ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja, Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez.Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF. Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF.Ujumbe huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono). Ujumbe huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).Ujumbe huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono). Ujumbe huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho (hawapo pichani) namna bidhaa aina ya Starch na unga wa muogo unavyozalishwa mara baada ya kuchakata muhogo. Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho (hawapo pichani) namna bidhaa aina ya Starch na unga wa muogo unavyozalishwa mara baada ya kuchakata muhogoMkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF. Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF.Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu  akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani. Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo. Mratibu Mkazi na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na baadhi ya wanahabari na ujumbe wa wanamawasiliano (hawapo pichani) baada ya ziara ya kukitembelea kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo eneo la Bungu Wilaya ya Rufiji jana. Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na baadhi ya wanahabari na ujumbe wa wanamawasiliano (hawapo pichani) baada ya ziara ya kukitembelea kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo eneo la Bungu Wilaya ya Rufiji jana.Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu  akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani. Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo 'African Starch Project' kilichopo Kata ya Bungu akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Rodriguez pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika wakitembelea moja ya mashamba ya zao la muhogo wilayani Rufiji jana. Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Rodriguez pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika wakitembelea moja ya mashamba ya zao la muhogo wilayani Rufiji jana.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...