Sunday, June 19, 2011

Angalia maharusi hawa walivyopendeza


Je, ulibahatika kuhudhuria harusi hii au unawajua maharusi hawa, waweza kujishindia zawadi! tutumie majina ya maharusi hawa, kanisa ilipofungwa ndoa hii, tumekurahisishia kwa kukutajia tarehe iliyofungwa ndoa yaani Aprili 30, 2011.


Maharusi hao wakiwa katika picha ya pamoja na kamati iliyoandaa hafla yao, siku ya harusi. (Picha na mpiga picha wa harusi na matukio)

Harusi ya Zakayo Majura na Jasmine Ngongolo


Bwana harusi Zakayo Majura (kulia) akiwa na mkewe Bi. Jasmine Ngongolo baada ya kufunga ndoa yao Juni 04, 2011 katika Kanisa Katoliki la St. Martha Dar es Salaam. Sherehe ya harusi hiyo ilifanyika Ukumbi wa Budget Resort - Kunduchi Beach. Ujumbe: "From sunrise to sunset, forever a whisper of love. Congratulations on your marriage, Majura!"

Bibi harusi Jasmine Ngongolo akiwa na wapambe wake katika picha ya pamoja. Duh, cheki walivyopendeza!


Baadhi ya wageni waalikwa wakisakata rumba pamoja na maharusi wao. IIikuwa kazi kweli kweli ndani ya Ukumbi wa Budget Resort - Kunduchi Beach.


Zakayo Majura (kushoto) akiwa na Jasmine Ngongolo wakiondoka ukumbini mara baada ya kumalizika kwa hafla yao, nyuma ni wasimamizi wao wakiwasindikiza. (Picha zote kwa hisani ya Blog ya Harusini)


Tuesday, June 14, 2011

Harusi ya Humphrey Milinga na Voronica Mande


Bwana Harusi Humphrey Millinga akiwa katika pozi na mke wake Voronica Mande wakionyesha vyeti vya ndoa baada ya kufunga ndoa yao Desemba 8, 2008 katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay na baadaye kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam.


Bwana Harusi Humphrey Millinga akiwa katika pozi na mkewake Voronica Mande baada ya kufunga ndoa yao katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay na baadaye kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam.


Send Off ya JAQUILINE


Bibi harusi mtarajiwa Jaquiline kushoto na matron wake Herieth wakipozi kwa picha wakati wa sherehe ya Send off ya Jaquiline inayofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Banora Mlimani City jijini Dar es salaam kama mnavyoona wadau Jaquiline na Herieth wakiwa wamependeza kwelikweli.


Bwana Harusi mtarajiwa Stanford kulia na Bestman wake Kevin wakipozi kwa picha wakatiwa send off ya mke wake mtarajiwa ilinayofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Banora Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Madada wa Jaquiline wakimsindikiza bibi harusi mtarajiwa wakati akiingia ukumbini tayari kwa kuanza kwa sherehe hiyo ya Send off.


Baadhi ya marafiki wa Stanford wakiongozwa na Charles (kushoto) wakiwa katika hafla hiyo. (Picha zote kwa hisani ya Full Shangwe Blog)





Thursday, June 9, 2011

Mkulo asoma bajeti ya Serikali 2011/2012; daladala, wapenda starehe kuumia

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo

BAJETI ya fedha ya mwaka 2011/2012 imeonesha kutoa matumani makubwa kwa mwananchi wa kawaida kutokana na dhamira ya Serikali kupunguza ukali wa maisha huku ikitangaza vipaumbele vyake ni umeme, maji, miundombinu, viwanja vya ndege, kuinua kilimo cha umwagiliaji na kupanua ajira.
 
Katika bajeti hii mpya Serikali inatarajia kutumia zaidi ya trilioni 13.5 ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi ya ile ya mwaka 2010/2011 ambapo ilitumia trilioni 11.1; bajeti ambayo ilipingwa na wabunge wa upinzani jambo ambalo halikufua dafu dhidi ya uwingi wa wabunge wa chama tawala.

Akisoma bajeti hiyo jana bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema kiujumla bajeti imelenga kupunguza ukali wa maisha kwa Mtanzania, kwa kuangalia kodi na tozo ambazo zimekuwa zikichangia kupanda kwa gharama za vitu mbalimbali muhimu.

“Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi pamoja na misingi na sera za bajeti, sura ya Bajeti inaonesha kwamba jumla ya shilingi bilioni 13,525.9 zinahitajika kutumika katika kipindi cha 2011/12.

 Alisema Serikali inatarajia kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya jumla ya sh. bilioni 6,775.9, sawa na asilimia 17.2 ya Pato la Taifa. Aidha, mapato kutoka vyanzo vya Halmashauri ni sh. bilioni 350.5. Kadhalika, kukopa kiasi cha sh. bilioni 2,475.9…,” alisema Mkulo.

Alisema kutoka kwa washirika wa maendeleo wanatarajiwa kuchangia bajeti kupitia misaada na mikopo ya jumla ya sh. bilioni 3,923.6. na kati ya fedha hizo, sh. bilioni 869.4 ni misaada na mikopo ya kibajeti huku sh. bilioni 3,054.1 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ikijumuisha mifuko ya kisekta.

Katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine, Serikali imeendelea kuwakamua watumiaji sigara na bia kwa kuongeza kodi ukilinganisha na ile ya mwaka wa fedha uliopita; huku kwa watakaofanya makosa ya barabarani sasa kutakiwa kulipa sh. 300,000 badala ya sh. 20,000.
 
“Kumekuwepo na changamoto ambazo zinahitaji hatua za maksudi kuchukuliwa na wadau ikiwemo Serikali, sekta binafsi na mwananchi mmoja mmoja ili kupunguza makali ya maisha kwa mwananchi.
 
“Kasi ya ongezeko la bei za bidhaa na huduma nchini pamoja na mambo mengine inasababishwa na kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia. Kutopatikana kwa umeme wa uhakika nalo ni tatizo lingine pamoja na upungufu wa chakula nchini. Hivyo Serikali itachukua hatua za kukabiliana na hiyo,” alisema Mkulo.
 
Akifafanua namna ya kupunguza ukali wa maisha Mkulo alisema bajeti ya mwaka wa 2011/2012 imeangalia maeneo mbalimbali muhimu na kuyafanyia marekebisho kwa maslahi ya Taifa ambapo, ili kupunguza bei ya mafuta, Serikali imeamua kufanya mapitio ya namna ya kuondoa tozo zinazotozwa na mamlaka mbalimbali kwa lengo la kupunguza kodi.
 
Waziri Mkulo alisema Serikali inakamilisha taratibu za ununuzi wa mafuta kwa wingi kwa lengo la kuyauzia kampuni ya usambazaji kwa bei ya jumla kufanya yatakavyo. Kanuni zitatoa muongozo katika uagizaji mafuta kwa pamoja zimekamilika na utaratibu huo unategemea kuanza kati kati ya mwaka wa fedha wa 2011/2012.
 
“Utaratibu huu unatarajiwa kupunguza bei na gharama za usafirishaji wa mafuta hayo. Pamoja na juhudi hizi za Serikali, sekta binafsi inahimizwa kuwezesha upatikanaji wa huduma ya kutumia gesi kama nishati mbadala wa mafuta ya petroli hasa mijini. Ni matarajia yangu hatua hizi zitaleta unafuu wa bei ya mafuta na hivyo kupunguza gharama za maisha,” alisema Mkulo.

Friday, June 3, 2011

Harusi ya Henry Mrutu na Mandarine Lewis


Wakiwa na nyuso za kutafakari maisha mapya ya ndoa ni Henry Mrutu na Mandarine Lewis baada ya kufunga ndoa, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Sinza jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika Ukumbi wa Serengeti Ball room hoteli Mai 28, 2011 Dar es Salaam. Bwana harusi ni mfanyakazi wa Paradise City Hotel. (PICHA NA MDAU KASSIM MBAROUK)

Harusi ya Kizega Kizega na Zawadi Muhidin

Wakionesha ishara ya upendo kwa kugongesha glasi zenye mvinyo ni maharusi, Kizega Kizega na Zawadi Muhidin, wakati wa hafla ya harusi yao iliyofanyika nyumbani kwa bwana harusi Chamazi Dar es Salaam Mai 30, 2011. (PICHA NA MDAU HAMISI MUSSA)

Happy birthday Lissa Alphonce

Mtoto Lissa Alphonce (kulia), akiwalisha keki watoto wenzake wanaoishi katika makao ya Watoto Yatima Kurasini, ikiwa ni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Mai 30, 2011 Dar es Salaam. Anaye msaidia kukata keki ni mama yake. (PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE)

Kwa heri ya kuonana Teddy Pesa


Familia ya Caristo Pesa wakiwa na furaha wakati wa hafla ya kumuaga binti yao, Teddy Pesa (Aliyekaa mbele), iliyofanyika Ukumbi wa New Vijana Kinondoni Dar es Salaam Mai 30, 2011. (PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE)

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...