Monday, January 31, 2011

Harusi ya Jeremiah Mayeye na Lightness Mayeye


Jeremiah Mayeye akiwa na mkewe Lightness Mayeye wakiwa na wapambe wao mara baada ya kufunga ndoa yao Agosti 29, 2009 jijini Dar es Salaam.


Jeremiah Mayeye akiwa na mkewe Lightness Mayeye baada ya ndoa yao.



Jeremiah Mayeye na mkewe Lightness wakikata keki kwa pamoja



Friday, January 28, 2011

Mkutano wa kimataifa wa afya ya akinamama, watoto

Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano wa kwanza wa Tume ya Kimataifa kuhusiana na masuala ya afya ya akinamama na watoto, akijibu maswali ya waandishi wa habari akiwa na Mwenyekiti Mwenza, Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper, baada ya Kikao cha kwanza cha tume hiyo mjini Geneva, Uswis kilichofanyika Januari 26, 2011. PICHA NA MDAU, FREDDY MARO.

Maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani



Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa kitaifa mkoani Lindi Januari 30, 2011. Picha na mdau Aron Msigwa wa MAELEZO.


Monday, January 24, 2011

Semina ya Wabunge wa CCM DAR


Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Waziri Mkuu Mstafu na mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa wakiwa katika mazungumzo wakati wa mapumziko katika semina ya wabunge wa CCM.


Makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es sa salaam leo. Kati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda. Wote walikuwa wanashiriki semina ya wa bunge wa CCM. Picha zote kwa hisani ya Blog ya MICHUZI




Basi latekwa abiria wakatwa mapanga

IMERIPOTIWA kuwa watu wanane wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Kampala nchini Uganda kwenda Dar es Salaam kutekwa na majambazi na kisha kuporwa fedha pamoja na mali nyingine.

Basi hilo mali ya Kampuni ya Falcon Excutive lenye namba za usajili T.386 AUD aina ya Nissan. Licha ya abiria kuporwa mali anuai na fedha taslimu, pia wamekatwa kwa mapanga na kupigwa kwa mawe sehemu mbalimbali za miili yao. Robo tatu ya abiria hao walikuwa ni raia kutoka nchi ya Uganda.

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa,Rajabu Muhuwila, aalisema kuwa tukio hilo limetokea jana kati ya saa tano na sita usiku katika eneo la mlima wa Sekenke uliopo kata ya Shelui wilayani Iramba.


Alisema abiria hapo akiwemo hilo aitwae Omari Mzee, wameumizwa na hali ya dereva huyo imeleezwa kuwa ni mbaya alikuwa hajitambui. ..........Taarifa kwa Hisani ya Mdau Iramba.

Friday, January 21, 2011

Ajali hizi mpaka lini?


Wananchi wakiangalia ajali ya gari dogo lililotumbukia katika mtaro eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam Januari 21, 2011. PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE.

Thursday, January 20, 2011

Waziri Chami atembelea wajasiriamali

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amewataka wajasiriamali nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya soko la bidhaa husika ili kuleta tija.
Katika ziara yake ya siku moja jijini Dar es Salaam, Waziri Chami amesema Serikali inathamini mchango wa wajasiriamali katika uchumi wa nchi na kuwaahidi ushirikiano wa serikali kuwawezesha kwa kuwatafutia fursa za mafunzo, mitaji, masoko, malighafi na maeneo ya kufanyia kazi.
Aidha, amewaahidi kuwa, wizara yake kupitia SIDO itaandaa mafunzo na baadae ziara ya mafunzo nchini India ili kuwawezesha kujifunza kwa vitendo maendeleo makubwa ya kiteknolojia yaliyofikiwa nchini India.
Ziara hiyo ilianzia Mtaa wa Gerezani Kariakoo na kuendelea Mtaa wa Tabata Dampo na kumalizikia katika eneo la SIDO Vingunguti, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wajasiriamali wanatengeneza bidhaa mbali mbali katika maeneo hayo na kubadilishana nao mawazo.
Dk. Chami amewataka wajasiriamali hao hasa wanaozalisha bidhaa za chuma kutotumia kisingizio cha ukosefu wa malighafi ya chuma  kama sababu ya kuharibu miundo mbinu ili kupata bidhaa hiyo.
Amesema Serikali iko mbioni kuanza uvunaji wa chuma ghafi katika migodi ya madini hayo iliyopo eneo la Liganga mkoani Iringa ili kuondoa kabisa tatizo la ukosefu wa chuma ghafi hapa nchini na kukomesha biashara haramu ya chuma chakavu inayovutia watu wasio waaminifu kufanya hujma ya kuharibu miundombinu.
Kwa upande wao wafanyabishara hao wameiomba serikali kutatua haraka tatizo la mgao wa Umeme na gharama kubwa za nishati hiyo zinazofanya shughulu zao kutokuwa na tija na kuiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia uwezekano wa kuwaondolea kodi kubwa wanazotozwa wajasiriamali hao.
Katika ziara hiyo, Dk. Chami aliongozona na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Dk. Adelhelm Meru, Mwakilishi wa Kamishna wa TRA, Allan Kiula na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Pius Wenga.
Habari hii na picha vimetumwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Nicodemas Mushi.


Dk. Cyril Chami wa nne kulia akitoa maelekezo katika moja ya ziara hiyo.


Waziri Chami (wa pili kulia) akiangalia moja ya mashine ya vyuma akiwa katika ziara yake.



Waziri Chami akiwa na baadhi ya maofisa alioongozana nao katika ziara yake.


Wednesday, January 19, 2011

Mchungaji adaiwa kukutwa na marehemu watatu

Tarehe: 19th January 2011

WANANCHI wa kijiji cha Nyankanga, Musoma Vijijini, mkoani Mara wamevamia kwa Mchungaji Paulo Magesa wa kitongoji cha Iginaimwe na kuchoma nyumba zake tatu na kuharibu bustani yake kwa tuhuma za ushirikina.

Tukio hilo lilitokea Januari 16 saa 3 asubuhi, wakati Mchungaji huyo alipokutwa akiwa na vijana watatu wa kijiji hicho ambao wanasadikiwa walishafariki dunia miaka mingi iliyopita.

Waandishi wa habari walifika eneo la tukio na kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi hao, lakini mtuhumiwa na familia yake hawakuwapo, kwa madai kuwa walitorokea kusikojulikana.

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, walidai kuwa Mchungaji huyo alikuwa anatoa huduma za kiroho kwa familia yake pekee alifika kijijini hapo takribani mwaka mmoja na nusu uliopita na kununua eneo la ekari zaidi ya 10 kutoka kwa Marwa Kitamara.

“Aliuziwa eneo hilo, lakini kitu cha kushangaza baada ya kuhamia vifo vya ajabu ajabu vilianza kutokea, lakini siku ya tukio alikutwa akiwa na watu waliokufa siku nyingi, kuna kijana wa Bweri na mama aitwaye Mama Asha, na mwingine hawakumfahamu jina.

“Ndipo vijana hao wakapiga yowe na kumhoji kuwa alikuwa anawapeleka wapi na wakati wakiendelea kumhoji watu hao walitoweka kusikojulikana ndipo wananchi walipopandwa hasira na kwenda kuchoma na kubomoa nyumba zake tatu na kuharibu bustani na shamba lake,” alisema Mamkama Imanyi wa Iginaimwe.

Wananchi hao walidai kuwa ilipofika saa 12 jioni aliokotwa kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 karibu na eneo la Mchungaji huyo akidaiwa ni msukule na baada ya kumhoji anatoka wapi alitaja zaidi ya vijiji vitano na jina lake halijui, ndipo wakamkabidhi kwa polisi wa doria na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi mjini hapa.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Masau Magalu, alikiri kupokea malalamiko ya wananchi kuwa Mchungaji huyo alikuwa anajihusisha na mambo ya kishirikina lakini Serikali haiamini mambo ya uchawi ingawa walikuwa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Tulishapata malalamiko kutoka kwa wananchi wetu, lakini sisi Serikali hatuamini mambo ya kishirikina, ingawa tulikuwa tunafuatilia malalamiko na jana (juzi) wananchi walimvamia kwa madai kuwa alikutwa na watu watatu akiwapeleka mjini, ndipo wakachoma na kubomoa nyumba zake tatu na kuharibu mashamba yake na sasa hatujui aliko,” alisema Magalu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, alisema: “Habari za kuchomewa na kubomolewa nyumba zake na kuharibiwa mashamba tumezipata, lakini cha kushangaza Mchungaji wa Kanisa atawezaje kuwa mchawi.

“Pia kijana ambaye wananchi wanadai kuwa ni msukule si kweli, kijana yule alikuwa amepotea njia lakini kwa kuwa alikuwa mazingira hayo, wananchi wakamhusisha na tukio hilo, lakini ameshachukuliwa na wazazi wake,” alisema Kamanda Boaz.

Kamanda aliongeza kuwa wanafanya uchunguzi wa kina kubaini wananchi waliohusika na uharibifu huo, ili sheria ichukue mkondo wake kwa kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho na mjini hapa zilisema matukio ya kuchomewa nyumba Mchungaji huyo yametokea mara nyingi kwani hata katika maeneo ya Majita, Musoma Vijijini, alichomewa nyumba na kufukuzwa kwa tuhuma hizo hizo za ushirikina.

Alihamia mjini Musoma na mwaka juzi aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari baada ya kuchomewa nyumba katika kitongoji cha Zanzibar karibu na Mlima Balima akidai kuwa alikuwa anafanya utafiti wa madini huku akijihusisha pia na masuala hayo
hayo. ……………..
                                                         Na Thomas Dominick, wa Habari Leo Musoma;

Tuesday, January 18, 2011

Harusi ya Mohamed Millanzi na Rufu Jumanne


Baadhi ya ndugu na jamaa wa Mohamed Millanzi wakimuombea dua bi harusi, Rufu Jumanne walipokuwa wakifunga ndoa Januari 14, 2011 Manzese Tip Top na kufuatiwa na hafla iliyofanyika nyumbani kwa mama yake mzazi na bwana harusi Kiwalani jijini Dar es Salaam.


Mohamed Millanzi akiwa na mkewe, Rufu Jumanne baada ya kufunga ndoa yao.

Harusi ya Ibrahim Joseph na Constasia Milinga

Bwana harusi Ibrahim Joseph na Mkewe Constasia Milinga na wapambe wao nje ya Jengo la Mkapa Tower (NSSF) tayari kwa kupiga picha za kumbukumbu baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam, Januari 16, 2011.



Wapambe wa maharusi wa harusi ya Ibrahim Joseph na Constasia Milinga



Hapa wapambe wakiwa katika mapozi mbalimbali.




Ndoa ya Ally Abdallah na Zainabu Habibu



Bw. Ally Abdallah na mkewe Zainabu Habibu wakionesha vyeti vyao vya ndoa baada ya kufunga ndoa Oktoba 15, 2011 katika Msikiti wa Mwenge na baadae kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka zilizofanyika katika Ukumbi wa Livestone  uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Friday, January 14, 2011

Kongamano la Majaji Wanawake Tanzania



Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiwa katika kongamano lao la siku moja lililofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani(kulia)akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Eusebia Munuo (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kimataifa cha Majaji Wanawake, Joan Winship (kushoto) jijini Dar es salaam kabla ya ufunguzi wa kongamano la siku moja la TAWJA. Picha zote na mdau Tiganya Vincent wa MAELEZO - Dar es Salaam.


Pengo: Sikutarajia Polisi Kuua Raia


Pengo: Sikutarajia Polisi Kuua Raia
 

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amesema
kitendo cha polisi waliopewa dhamana ya kulinda wananchi kuua watu wasio na hatia kinaashiria maafa makubwa kutokea nchini.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Dar es Salaam katika misa ya kuwaombea wafiadini wa Pugu iliyofanyika Kituo cha Hija, Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema hakutarajia jambo hilo linaweza kutokea Tanzania bara, ambako kuna historia ya kuitwa kisiwa cha amani duniani.

"Sikutegemea hata mara moja kwamba walinda usalama wanaweza kutumia silaha wakaua watu. Sikutegemea kwamba wanaweza kuua hata mtu mmoja. Wale wanapaswa kutetea uhai wa Watanzania. Wachukue silaha dhidi ya Watanzania, waue watu haidhuru wamekosaje, ni jambo ambalo sikutegemea kamwe kwamba lingeweza kutokea," alisema kardinali Pengo.

Kutokana na tukio hilo kiongozi huyo aliwataka Watanzania bila kujali madhehebu yao wasimpuuze Mungu, bali warejee kumuomba ili arejeshe amani Tanzania iliyoachwa na waasisi wa nchi hii, Mwalumu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

Kardinali Pengo alisema tukio la polisi kuua raia lililotokea Arusha kwa wananchi wasio na hatia kupigwa risasi liimetia doa Tanzania, limeipaka matope Tanzania.

Kiongozi huyo aliwataka Watanzania watambue kuwa hana lengo la kueneza hisia za chuki, woga wala hisia za aina yoyote, bali lengo lake kuwafanya watu watambue kwamba kama tumeishi kwa amani ni mwenyezi aliyetuopa amani hiyo.

"Tutambue kwamba tulipoitwa kisiwa cha amani ilitokana na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani, kama tukidhani ilitokana na nguvu yoyote ya kibinadamu tutakuwa tunajidanganya," alisema.

"Kitendo cha watu kutegemea nguvu ya silaha wakifiriki kwamba njia hiyo ndiyo italeta amani au wataweza kuleta ushindi wao, huko ni kujidanyanganya na kumtukana Mungu, kwa vile hayo ni maandalizi ya maafa makubwa kwa ajili ya taifa la Tanzania," alisema na kuongeza Mwenyezi atuepushie na laana hiyo..

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha watu watatu kuuawa kwa risasi na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, Kardinali pengo aliwataka Watanzania waungane naye kuomba ili laana inayonyemelea Tanzania kutokana kwa kumpuuza Mungu iepukwe.

Habari na Gazeti la Majira

Mdau Dotto Mwaibale ziarani Njombe

Mdau wa Blog ya Harusi na Matukio, Dotto Mwaibale akisaka matukio. Hapa anaonekana ameingia mjini Njombe kikazi zaidi na bango hili ni hoteli aliyofikia. 


Pombe ya ulanzi mjini Iringa

Wauzaji wa pombe aina ya ulanzi ambayo ni maarufu katika Mkoa wa Iringa wakisukuma baiskeli zenye pombe hiyo kutafuta wanunuzi. Picha na mdau Dotto Mwaibale ambaye alitembelea mkoa huo hivi karibuni.

Maharusi kutoka ‘majuu’


Moja ya harusi kutoka ‘majuu’. Maharusi kutoka Mji wa Vancouver nchini Canada wakiwa katika picha ya pamoja na wapambe wao baada ya kufunga ndoa.



Maharusi 'majuu' wakipata picha za kumbukumbu mara baada ya kufunga ndoa



Wageni katika harusi majuu huonekana hivi.



Kitabu cha kuwatakia heri wanandoa kwa wenzetu ni moja ya mambo muhimu 'majuu' katika kwenye harusi.







Wanamawasiliano kutoka SAUT wakiwa ufukweni

Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Kwanza ya Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustino- Mwanza (SAUT) wakiwa ufukweni mwa ziwa Victoria kwa michezo mbalimbali kwenye hafla ya kuagana.


Wanamawasiliano walicheza michezo mbalimbali pia, hapa wanavuta kamba kwa staili ya pekee wakishindana wanaume na wakinadada. Katika mchezo huu akinadada waliwashinda  wanaume.



Mdau Edson Kamukara ni mmoja wa wanamawasiliano waliomaliza SAUT, hapa anapata upepo mwanana. Picha zote na mdau Edson Kamukara.

Beach si za wazungu pekee bwana!

Mdau naomba pokea picha hii nadhani inaweza kuwavuta na wadau wengine, hatimaye kupenda kutembelea fukwe zetu. Pichani ni mdau Said Mwishehe akijivinjari pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


Said Mwishehe akitafakari pembezoni mwa ufukwe



Mdau Mwishehe akiwa pembezoni mwa Hoteli ya Double Tree



Mpiga picha maarufu, Richard Mwaikenda (Kamanda) ambaye pia ni mmiliki wa blog ya Kamanda wa Matukio akiwa katika pozi kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.  


Mdau Said Mwishehe akiwa na mdau Kilian


Harusi ya Eric Kafula na Esther Joseph


Wakitafakari jambo ni Eric Kafula na Esther Joseph wakiwa katika ibada ya sakramenti ya ndoa yao, iliyofanyika Jumamosi ya Mei 6, 2010 ndani ya Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam na kufuatiwa na tafrija ya nguvu kwenye ukumbi wa hoteli ya Beriego Ilala Bungoni. PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE

Harusi ya Ellyneema Mwasalanga na Frola Simon

Akitafakari namna atakavyoilinda ahadi yake aliyoitoa mbele ya Mungu na Kanisa ya kumpenda na kumtunza mke wake Frola Simon katika hali ya shida na raha hadi kifo kitakapo watenganisha ni Ellyneema Mwasalanga baada ya kufunga ndoa na mkewe huyo Jumamosi ya Mei 6, 2010 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam. PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE.

Harusi ya Abdallah Molanga na Khadija Salum


Maharusi Abdallah Molanga na Khadija Salum wakinyweshana divai baada ya kufunga ndoa Ilala Sharifu Shamba Dar es Salaam Novemba 6, 2010, nyumbani kwa kaka wa bwana harusi, Ibrahim Makaberi na kufuatiwa na sherehe kabambe iliyofanyika katika Ukumbi wa Msasani klabu. PICHA NA MDAU DOTTO MWAIBALE.

Thursday, January 13, 2011

Miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi mjini Zanzibar wakati sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12, 1964.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein (kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete (kushoto) wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Maziri wakuu wastaafu, Dk. Salim Ahmed Salim (kushoto) na Fredrick Sumaye (katikati) wakibadilishana mawazo na Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha (kulia) wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya mapinduzi ya Zanzibar.



Katibu wa CCM, Yusuph Makamba (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) mjini Zanzibar wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanznibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amani.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete (kushoto) wakiwa wamesimama kupokea maandamano ya wawakilishi wa wananchi kutoka mikoa mbalimbali za Zanzibar kwa ajili ya kusherekea miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Tuesday, January 11, 2011

Waziri Mkuu Pinda akutana na Balozi wa UAE

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza masuala ya kazi na Balozi wa Falme za Kiarabu (UAE), Mallalla Mubarak al Amirer, Dar es Salaam Januari 11, 2011. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Askofu RC atishiwa bastola madhabahuni

Askofu, Alfred Maluma

Monday, 10 January 2011

MWANAMKE ambaye jina lake halikufahamika, amevamia madhabahuni na kuchomoa bastola kisha kutishia kumwua askofu wa Jimbo Kuu la Njombe, Alfred Maluma aliyekuwa akiendesha ibada katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jimboni humo.

Jaribio hilo la mauaji lililozua tafrani kubwa kanisani hapo na hata kuvuruga kwa muda mwenendo wa ibada, lilidhibitiwa na padri mmoja aliyekuwapo madhabahuni hapo ambaye alimrukia mama huyo na kuikamata bastola hilo.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa tukio hilo la kwanza kutokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililoko Jimbo Kuu la Njombe, lilitokea Alhamisi iliyopita wakati wa ibada ya kusimika mashemasi. 

Kwa mujibu wa habari hizo, mwanamke huyo awali alikuwa ameketi kwenye mabenchi kama mumini wa kawaida aliyekuwa akifuatilia ibada hiyo, lakini ghafla alisimama na kufuata askofu huyo na kumnyoshea bastola hiyo. 

"Wakati wa kipindi cha mageuzo, mwanamke huyo alienda altareni na kumnyoshea bastola Askofu huyo akitaka kumuua," mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alilieleza gazeti hili na kuongeza. Baada ya kutoa bastola hiyo huku askofu akiendelea na mageuzo, padri aliyefamika kwa jina la Ngiri, alimrukia kwa haraka na kumpokonya bastola hiyo." 

Hata hivyo, habari zaidi zilieleza kuwa baada ya kuikagua bastola hilo ilikuwa haina risasi, lakini mwanamke huyo alikutwa na risasi kwenye begi lake la mkononi. 

Mashuhuda wengine walilieleza gazeti hili kuwa bastola hiyo ilifahamika kuwa ya mmoja wa mapadre wa parokia za Jimbo la Njombe (jina la parokia na padre vimehifadhiwa), lakini haikufahamika mwanamke huyo aliipataje. “Ni Mungu tu aliyesaidia kwa kuwa huyo mtuhumiwa alikuwa amedhamiria kuja kuua na akasahau kuweka risasi hivyo inatakiwa polisi litupe ufafanuzi zaidi,” alisema shuhuda mwingine wa tukio hilo. 

Jumapili iliyopita, baadhi ya mapadre walielezea tukio hilo kwenye ibada zao na kufafanua kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mwanamke huyo ana matatizo ya akili. 

Katibu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe, Erasmo Mligo alithibitisha tukio hilo, lakini akaeleza kuwa hawawezi kuzungumza chochote kwa kuwa suala hilo sasa liko mikononi mwa polisi. "Suala hilo sasa liko kwa mkuu wa upelelezi Wilaya ya Njombe hivyo sisi kama kanisa hatuwezi kuzungumza chochote zaidi ya kuthibitisha kuwa tukio limekuwapo," alisema Mligo. 

Kamanda wa Polisi wa Iringa, Everist Mangara aliliambia Mwananchi jana kuwa ana taarifa ya tukio hilo, lakini bado anafuatilia taarifa zake. "Tukio hilo nimelisikia, lakini sijalipata vizuri ila ninaendelea kulifuatia kwa karibu," alisema Mangara   

                                                                      Na Devotha John wa Gazeti la Mwananchi 



Saturday, January 8, 2011

Ndoa ya Mike Ezuruonye na Nkechi Nnorom wa Nigeria

Novemba 13, 2010 msanii wa filamu wa Nigeria Mike Ezuruonye alifunga ndoa  kanisani na mkewe Nkechi Nnorom. Pichani ni Nkechi akimvisha pete kanisani mumewe mbele ya kasisi.

Mike Ezuruonye na Nkechi Nnorom wakionesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa kanisani na baadaye kufuatiwa na tafrija kabambe nchini Nigeria. Waliosimama pembeni mwao ni wasimamizi wao.

Mike Ezuruonye na Nkechi Nnorom wakiwa katika picha na wapambe wao pamoja na wasimamizi baada ya kufunga ndoa yao


Mike Ezuruonye akimchumu Nkechi siku ya harusi yao.

Huu ndio usafiri waliotumia maharusi hawa

Ndoa ya Bw. Chutamanile na Zena Kisute

Bw. Said Chutamanile na Bi. Zena Hemed Kisute wakiwa katika pozi mara baada ya kufunga ndoa yao jijini Dar es Salaam hivi karibuni.


Bi. Zena Hemed Kisute akimchumu mumewe Bw. Said Chutamanile baada ya ndoa yao. 

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...