Sunday, May 29, 2011

Siku Deogratius Temba alipofunga ndoa na Sylvia Rwanyamva

MAI 21, 2011 itabaki kuwa kumbukumbu ya milele kwa mwanahabari Deogratius Temba mkewe Sylvia Rwanyamva baada ya kufunga pingu za maisha.
Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofayika katika Ukumbi wa King Palace Sinza Kamanyora.



Deogratius Temba akiwa na mkewe Sylvia katika pozi eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam mara baada ya kufunga ndoa Mai 21, 2011.




"Riambe, riamaye..." "Kunywa baba, kunywa mama..." Kwa mila za kichaga anakotoka bwana harusi ukikaribishwa nyumbani kiheshima lazima upewe pombe aina ya mbege unywe kidogo. Hapa maharusi wakinywa mbege baada ya kuingia ukumbini kukaribishwa uchagani.

Cheki pozi hili...duh, wanapendeza, Mungu aendelee kuwalinda mkae katika upendo milele. 
********
Bwana harusi ni Ofisa Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) huku mkewe ni mfanyakazi wa Benki ya Access Tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Blog ya Harusi na Matukio inawapongeza na kuwatakia maisha mema, marefu na yenye mafanikio.



Wednesday, May 18, 2011

Ajali ya kutisha Geita, watu 15 wafa, 67 wajeruhiwa vibaya

Geita
WATU 15 wakiwemo watoto wawili, askari polisi mmoja wa jijini Mwanza wamepoteza maisha na wengine 67 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Sheraton lenye namba T 268 AJC na basi la Bunda Expres namba T 810 BDW baada ya kugongana uso kwa uso eneo la Kijiji cha Chibingo Wilaya ya Geita mkoani Mwanza.

Ajari hiyo ambayo imetokea jana mjini hapa majira ya saa tatu asubuhi eneo la barabara kuu ya Mwanza-Bukoba imehusisha mabasi mawili na roli la mizigo aina ya Fusso namba T 823 BDV baada ya basi la Sheraton lililokuwa likitoka Ushirombo Shinyanga kwenda Mwanza, kutaka kulipita lori lililokuwa likipanda kilima cha Chibingo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio wamesema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi wa madereva wa mabasi hayo huku yule wa basi la Sheraton akitupiwa lawama kwa kushindwa kufuata sheria za barabarani kutokana na kutaka kulipita gali lililokuwa kwenye kilima bila kuhofia atari yoyote eneo hilo.

“Tulikuwa tukitokea Shinyanga kwenda Mwanza na basi la Sheraton tulipofika Kijiji cha Chibingo dereva wetu alijalibu kulipita gari la mizigo, lakini alishindwa kulimudu gari kisha kugongana uso kwa uso na basi la
Bunda hali iliyosababisha vifo...huu ni ukiukaji wa sheria za barabarani,” alisema, Yunusu Mathias.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita, Dk. Abdallah Dihenga amethibitisha kupokea miili 15 na majeruhi zaidi ya 60 na kuongeza kati yao watu sita wamepelekwa katika hospital ya rufaa ya Bugando Mwanza baada ya hali zao kuwa mbaya.

Alisema madaktari wanaendelea kuwahudumia majeruhi hao na hali zao zinaendelea vizuri baada ya wengine saba kutibiwa na kuruhusiwa, huku akiwataka ndugu, jamaa na marafiki kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kutambua  miili ya marehemu ambao wamehifadhiwa chumba cha maiti hospitalini hapo.  

Kutokana na ajali hiyo mamia ya wananchi wamefulika katika eneo la tukio wakisaidia kutoa miili ya marehemu na majeruhi katika magari yaliyo gongana uso kwa uso licha ya zoezi hilo kuwa gumu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutoklea huduma ya kwanza.

Sunday, May 15, 2011

Harusi ya EDSON Ishengoma na JOVINA John

Edson Ishengoma (wapili kushoto) akiwa na mkewe Jovina John (wa pili kulia) pembeni mwao ni wasimamizi wao.


Edson na mkewe Jovina wakipiga picha ya ukumbusho na mama mzazi wa bwana harusi, Geraldina Ishengoma (wa kwanza kulia) muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa Katoliki Tegeta jijini Dar es Salaam. Waliosimama mbele ni wapambe wa harusi hiyo. 


Katika harusi nyingi ni mara chache hii kutokea, Pichani Bwana harusi Edson akimuendesha mkewe, wakiwasili katika Ukumbi wa Camp David Tegeta jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo hafla hiyo kabambe ilipofanyika Mei 14.

Dani ya Ukumbi wa Camp David; hapa ndio mahali maalumu ambapo maharusi waliketi.

Wapambe wa maharusi wakisafisha njia kuingia ukumbini kabla ya kuingia maharusi, Edson na Jovina.

Edson na mkewe Jovina wakiingia ndani ya Ukumbi wa Camp David kwa staili ya aina yake.


Mwanamama maalumu aliyeandaliwa akishusha baraka (sala) ndani ya ukumbi kabla ya shughuli za hafla hiyo kuendelea.


Mratibu wa hafla hiyo (floor manager), Bw. Samuel akiwakaribisha rasmi wageni waalikwa kwenye hafla hiyo, pembeni yake ni msema chochote maharufu, DC Kashasha (MC) ambaye ndiye alieongoza shughuli nzima ukumbini. 



Mama Geraldina Ishengoma akishauriana jambo na shangazi yake na Edson, Mrs Ewald Mushi. 


Picha ya kushoto ni dada wa bwana harusi, Janeth Ishengoma (wa kwanza kulia) akiingia ukumbini. Picha ya kulia Janeth akimpongeza mama yake, Geraldina Ishengoma baada ya kutoa nasaha kwa maharusi.



Wasimamizi wa harusi ya Edson na Jovina wakiwa katika pozi ukumbini.


Meza ya wazazi wa bwana harusi, Edson


Baadhi ya wageni waalikwa wakifurahia moja ya matukio katika hafla hiyo


Baadhi ya ndugu wa bwana harusi, Edson wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla hiyo




Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea na utaratibu wa 'kata mti panda'. Juu yao ni moja ya screen kubwa ambazo zilikuwa pande mbalimbali za ukumbi huo zikionesha matukio yote 'live' wakati hafla ikiendelea.
Picha zaidi za harusi hii tembelea gazeti la mtandao:- http://thehabari.com/ mtandao mshirika wa Harusi na Matukio. Lakini kama una picha za harusi tutumie matukio@thehabari.com


Saturday, May 14, 2011

Rais Museveni aapishwa Uganda, JK ashuhudia kiapo





Rais Yoweri Kaguta Museveni akila kiapo cha urais katika sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda jana huku mkewe Mama Janeth Museveni akishuhudiaRais Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na Rais mstaafu wa Kenya Mzee Daniel arap Moi wakati wa sherehe za kuapishwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda zilizofanyika katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda Mai 11, 2011. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



Thursday, May 12, 2011

JK awasili Uganda kushuhudia kuapishwa kwa Museveni


Rais Jakaya Kikwete akipokelewa kwa maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe Uganda tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni. Marais wengine waliowasili Kampala jana ni pamoja na Goodluck Jonathan wa Nigeria na, Robert Mugabe wa Zimbabwe na viongozi wengine na wawakilishi wa marais walitarajiwa kuwasili baadaye kuhudhuria sherehe hizo. (Picha na Freddy Maro)

Tuesday, May 10, 2011

Mashindano ya KBC East African Tour 2011 yazinduliwa Arusha


Mwenyekiti wa Mchezo wa Golfu Arusha Gymkana Clab, Richard Gomes akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya KCB East African Tour  2011, mashindano hayo yanatarajia kuanza leo katika viwanja vya Gymkana mjini Arusha. (Picha hii imetumwa na mdau Janeth Mushi wa Arusha)

Monday, May 9, 2011

Serikali yafanya semina elekezi Dodoma

Rais Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Semina Elekezi ambao ni viongozi na watendaji wakuu wa taasisi na idara za Serikali, mjini Dodoma Mai 9, 2011.


Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo (katikati) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa. baada ya ufunguzi wa Semina Elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali.


Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (katikati) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa wakati wa semina hiyo.

Mgeni wa Blog ya Harusi na Matukio

Karibu mgeni! Wadau hapa vip?

Mwanahabari Amiri Mvungi auaga ukapera


Mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo mkoani Arusha,  Amiri Mvungi akiwapungia mkono wageni waalikwa (hawapo pichani) pamoja na mkewe Sophia Atwaa, mara baada ya kufunga pingu za maisha hivi karibuni wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.


Mr. Mvungi akiwa na mkewe Sophia wakati hafla ya kukata na shoka ikiendelea ukumbini.


Mvungi wakiwa na mkewe katika mapozi kabla ya hafla yao rasmi. Picha zote na mdau Janeth Mushi wa A-town. Blog ya HM inawatakiwa kila lililo heri katika maisha mapya ya ndoa yenu.


Siku mtangazaji Ssebo alipopata jiko la milele


Mtangazaji Abdulhakim Busulwa a.k.a Ssebo akiwa na mkewe Tahjir Siu Busulwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika kwenye Hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salam hivi karibuni. Picha kwa hisani ya maharusi.

Thursday, May 5, 2011

Harusi ya mwana Mfalme Prince William na Kate Middleton

Ilikuwa ni harusi ya kifahari;

Aprili 29 itabaki kuwa siku ya kumbukumbu ya milele kwa wanandoa Prince William pamoja na mkewe Catherine (Kate) Middleton baada ya kufunga ndoa yao ya kifahari iliyogharimu mamilioni ya paundi za Uingereza.

Harusi hiyo iliyoudhuriwa na umati mkubwa wa viongozi na watu maarufu inakadiriwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha kuliko harusi zilizowahi kufungwa ulimwenguni. Zaidi ya watu bilioni mbili kutoka nchi mbalimbali walikuwa wakiishuhudia kupitia luninga zao. Zifuatazo ni picha mbalimbali za harusi hiyo:-


Kate akiwasili kwenye makazi ya Mwana Mfalme, Prince William kabla ya kufunga ndoa, akiwa na msimamizi wake pamoja na baba yake Middleton.



Prince William na Kate mbele wakiingia kanisani wakiambatana na msafara wao wa harusi. 


Prince William akimvisha pete Kate kanisani mbele ya Mchungaji.


Maharusi Kate na William baada ya ndoa yao ya kifahari.



Prince William akimbusu mkewe mara ya kwanza muda mfupi baada ya kufunga ndoa. Hata hivyo taarifa zinaeleza maarusi hawa waliahirisha kwenda fungate baada ya sherehe hiyo kwa kuvikwepa vyombo vya habari. Walipanga kulifanya tukio hilo kimya kimya baadaye bila mapaparazi kuwafuatilia.



Mwanasoka maarufu duniani David Beckham na mkewe ni miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ndoa hiyo



SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...